Kamati za bunge na majukumu yake ,muongozo wake na muundo wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za bunge na majukumu yake ,muongozo wake na muundo wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Feb 10, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NAOMBA TUZIJUE KAMATI ZA BUNGE HALAFU TUANGALIE WALE WALIOCHAGULIWA JANA WANAWEZA KUFANYA KAZI WALIZOPEWA AU???  KAMATI ZA BUNGE: MUUNDO NA MAJUKUMU YAKE
  1.0 UTANGULIZI:
  1.1 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Chombo Kikuu cha
  Kikatiba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  ya mwaka 1977 pamoja na mabadiliko yote yaliyofanywa hadi tarehe
  20 June, 2005. Maelezo ya kina kuhusu Bunge na mamlaka yake
  yametolewa katika Sura ya Tatu ya Katiba kuanzia Ibara ya 62 hadi
  101.
  1.2 Bunge kwa hadhi yake ya Kikatiba ni moja ya Mihimili Mitatu
  Mikuu ya Nchi ambayo ni Mamlaka Kamili (Sovereign State).
  Mihimili hiyo kwa pamoja ni:
  1.2.1 Bunge (Parliament) ambalo ni Mamlaka ya Kutunga Sheria
  Nchini.
  1.2.2 Mahakama (Judiciary) ambayo ndiyo Mamlaka ya Kutafsiri
  Sheria na kutoa Haki Nchini.
  1.2.3 Serikali (Executive) ambayo ndiyo Mamlaka ya kutekeleza
  Sheria na Mambo mengine ya kiutendaji ya Serikali.
  1.3 Mamlaka yote yanavyotekelezwa na kila Mhimili yamewekewa
  mifumo na taratibu ambazo zinaonyesha waziwazi mwanzo na
  ukomo wa utekelezaji wa madaraka ya kila Mhimili.
  3
  2.0 MAJUKUMU YA JUMLA YA BUNGE
  Majukumu ya jumla ya Bunge yameainishwa katika Ibara 63(2) ya Katiba
  kama ninavyoyanukuu hapa chini nikiacha sehemu moja ya Bunge ambayo ni
  Rais na madaraka yake ya Kikatiba:
  (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho Chombo Kikuu cha Jamhuri ya
  Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya Wananchi,
  kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
  vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba
  hii.
  (3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza:-
  (a) Kumwuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya
  umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika
  wajibu wake,
  (b) Kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa
  Bunge wa kila mwaka wa Bajeti;
  (c) Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au
  wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya
  Muungano na Kutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa
  mpango huo;
  (d) Kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo
  Sheria;
  (e) Kujadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya
  Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.
  4
  3.0 MFUMO WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BUNGE
  Kwa upande wa utekelezaji wa Majukumu ya Bunge, Katiba vilevile imeweka
  mfumo na utaratibu ambao unahakikisha utekelezaji wenye ufanisi. Maeneo
  hasa ambayo yanahusika na kifungu hiki ni Ibara ya 89 ambayo inazungumzia
  Kanuni za Kudumu za Bunge; Ibara ya 92 kuhusu Mikutano ya Bunge na
  Ibara ya 96 inayohusu Kamati za Kudumu za Bunge
  3.1 KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE
  Kama inavyotamkwa na Katiba, Bunge limetunga Kanuni ambazo
  zinaongoza utekelezaji wa majukumu yake. Kanuni hizo huwa
  zinafanyiwa mapitio ili ziwe za wakati kwa kuzingatia ukomavu wa
  kisiasa ndani ya Bunge na mabadiliko ya jumla katika nyakati hizi za
  utandawazi. Kanuni kwa jinsi zilivyo, zimeainisha waziwazi kuhusu
  Bunge na Kamati zake litakavyotekeleza mamlaka yake.
  3.2 MIKUTANO YA BUNGE
  Katiba vilevile katika Ibara ya 92 imetamka jinsi Bunge linavyoweza
  kujiwekea utaratibu wa Mikutano yake ili litekeleze Mamlaka yake ya
  Kutunga Sheria na kusimamia utekelezaji wa Serikali kwa ufanisi; kwa
  niaba ya Wananchi. Kwa ajili ya msisitizo kuhusu mfumo wa
  utekelezaji wa majukumu yake, Bunge limeweka Kanuni za kuongoza
  jukumu hili kama ilivyoanishwa katika Sehemu ya Tatu ya Kanuni za
  Kudumu za Bunge Toleo ya 2004 — Kanuni ya 18 mpaka 22.
