Kamati ya Zitto yatengua maamuzi ya Waziri Maige | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Zitto yatengua maamuzi ya Waziri Maige

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 25, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Kamati ya Zitto yatengua maamuzi ya Waziri Maige

  Patricia Kimelemeta

  KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imetengua maamuzi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ya kutaka wawekezaji wa mahoteli kwenye hifadhi za Taifa watozwe asilimia 10 ya kodi ya mapato.

  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alisema kiasi hicho cha kodi ni kidogo na kinaitia Serikali hasara isiyokuwa ya lazima. Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema hayo wakati wa kupitia hesabu za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).

  Alisema Tanapa ilipaswa kuingiza kiasi cha Sh21 bilioni ya mapato kwa mwaka, hii inatokana na kila mgeni anayefika kwenye hifadhi za Taifa kulipa kodi stahiki kwa Serikali.

  “Kwa mujibu wa Sheria za Bunge, ninatengua maamuzi ya waziri ya kutoza asilimia 10 ya mapato kwa wawekezaji wa mahoteli kwenye hifadhi za taifa, badala yake nataka watozwe dola 10 hadi 50 kama ilivyopendekezwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Tanapa,” alisema Zitto.

  Alisema Tanapa inatakiwa kubadili utaratibu wa utozaji wa kodi hiyo na kuwasilisha taarifa zao kabla ya kikao cha Bunge cha Juni, mwaka huu ili wajumbe wa kamati hiyo waipitie mapema na kujiridhisha. Alisema Bodi ya Tanapa imetakiwa kuwasilisha taarifa utenguzi wa maamuzi hayo kwa Waziri mwenye dhamana ili atambue na kuthibitisha kuridhishwa kwa maamuzi hayo kabla ya Kikao cha Bunge cha mwezi ujao.

  “Tunamtaka Waziri kudhibitisha kuridhishwa na maamuzi ya kamati kabla ya Kikao cha Bunge kijacho na kwamba kama atakataa maamuzi haya, lazima aandae majibu kwenye kikao kijacho cha Bunge, kwa sababu hana mamlaka ya kuwapunguzia kodi wawekezaji hawa,” alisema.

  Alisema hatua ya Waziri Maige inakwenda kinyume na sheria kwani hana mamlaka yoyote ya kuizuia bodi ya wakurugenzi kufanya maamuzi ya kuongeza mapato ya kodi ya shirika hilo na kusisitiza kuwa kitendo hicho ni sawa na kuwabeba wawekezaji hao kinyume na taratibu. Alisema kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2009/10 ambayo imepitishwa na Bodi ya Tanapa.

  Mkurugenzi wa Tanapa, Edward Kisha alisema shirika lake lilipendekeza wawekezaji hao kutozwa kiasi cha dola 10 hadi 50 ili kuongeza mapato kwa Taifa ili kuliwezesha lijiendeshe bila hasara. “Bodi ya Tanapa ilipendekeza wawekezaji hao kulipa kiasi cha dola 10 hadi 50, lengo ni kuongeza mapato kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii na kwamba Serikali inaweza kuingiza mapato kupitia utalii,” alisema Kisha.

  Alisema wakati kamati ya bodi hiyo ikifanya marekebisho ya kuongeza kodi kwa wawekezaji hao, Chama cha Wawekezaji wa kwenye Mahoteli kiliwasilisha barua ya malalamiko ya kupinga ongezeko hilo kwa waziri ambaye aliamua kuwapunguzia kodi hiyo.

  Hata hivyo, kamati hiyo imeitaka bodi hiyo kufanyia kazi baadhi ya kasoro zilizojitokeza hasa suala zima la kufuata utaratibu wa sheria ya ununuzi wa mali za shirika, kurekebisha utaratibu wa mfumo wa bima kwa wafanyakazi wake.
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,620
  Trophy Points: 280
  Tanzania tuna laana nahisi;kila bosi ktk serikali yetu anajimulia tu kusamehe fedha halali tulizo paswa kuzipata kutoka ktk vyanzo vyetu halali vya mapato;then baadae Waziri huyo huyo akiombwa awasemee wafanyakazi waliopo chini yake kuhusu maboresho ya mishahara yao bila aibu huwa anabwatuka"Serikali haina hela"

  Ingekuwa nchi za wenzetu huyu Maige siku nyingi yupo nje ya serikali lkn TZ kila kitu siasa!
   
