Kambi ya mzinga na maghorofa mafupi Morogoro

Kambi ya mzinga na maghorofa mafupi Morogoro

Habari hii nimeshaitolea ufafanuzi siku za nyuma. Lakini kwa ufupi unayesema ni Juma Kilaza siye kabisa, umekosea huyo kwenye picha aliyeshika gitaa la rythm ni Ally Saidi ambaye alikuwa Cuban Marimba, TK Lumpopo na baadae alihamia Urafiki Jazz band anayefutia kwenye picha ni Juma Bamam aliyekuwa akipiga drums sijui imekuwaje ameshika gitaa kwenye picha hii. Juma Kilaza hayupo kwenye kipande ulichoweka yeye alikuwa hapigi gitaa. Alikwa kiongozi,mwimbaji na mtunzi mkuu wa bendi ya Cuban Marimba, TK Lumpopo, Magola International na hatimaye Les Cuban kabla hajastaafu muziki na alifariki 27.02.2003
 
Moro home sweet home!
Miaka ya tisini chem chem za maji safi baridi zinatiririka mpaka mitaani!Kwa ufupi kama unavyoona mifereji ya maji machafu Dar iliyo pembenio ya barabara, basi kwa Moro ilikuwa ni mifereji ya maji safi pembeni ya barabara.
Lakini sasa mifereji yote imekauka ni vumbi tu!Kunasikitisha sana
Mjimpya, kihomda, forest, masika, misufini, modeko, sua, kilakala, sabasaba, kola!
Dah Moro enzi hizo
 
Nimezaliwa Morogoro!
Nimekulia Morogoro!
Nimesomo Morogoro secondary
Chuo pia Morogoro!
Nimeishi na wazazi wng mtaa mmoja na Mkali JUMA KILAZA (RIP)
Juma Shabaan (Yanga legend?) na ADAM SABU (SIMBA legend) walikuwa majirani zetu!
Naipenda Moro
Sijazaliwa Moro,Sema naijuwa Moro yote na vitongoji vyake na Watu Wake.
 
Nje ya mada mkuu Mfano ukiwa huna akili/ performance yako ikawa chini unaitwa kilaza
nataka kuuliza je huyu juma kilaza ndo (jina lake linatumika Kama SI-UNIT ya pumbavu) Au ni rare coincidence ?
Kilaza alikuwa mwanamuziki ambaye alishindwa vibaya na mbaraka mushehe banda ya kushindanishwa kwenye shindano la music. Hivyo tokea wakati huo ukishindwa jambo lolote unapewa jina la kilaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika mambo mengi sahihi ......marekebisho ......hiyo ngoma inaitwa *mdundiko* sio *mganda* na jina la kikundi kilichofadhiliwa na mzungu huyo ndio kinaitwa ^kudauimbe* na sio jina la huyo mzungu......pamoja na kwamba alipotea ghafla lakini alikuja kama mtafiti wa mambo ya utamaduni
 
Back
Top Bottom