  5
  3.3. MUUNDO WA KAMATI ZA BUNGE
  Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 96, Bunge limepewa madaraka ya
  kuunda Kamati za Bunge za aina mbalimbali na kwamba muundo wa
  Kamati hizo umefafanuliwa na Kanuni za Kudumu za Bunge. Kwa
  hiyo, kwa mujibu na Kanuni za Bunge, Kamati zifuatazo
  zimebainishwa:
  3.3.1 KAMATI ZA KUDUMU
  3.3.1.1 Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 89 limeunda Kamati 15
  zifuatazo:
  (i) Kamati ya Uongozi;
  (ii) Kamati ya Fedha na Uchumi;
  (iii) Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
  (iv) Kamati ya Hesabu za Serikali;
  (v) Kamati ya Uwekezaji na Biashara;
  (vi) Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje;
  (vii) Kamati ya Kanuni za Bunge;
  (viii) Kamati ya Ulinzi na Usalama;
  (ix) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge;
  (x) Kamati ya Huduma za Jamii;
  (xi) Kamati ya Maliasili na Mazingira;
  (xii) Kamati ya Maendeleo ya Jamii;
  (xiii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
  (xiv) Kamati ya Kilimo na Ardhi;
  (xv) Kamati ya Miundombinu.
  3.3.2.1 Aidha, Kanuni 88(12) imetoa fursa kwa kila Kamati kuunda
  Kamati Ndogo kwa ajili ya uendeshaji bora wa shughuli
  zake.
  6
  3.3.2 KAMATI TEULE
  Kamati Teule zimewekewa utaratibu wa kuundwa katika Kanuni ya 104. Kwa
  mujibu wa Kanuni hii Kamati Teule itaundwa na Bunge kwa madhumuni
  maalum, kwa hoja mahsusi itakayotolewa kwa ajili hiyo na kuafikiwa. Aidha,
  Kamati Teule inaweza kuundwa kama Bunge litaamua kwamba hoja fulani
  iliyojadiliwa ikafanyiwa kazi zaidi na Kamati Teule. Kamati Teule hukoma
  mara imalizapo kufanya kazi iliyopangiwa na Bunge.
  Katika vifungu vinavyofuata, mada hii itajihusisha zaidi na Kamati za
  Kudumu. Kwa mantiki hii, basi vifungu vilivyotangulia vihesabiwe kama ni
  vifungu vya kufungua macho tu na kuona jinsi Bunge lenyewe, Kamati na
  Kanuni zake zivyopewa uzito Kikatiba.
  4.0 MAJUKUMU YA MSINGI NA YA JUMLA YA KAMATI
  4.1 Kwa mujibu wa mgawanyo wa Mamlaka kama ilivyoainishwa katika
  vifungu vilivyotangulia, Bunge na Kamati zake za Kudumu hufanya
  kazi za kusimamia Utendaji wa Serikali kwa niaba ya Wananchi.
  Bunge na Kamati zake ndiyo darubini (Oversight or Watch-dog organ)
  ya kuhakikisha kwamba mambo yote ya uendeshaji wa kazi za Dola
  unafanywa kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa.
  Kwa hiyo, kuna majukumu ambayo hutekelezwa na Bunge lenyewe na
  baadhi ya majukumu ambayo utekelezaji wake ni wa siku hadi siku
  yanashughulikiwa na Kamati za Kudumu.
  7
  4.2 Kila Kamati ya Kudumu ma majukumu ya msingi na inalo jukumu la
  jumla la kufuatilia utekelezaji wa Ahadi za Serikali zilizotolewa
  Bungeni ambazo zinagusa mambo yaliyo katika Mamlaka ya Kamati
  inayohusika. Aidha, Kamati inaweza kupendekeza kwa Spika
  nyongeza ya majukumu ambayo yatajitokeza katika kutekeleza
  majukumu ya msingi. Kwa upande mwingine, Spika anaweza
  kukabidhi jambo lingine lolote kwa Kamati yoyote kama atakavyoona
  inafaa, kwa ajili ya kushughulikiwa na Kamati hiyo, kwa mujibu wa
  Kanuni za Kudumu za Bunge Kanuni ya 90(1) na (2).
