MORUWASA: Bomba lililopasuka Mtaa wa Bomaroad imerekebishwa

MORUWASA: Bomba lililopasuka Mtaa wa Bomaroad imerekebishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,217
Reaction score
15,567
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imesema changamoto ya bomba lililopasuka katika Mtaa wa Bomaroad iliripotiwa na wananchi wa eneo husika imeshashughulikiwa na sasa hali ipo sawa.

MORUWASA inatoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji kwa wakati ikiwemo kupitia kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa ili changamoto hizo zifanyiwe kazi kwa wakati.

Awali, Mdau aliandika kuwa wanapata changamoto hiyo katika Wilaya ya Morogoro Mjini, Kata ya Mji Mkuu, Mtaa wa Bomaroad ambapo bomba la maji safi limepasuka, maji yanavuja na hatua hazijachukuliwa.

Hoja ya awali ~ Morogoro Mjini, Mtaa wa Bomaroad bomba limepasuka linamwaga maji safi miezi 6 hakuna anayejali
 
Back
Top Bottom