 3. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Keep it up Zitto!
   
 4. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Sio mbaya,lakini haitoshi.Mashirika ya Umma bado hayakizi haja za kuwepo!!Tunahitaji Mashirika yaweze kujiendesha kwa faida na yasiwe ya watu Binafsi kama wakurugenzi n.k
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hizi kamati zenyewe za wabunge zina competence kiasi gani? how reliable they are? Mi nadhani mojawapo ya ishu kubwa kama taifa ni kukosekana kwa competent check and balance bodies ambazo zipo kisheria ktk sekta muhimu, ndio maana kila kitu kinapelekwapelekwa tu na wanasiasa uchwara, wafanyabiashara na matapeli ndio wanapotokea hapohapo na kutupiga bao.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Kamati ya Zitto yatengua maamuzi ya Waziri Maige Send to a friend Thursday, 24 March 2011 21:30

  Patricia Kimelemeta
  KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imetengua maamuzi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ya kutaka wawekezaji wa mahoteli kwenye hifadhi za Taifa watozwe asilimia 10 ya kodi ya mapato.

  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alisema kiasi hicho cha kodi ni kidogo na kinaitia Serikali hasara isiyokuwa ya lazima. Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema hayo wakati wa kupitia hesabu za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
  Alisema Tanapa ilipaswa kuingiza kiasi cha Sh21 bilioni ya mapato kwa mwaka, hii inatokana na kila mgeni anayefika kwenye hifadhi za Taifa kulipa kodi stahiki kwa Serikali.

  “Kwa mujibu wa Sheria za Bunge, ninatengua maamuzi ya waziri ya kutoza asilimia 10 ya mapato kwa wawekezaji wa mahoteli kwenye hifadhi za taifa, badala yake nataka watozwe dola 10 hadi 50 kama ilivyopendekezwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Tanapa,” alisema Zitto.

  Alisema Tanapa inatakiwa kubadili utaratibu wa utozaji wa kodi hiyo na kuwasilisha taarifa zao kabla ya kikao cha Bunge cha Juni, mwaka huu ili wajumbe wa kamati hiyo waipitie mapema na kujiridhisha. Alisema Bodi ya Tanapa imetakiwa kuwasilisha taarifa utenguzi wa maamuzi hayo kwa Waziri mwenye dhamana ili atambue na kuthibitisha kuridhishwa kwa maamuzi hayo kabla ya Kikao cha Bunge cha mwezi ujao.

  “Tunamtaka Waziri kudhibitisha kuridhishwa na maamuzi ya kamati kabla ya Kikao cha Bunge kijacho na kwamba kama atakataa maamuzi haya, lazima aandae majibu kwenye kikao kijacho cha Bunge, kwa sababu hana mamlaka ya kuwapunguzia kodi wawekezaji hawa,” alisema.

  Alisema hatua ya Waziri Maige inakwenda kinyume na sheria kwani hana mamlaka yoyote ya kuizuia bodi ya wakurugenzi kufanya maamuzi ya kuongeza mapato ya kodi ya shirika hilo na kusisitiza kuwa kitendo hicho ni sawa na kuwabeba wawekezaji hao kinyume na taratibu. Alisema kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2009/10 ambayo imepitishwa na Bodi ya Tanapa.

  Mkurugenzi wa Tanapa, Edward Kisha alisema shirika lake lilipendekeza wawekezaji hao kutozwa kiasi cha dola 10 hadi 50 ili kuongeza mapato kwa Taifa ili kuliwezesha lijiendeshe bila hasara. “Bodi ya Tanapa ilipendekeza wawekezaji hao kulipa kiasi cha dola 10 hadi 50, lengo ni kuongeza mapato kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii na kwamba Serikali inaweza kuingiza mapato kupitia utalii,” alisema Kisha.

  Alisema wakati kamati ya bodi hiyo ikifanya marekebisho ya kuongeza kodi kwa wawekezaji hao, Chama cha Wawekezaji wa kwenye Mahoteli kiliwasilisha barua ya malalamiko ya kupinga ongezeko hilo kwa waziri ambaye aliamua kuwapunguzia kodi hiyo.