  5.0 AINA YA KAMATI NA KAZI ZAKE
  5.1 AINA YA KAMATI
  Kamati za Kudumu za Bunge ambazo ziko Kumi na Tano
  (15) kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 3.3.1 zinaweza
  kugawanyika katika makundi matatu (3):
  (a) Kamati zenye Majukumu ya Msingi ya kushughulikia mambo ya
  Ndani ya Bunge (Parliamentary Institutional Functions).
  (b) Kamati zenye Majukumu ya Msingi ya Kusimamia Uendeshaji
  wa Shughuli za Serikali (Oversight or Watch-dog Functions) au
  Kamati zenye “Portfolio”.
  (c) Kamati zenye Majukumu ya Msingi yanayohusu Maeneo
  Maalum yanayogusa Uendeshaji wote wa Serikali (Specific
  Oversight or Watch-dog Functions).
  8
  5.1.1 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI YA
  KUSHUGHULIKIA MAMBO YA NDANI YA BUNGE
  (PARLIAMENTARY INSTITUTIONAL FUNCTIONS)
  Ziko Kamati Tatu (3) zenye majukumu ya aina hii nazo ni:
  (i) Kamati ya Uongozi
  (1) Wajumbe wake ni:
  (a) Spika, ambaye ndiye Mwenyekiti,
  (b) Naibu Spika
  (c) Kiongozi wa shughuli za Serikali
  Bungeni au Mwakilishi wake;
  (d) Kiongozi wa Upinzani Bungeni au
  Mwakilishi wake;
  (e) Wenyeviti wa Kamati za Kudumu;
  (f) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
  (2). Katibu
  Katibu wa Bunge ndiye Katibu wa Kamati
  (3) Majukumu ya Kamati
  Majukumu ya Kamati ya Uongozi ni kufikiria na kumshauri
  Spika kuhusu mambo yote yanayohusu shughuli za Bunge
  kwa jumla; ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu
  utakaorahisisha maendeleo ya shughuli za Bunge au za
  Kamati yake yoyote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo.
  9
  (ii) Kamati ya Kanuni za Bunqe
  (1) Wajumbe wa Kamati wanateuliwa na Spika na Mwenyekiti
  wake ni Spika na Naibu Mwenyekiti ni Naibu Spika.
  (2) Katibu huteuliwa na Ofisi ya Spika
  (3) Majukumu ya Kamati
  (a) Kufikiria na kutoa mapendekezo juu ya kufanya
  mabadiliko katika Kanuni za Bunge.
  (b) Kuchunguza na kutoa taarifa juu ya pendekezo
  lolote linalohusu Kanuni za Bunge ambalo
  limepelekwa kwenye Kamati hiyo na Spika au
  na Mbunge yeyote.
  (c) Kuchunguza na kutoa taarifa juu ya lalamiko lolote
  kuhusu uamuzi wa Spika ambalo limepelekwa
  kwake na Mbunge yeyote.
  (iii) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
  (1) Wajumbe wake huteuliwa na Spika.
  (2) Katibu huteuliwa na Ofisi ya Spika.
  (3) Majukumu ya Kamati;
  (a) Kuchuguza masuala yote yahusiyo Haki,
  Kinga na
  10
  Madaraka ya Bunge yanayopelekwa kwake na
  Spika;
  (b) Kushughulikia mambo yanayohusu Maadili ya
  Wabunge;
  (c) Kufikiria jambo lingine lolote litakalopelewa
  kwake na Spika
  5.1.2 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI YA
  KUSHUGHULIKIA UENDESHAJI WA SERIKALI
  (OVERSIGHT OR WATCH-DOG FUNCTIONS) AU
  KAMATI ZENYE “PORTFOLIO”
  Ziko Kamati Kumi (10) katika aina hii ya Kamati kama
  ifuatavyo:
  (i) Kamati ya Fedha na Uchumi
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Fedha;
  (b) Wizara ya Mipango, Uchumi na
  Uwezeshaji.
