Upinzani watofautina bungeni
Send to a friend Thursday, 11 November 2010 20:42 0diggsdigg
Boniface Meena na Habel Chidawali, Dodoma
VYAMA vya upinzani vimemeguka bungeni baada ya Chadema kuchukuanafasi zote za juu za uongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni bila kuvihusisha vyama vingine.
Baada ya Chadema kutangaza jana kuwa imewateua Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Tundu Lissu kuwa viongozi wake wakuu bungeni, vyama vyama vya CUF, TLP na NCCR Mageuzi, viliamua kuunda kambi nyingine ya upinzani isiyorasmi.
Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge wa Chadema, John Mrema aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama hicho kimemteua Mbowe kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Naibu wake ni Zitto na Tundu Lisu anakuwa Mnadhimu Mkuu.
Mbowe ni Mbunge mteule wa jimbo la Hai, Zitto Kigoma Kaskazini na Tundu Lissu, Singida Mashariki.
"Tuna asilimia 12.5 ya wabunge na hiyo inatupa nafasi ya kuunda kambi ya upinzani bungeni," alisema Mrema.
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kambi ya upinzani bungeni, Mrema alieleza kuwa amepata taarifa kuwa CUF kimeungana na NCCR Mageuzi na TLP kuunda kambi yao.
Mrema alisema CUF kimewaeleza kuwa kimeunda kambi yao kwa kushirikiana na NCCR-Mageuzi na TLP.
"Sijui wanaunda kambni gani, lakini Hamad Rashid ametueleza kuwa wao wameungana na NCCR na TLP kuunda kambi yao," alisema Mrema.
Kauli hiyo ya Mrema iliungwa mkono na aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed aliyesema kuwa CUF imeamua kuunda kambi yao inayojulikana kwa jina la ‘Minority opposition' ambayo ina viongozi wake.
"Kama baadaye wenzetu wa Chadema watataka tushirikiane tutafanya hivyo, lakini hiyo ndiyo kambi yetu tuliyoiunda," alisema Hamad na kufahamisha kuwa yeye ndiye kiongozi wa kambi hiyo.
Alisema kambi hiyo inaongozwa na yeye (Hamad) kama mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti ni Khalifa Suleiman na Katibu Mkuu ni David Kafulila wa NCCR.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF imeamua kuunda kambi yake kwa kuwa Chadema kimetangaza kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni.
Kitendo cha kuunda kambi mbili za upinzania bungeni kinaonyesha kuwa bado kuna tatizo la ushirikiano miongozi mwa vyama hivyo, ambavyo vimekuwa vikivutana kwa muda mrefu kuhusu kuunganisha nguvu.
Mgororo huo umesabisha kutoshirikiana wakati wa uchaguzi, ambapo kila chama husimamisha mgombea wake katika majimbo ambayo chama kimojawapo kina nguvu zaidi.
Utengeno huo umesababisha vyama hivyo kupoteza ushindi dhidi ya CCM kwa kugawana kura, kama ilivyotokea Tarime mkoani Mara katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Katika jimbo hilo ambalo ni ngome ya Chadema, chama hicho kilimsimamisha Mwita Waitara na CUF walimsimamisha Charles Mwera aliyekuwa mbunge wa Chadema, lakini aliunguliwa wakati wa mchakato kuteua wagombea.
Hatua hiyo ilisababisha wagombea hao kugawana kura ambazo zingejumlishwa zingewezesha jimbo hilo kuwa mikononi mwa Chadema, lakini likaenda CCM.
Pia katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijini mwaka mapema mwaka jana CUF ambayo haikuwa na nguvu Mbeya Vijijini ilimsimamisha mgombea na kuvishawishi vyama vingine kukiunga mkono.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema nayo ilisimamisha wagombea katika majimbo yote ya mikoa ya Kusini mwa Tanzania ambako ni ngome ya CUF
source : mwananchi
au mwananchi nayo imenunuliwa, they have reported what happened, na kama ni hivyo kazi ipo!!!!!!!!!!