Mtalii wa Kisiasa
Member
- May 3, 2019
- 53
- 145
KAMBI YA MZINGA NA MAGHOROFA MAFUPI MOROGORO.
Leo 14:15pm,19/10/2019.
Mji wa Morogoro ambao una maghorofa machache,ni mji ambao ulikuwa mahali pa kutunza Usalama wa nchi kwani kambi kubwa za kijeshi zilipata kuwa hapo,Majengo ya maghorofa yalikuwa yasiyozidi ghorofa moja si kwamba ardhi ilikuwa si salama bali ilikuwa ni hitaji la kiusalama,rejea kisa cha "Kudaulimbe" miaka ya 1980, kaburu mzungu mcheza mganda maarufu mjini Morogoro aliyekamatwa katika Milima ya Uluguru akipiga picha kambi ya Mzinga na kuamliwa kurudi nchini kwake Afrika ya Kusini ndani ya Masaa 24.
Kisa cha kudaulimbe kinatupa usahihi wa wazo la uwepo wa nyumba za chini kwa ajili ya kuhifadhi Usalama wa nchi kupitia kambi za kijeshi ambapo ilisemekana ujenzi wa maghorofa marefu haukuwa sahihi kiusalama na ungeathiri usalama wa kambi hizo na Usalama wa nchi na kupelekea Morogoro kuwa na nyumba fupi za chini na maghorofa yasiyozidi ghorofa moja,na hili ungeweza kuliona miaka ya 1960 hadi 2000 japo hivi karibuni ujenzi wa Maghorofa marefu umeanza kuonekana mjini Morogoro.
-Uzuri wa Mji wa Morogoro.
Uzuri wa Mji wa Morogoro unafanana na mji wa zamani wa Babylon (au Babeli), Babylon inasadikika ilikuwepo eneo ambalo hivi leo linajulikana kama Al Hillah, jimbo la Babil, nchini Iraq.
Jiji hilo ambalo leo halipo lilipambwa na Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon au “Hanging Gardens of Babylon” kwa Kiingereza.Jiji hilo la Babylon au Babeli lilikuwa na maajabu yaliyokuwa yakijulikana kama “Bustani Zenye Kuning’inia za Semiramis”.
Uoto wa asili kama uliopo katika Milima ya Uluguru,Maua Waridi au Roses yaliyopatikana katika Milima hiyo na Makazi ya watu ni sawa na bustani katika vibaraza vya pembeni na kwenye mapaa ya Mji wa Babylon kiasi kwamba miti hiyo ambayo matawi yake yalikuwa yanatokeza au kuning’inia pembeni mwa majengo, ikazaa maneno “Bustani Zenye Kuning’inia za Babylon”
-Maisha na Burudani Mjini Morogoro miaka ya 1970.
Morogoro, moja ya miji iliyokuwa maarufu kwa burudani katika miaka ya hamsini, sitini na sabini. Watu walitoka Dar es Salaam na kufuata week end Morogoro. Hali yake ya hewa, na kuwepo kwa bendi mbili maarufu zilizokuwa na uwezo mkubwa zilifanya wafanyakazi watake kupangiwa vituo vya kazi Mjini Morogoro.
Tayari Wilaya mbili za Morogoro zilikuwa Miji,Wilaya ya Morogoro mjini,Wilaya ya Kilosa,Wilaya ya Morogoro Vijijini (Matombo,Kisaki na Mgeta),Wilaya ya Kilombero,Wilaya ya Mikumi,Wilaya ya Ifakara,Wilaya ya Gairo,Wilaya ya Mahenge,Wilaya ya Mvomero,Wilaya ya Malinyi,zote hizi zilikuwa na shughuli za kiuchumi na kimaendeleo na Viwanda vikubwa vya Serikali vilipata kuwemo katika Wilaya hizo toka miaka ya 1950.