  (ii) Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii,
  UTUMISHI na Utawala Bora);
  (b) Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano);
  11
  (c) Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na
  Serikali za Mitaa, Bunge, Maafa na Kampeni
  Dhidi ya UKIMWI).
  (d) Wizara ya Katiba na Sheria.
  (iii) Kamati ya Uwekezaji na Biashara
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko;
  (b) Wizara ya Nishati na Madini.
  (iv) Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
  Ushirikiano wa Kimataifa.
  (b) Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  (v) Kamati ya Ulinzi na Usalama.
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;
  (b) Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;
  (c) Wizara ya Usalama wa Raia.
  12
  (vi) Kamati ya Huduma za Jamii
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii;
  (b) Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya
  Juu;
  (c )Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  (vii) Kamati ya Mahasili na Mazinqira
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira);
  (b) Wizara ya Maliasili na Utalii.
  (viii) Kamati va Maendeleo ya Jamii
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
  Watoto;
  (b) Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya
  Vijana;
  (c) Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
  (ix) Kamati ya Kilimo na Ardhi
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  (a) Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi;
  (b) Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika;
  13
  (c) Wizara ya Maji;
  (d) Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.
  (x) Kamati ya Miundombinu.
  Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
  Wizara ya Miundombinu (Ujenzi,Mawasiliano
  na Uchukuzi).
  5.1.2 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI
  YANAYOHUSU MAENEO MAALUMU
  YANAYOGUSA UENDESHAJI WOTE WA
  SERIKALI (SPECIFIC OVERSIGHT OR WATCH-DOG
  FUNCTIONS)
  Kamati zinazohusika na aina hii ya majukumu ni hizi:
  (i) Kamati ya Hesabu za Serikali
  Kamati hii ina majukumu yafuatayo.
  (a) Kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu
  yaliyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti
  Mkuu wa Serikali kuhusu Serikali Kuu.
  (b) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyokwisha
  kutolewa na Kamati hiyo ya kuondoa matatizo husika, ili
  yasionekane tena katika Taarifa zitakazofuata.
  14
  (ii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa
  Kamati hii ina majukumu yafuatayo:
  (a) Kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu
  yaliyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na
  Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuhusu Serikali za
  Mitaa.
  (b) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo
  yaliyokwisha kutolewa na Kamati hiyo ya kuondoa
  matatizo husika, ili yasionekane tena katika Taarifa
  zitakazofuata.
  5.2 MAJUKUMU YA MSINGI YA KAMATI
  Majukumu ya Msingi ya kila Kamati ya Kudumu ya Bunge yameorodheshwa
  kwenye Kanuni za Kudumu za Bunge kuanzia Kanuni ya 91 hadi 103B.
  5.2.1 Kamati tano (5) zifuatazo:
  (i) Kamati ya Uongozi (Kanuni 91);
  (ü) Kamati ya Kanuni za Bunge (Kanuni 97);
  (iii) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge (Kanuni 99);
  (iv) Kamati ya Hesabu za Serikali (Kanuni 94);
  (v) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Kanuni 103).
  Majukumu yake yameelezwa katika Vifungu 5.1.1 na
  5.1.3 vilivyotangulia
  15
  5.2.2 Kamati nyingine Kumi (10) zenye Majukumu ya Kusimamia
  Uendeshaji wa Serikali (Oversight or Watch—dog Functions) au
  Kamati zenye “Portfolio”, majukumu yake ya msingi na ya jumla ni
  haya yafuatayo:
  (i) Kushughulikia Bajeti za Wizara zilizowekwa chini ya kila Kamati;
  (ii) Kushughulikia mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato
  na Matumizi ya kila mwaka;
  (iii) Kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikataba inayopendekezwa
  kuridhiwa na Bunge ambayo chanzo chake ni Wizara hizo;
  (iv) Kushughulikia Taarifa za kila mwaka za Utendaji na
  Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma yaliyo
  chini ya Wizara zilizowekwa chini ya kila Kamati;
  (v) Kufuatilia utekelezaji unaofanywa na Wizara hizo za kila Kamati kwa
  mujibu wa Ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
  Tanzania, na kama ilivyonukuliwa katika Kifungu 2.0 cha Mada hii.