Wilaya zote zilikuwa ni sehemu zinazojitegemea na Morogoro Mjini ilikuwa ndiyo Makao Makuu ya Mji na mtu akitoka kati ya Wilaya mojawapo akitaka kwenda Morogoro mjini anasema na anapanga safari kwamba anaenda Morogoro kama vile watu wanavyotoka mkoani na kwenda Morogoro.
Wakati huo kila mtu alitamani kufika Morogoro mjini,hii ilitokana na burudani murua zilizopatikama Mjini Morogoro, kwa uwepo wa bendi mbili kubwa katika Afrika Mashariki,bendi ya Cuban Marimba na Morogoro Jazz zilizoongozwa vyema na Manguli wa Muziki nchini Tanzania Salum Abdalla na vibao vyake maarufu kama "Shemeji shemeji huku wazima taa" na "Mkono wa Iddi".
Morogoro ni mji ambao uliutambulisha Muziki wa kitanzania duniani,na Magwiji awa ndio walipata kuzunguka duniani kupiga muziki wa Kitanzania,Salum Abdallah,Mbaraka Mwishehe na Juma Kilaza wao walikuwa alama ya muziki wa Kitanzania.
Kwanza kabisa Mji wa Morogoro ndio ulikuwa makao ya bendi maarufu ya Cuban marimba band chini ya mwanzilishi wake Salum Abdallah, mzaliwa wa mji wa Morogoro, Makao makuu ya bendi hiyo yalikuwa Kichangani, mjini Morogoro. Nyimbo za santuri nyingi za miaka ya 1950 na 1960 zilitungwa mjini humo. Mji huo ulikuwa makao ya bendi nyingine ya Moro jazz.
Mwaka 1968, Mbaraka Mwinshehe Nguli aliyetikisa anga la Afrika Mashariki balabala, Mwanamuziki mashuhuri toka Mji wa Morogoro aliiwakilisha Tanzania kwenye maonyesho ya ulimwengu ya biashara yaliyokuwa mjini Osaka, Japan, na baada ya kurudi kwake alitunga wimbo uliokuwa maarufu nchini wa maonyesho hayo,Nyimbo zake nyingine zilikuwa "Mtaa wa Saba" na "Jamani Morogoro".
-Fursa zilizopatikana Morogoro zingejenga Maghorofa makubwa toka 1970 .
Ujio wa wageni kufanya utalii wa burudani,ujio wa bendi kubwa kuja kushindana na bendi ya Cuban Marimba chini ya Salum Abdallah na Morogoro Jazz chini ya Mbaraka Mwishehe zilileta watu mbalimbali kutoka kila kona ya nchi na kufanya Mji wa Morogoro kuwa busy kila ifikapo Weekend.
Biashara zilizofanyika kutokana na ujio wa watu,Utalii wa ndani uliofanyika kuipanda na kuizunguka Milima ya Uluguru ingeweza kufanya mzunguko wa hela kuwa mkubwa katika mji wa Morogoro.
Vivutio kama Nne ya kirumi iliyochoreka vyema katika moja ya safu ya Milima ya Uluguru,Uwepo wa kambi kubwa ya Scauti kwa jina la "morning site", Vilima vyenye minara,Beach pekee chini ya Milima ya Uluguru inayotambulika kama " Rock garden", kunduchi,Kambi ya Scauti ya Bahati Camp iliyopo juu ya Vilima vya Uluguru.
Kwa Utatalii huu wa ndani basi ingewezekana kuupendezesha Mji wa Morogoro kwa Maghorofa Marefu toka miaka ya 1970.
Nimalizie kwa kusema Morogoro ilipaswa kuwa Jiji toka miaka ya 1970 kwani Wilaya mbili za Morogoro tayari zilikuwa Halmashauri za miji toka miaka ya 1928.Kama kungekuwa na Maendeleo basi miaka hamsini mbele yaani 1978,Morogoro ilipaswa kuwa Jiji.
Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Morogoro,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumlinda na kumbariki Rais wetu John Magufuli.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.