  5.2.3 UONGOZI WA KAMATI
  Kila Kamati huongozwa na Mwenyekiti na kama hayupo, Makamu
  Mwenyekiti ambaye huchaguliwa kutokana na Wajumbe wa kila
  Kamati, isipokuwa tu kwa Kamati ya Uongozi na Kamati ya Kanuni za
  16
  Bunge kama ilivyokwisha elezwa ambazo Mwenyekiti wake ni Spika.
  Aidha, Mawaziri hawawi Wajumbe wa Kamati isipokuwa tu kwenye
  Kamati ya Uongozi ambayo Kiongozi wa Shughuli za Serikali
  Bungeni au Mwakilishi wake huwa Mjumbe.
  5.2.4 WAJUMBE WA KAMATI
  • Kwa mujibu wa Kanuni 87, Spika huteua Wabunge kuingia katika
  Kamati isipokuwa Kamati ya Uongozi ambayo Wajumbe wake ni
  Wenyeviti wa Kamati za Kudumu.
  • Kwa upande mwingine, Mbunge mmoja mmoja anaweza kuteuliwa
  kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Haki, Maadili na
  Madaraka ya Bunge zaidi ya kuwa kwenye zile Kamati nyingine kumi
  na mbili.
  5.2.5 UHAI WA KAMATI ZA KUDUMU
  Uhai wa Kamati za Bunge na Wajumbe wake umeelezwa waziwazi katika
  Kanuni 87(4) kama ninavyonukuu hapa chini:
  “(4) Wabunge walioteuliwa watashika nafasi zao kama Wajumbe wa
  Kamati zao kwa muda ambao wataendelea kuwa Wabunge (bila kuwa
  Waziri au Spika) mpaka mwisho wa Mkutano unaofuatia mara baada
  ya Mkutano wa Kumi wa Bunge (ambao ndio hukamilisha nusu ya
  kwanza ya maisha ya Bunge) utakaofanywa baada ya kuteuliwa kwao,
  lakini waweza kuteuliwa tena kwenye Kamati hizo katika kipindi cha
  pili kilichobaki cha maisha ya Bunge la kipindi kinachohusika”.
  17
  6.0 UTARATIBU WA KUFANYA KAZI ZA KAMATI
  Kama ilivyoelezwa kwenye vifungu vilivyotangulia, Kamati zina kazi nyingi
  ambazo hapana budi zitengenezwe utaratibu mzuri wa kuzitekeleza. Kwa
  hiyo, kila Kamati inawajibika kuwa na Ratiba ya Kazi ambayo imepata
  mwafaka wa Wajumbe wa Kamati.
  6.1 RATIBA YA KAZI
  Ratiba ya Kazi za Kamati ina sehemu mbili zifuatazo:
  6.1.1 KAZI ZINAZOPANGIWA KAMATI NA SPIKA
  Kazi zinazopangiwa Kamati na Spika ndizo hupewa
  kipaumbele ili Ratiba ya Bunge lenyewe itekelezwe bila
  matatizo. Na kwa utaratibu ulivyo, Mikutano ya Bunge ya
  mwaka mzima inafahamika na Kalenda ya mwaka mzima
  hutolewa ambayo inatakiwa kuzingatiwa na kila Kamati wakati
  wa kupanga kazi zake.
  6.1.2 KAZI ZINAZOPANGWA NA KAMATI
  Kila Kamati ina wajibu wa kupanga Ratiba yake ambayo
  inazingatia Ratiba ya Bunge lenyewe na kutoa nafasi ya
  kwanza kwa kazi ambazo zinatakiwa kutolewa Taarifa Bungeni
  na kwa muda uliowekwa na Spika. Kazi nyingine ni zile
  ambazo zinafanyika wakati Bunge limeahirishwa lakini
  zinazingatia siku 60 zilizotengwa kwa kazi za Kamati kila
  18
  mwaka. Na kwa mujibu wa utaratibu, siku 15 zimetengwa kwa
  kazi za Kamati kabla ya kila Mkutano wa Bunge na hufanyikia
  Jijini Dar es Salaam au Dodoma kwa jinsi Spika
  atakavyoelekeza.
  6.2 MBINU ZA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAMATI
  Kila Kamati inatakiwa kujiwekea utaratibu mzuri wa kutekeleza kazi
  zake. Mbinu mbalimbali hutumika kama ifuatavyo:
  6.2.1 Kufanya kazi kwa kutumia Mikutano ya Kamati nzima au Kamati
  Ndogo.
  6.2.2 Kutembelea maeneo ya uendeshaji wa kazi za Serikali ili kupata
  uelewa zaidi wa hali ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
  6.2.3 Kuandaa Semina ambapo Wataalam wa fani mbalimbali hutoa Mada
  za kuongeza uelewa na elimu ya Wajumbe kuhusu maeneo mbalimbali
  ya shughuli za uendeshaji wa Serikali, Taasisi na Asasi zake.
  6.2.4 Kufanya Mikutano na Wadau (Public Hearing) mbalimbali ili kupata
  michango au maoni yao kuhusu masuala mbalimbali na hasa kwenye
  baadhi ya Miswada ambayo inatazamiwa kuwasilishwa Bungeni na
  inagusa maisha ya Wananchi wengi.
  19
  6.3 BAJETI
  Shughuli za Kamati hufanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Kamati ya kila
  mwaka. Ila uzoefu umeonyesha kwamba Semina mbalimbali zinaweza kwa
  kuafikiana, kugharamiwa na Wizara au Taasisi hapa Nchini na za Kimataifa
  7.0 TAARIFA ZA KAZI ZA KAMATI
  7.1 Kila Kamati inawajibika kuwasilisha Taarifa za kazi ambazo
  imepangiwa na Spika au kazi zake za msingi katika wakati
  zinaotakiwa. Na kila mwisho wa mwaka kila Kamati inatakiwa
  kuandaa Taarifa ya mwaka ya kazi zake na kuiwasilisha Bungeni kama
  Spika atakavyoelekeza
  7.2 Wakati wa kuwasilisha Taarifa Bungeni, Mwenyekiti kwa kuafikiana
  na Wajumbe anaweza kutoa nafasi kwa Wajumbe wa Kamati
  kuwasilisha Taarifa hizo kwa niaba yake. Ila Mwenyekiti anachukua
  jukumu la kuwajibika kwa yale yatakayotolewa kwa niaba yake.
  7.3 Utaratibu huu wa kuwashirikisha Wajumbe pia unatumika kwenye
  kuongoza Vikao vya Kamati hasa vile vya kushughulikia Hesabu
  zilizokaguliwa za Mashirika chini ya “Portifolio” ya Kamati. Utaratibu
  huu ni mzuri kwa kuwa Mashirika ni mengi na kwa siku Kamati
  inaweza kushughulikia Mashirika hadi matatu.
  Utaratibu wa kuwashirikisha Wajumbe wa Kamati katika kuongoza
  Vikao unajenga mshikamano wa dhati na uzoefu katika kazi za
  Kamati.
  20
  8.0 HUDUMA KWA KAMATI
  Ofisi ya Bunge inao utaratibu mahsusi wa kuhudumia Kamati za Bunge kwa
  kuzipatia Makatibu wa Kamati, huduma za kuchapa Taarifa na Usafiri kama
  Kamati itapanga kufanya kazi mahali ambapo usafiri unahitajika n.k.
  9.0 HITIMISHO
  9.1 Mada hii imejaribu kutoa maelezo kuhusu Kamati za Bunge
  (Parliamentary Committees) Muundo wake, Majukumu yake na jinsi
  zinavyofanya kazi zake za kusimamia uendeshaji wa shughuli za
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Bunge.
  Vilivyo, Kamati za Bunge hapana budi zitekeleze kazi zake kwa niaba
  ya Bunge kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
  pamoja na Kanuni za Kudumu za Bunge. Kwa mantiki hii kila Mbunge
  anahitajika kujizoesha kusoma Katiba na Kanuni za Bunge ili ajipatie
  uelewa wa kina wa nyenzo hizi zinazoongoza kazi za Bunge na Kamati
  zake.
  9.2 Mada hii pia imegusia uzoefu wa aina mbalimbali ambao kama
  utatumika basi utaimarisha na kuongeza ufanisi wa utendaji wa
  Kamati za Kudumu za Bunge.
   
Loading...