  Hata hivyo, kamati hiyo imeitaka bodi hiyo kufanyia kazi baadhi ya kasoro zilizojitokeza hasa suala zima la kufuata utaratibu wa sheria ya ununuzi wa mali za shirika, kurekebisha utaratibu wa mfumo wa bima kwa wafanyakazi wake.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Maige adaiwa kuivuruga TANAPA

  Thursday, 24 March 2011 20:05 newsroom



  NA WAANDISHI WETU
  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imefichua mgogoro kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii na Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaosababisha serikali kupoteza mabilioni ya shilingi, kwa kukubali kutoza ada ndogo kwa wawekezaji wa hoteli za mbugani. Mgogoro huo unatokana na kitendo cha waziri huyo, Ezekiel Maige, kudaiwa kuingilia kati na kuondoa maamuzi ya bodi ya TANAPA, iliyowataka wawekezaji wa hoteli kwenye hifadhi za taifa kuongezewa kiasi cha tozo.
  Kitendo hicho kimeelezwa kuchangia kuikosesha serikali mapato ya zaidi ya sh. bilioni 21 kwa mwaka, ikilinganishwa na sh. bilioni 1.5 zinazokusanywa hivi sasa kutoka kwa wawekezaji hao kwa mwaka.
  POAC katika kikao chake cha jana, kilichofanyika ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam, wajumbe wa kamati hiyo walikutana na uongozi wa TANAPA kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2008/2009.
  Akichangia mada kwenye mkutano huo, Kangi Lugola, mbunge wa Mwibara (CCM), alisema katika taarifa za CAG, TANAPA imekuwa ikitoza ada ndogo kwa wawekezaji wa hoteli, hivyo kushuka kwa mapato na kufikia sh. bilioni 1.5 kwa mwaka kutoka sh. bilioni 21.
  Suala hilo liliibua hoja kwa wajumbe wengine wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, aliyetaka kujua kwa nini hatua madhubuti hazijachukuliwa ili kuongeza mapato ya TANAPA.
  Wajumbe wa kamati walimtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, ambaye alisema awali bodi ya TANAPA ilikubali kuongeza viwango vya malipo kwa wawekezaji wa hoteli.
  "Bodi iliongeza viwango ndani ya hifadhi zote lakini Chama cha Wamiliki wa Hoteli (HAT) kilipinga na kwenda kwa waziri kulalamika, ambaye aliingilia kati na kuitaka TANAPA kuacha kukusanya mapato kwa kodi mpya, badala yake itoze kiwango cha chini.
  "Sisi tunatekeleza agizo la waziri mwenye dhamana, na hivi sasa tunawatoza kati ya dola tano na 13 za Marekani, badala ya 20 na 50 zilizopitishwa na bodi ya TANAPA. Hatuna budi kufanya hivyo kama tulivyoelekezwa, kwani sheria inampa mamlaka waziri," alisema Kijazi.
  Zitto alimtaka kueleza ni sheria ipi inayompa mamlaka waziri kukiuka maagizo ya bodi, hususan kutokubali kupandishwa ada kwa wawekezaji wa hoteli katika mbuga za taifa.
  "Hapa kuna haja gani ya kuwa na bodi, ni bora kuwa na idara ambayo itakuwa chini yake, lakini kwa hili tunahitaji tupate maelezo ya kina. Bodi ni chombo kizito na kina sheria zake,'' alisema Zitto.
  Mjadala huo ulimfanya mwanasheria wa TANAPA kusoma vipengele vya sheria ambavyo vilikuwa tofauti na uamuzi uliofikiwa wa kuondoa ada hiyo kwa wawekezaji.
  Kutokana na hilo, Zitto alisema wajumbe wa kamati hiyo wanatengua uamuzi wa Maige kwa mujibu wa sheria ya Bunge, kwa kuwa hauna maslahi kwa taifa.

  "Kamati inafuta maamuzi ya waziri kuhusu agizo lake na barua ya katibu mkuu kwa mujibu ibara 63, kifungu cha pili cha sheria ya Bunge na ibara ya 8 ya katiba, ambayo imeipa Bunge nguvu ya kisheria. Tunaitaka TANAPA ipange utararibu upya ili kulinda rasilimali za Watanzania kupitia sekta ya utalii," alisema.

  POAC imesema itakutana bungeni na Waziri Maige na kumweleza uamuzi huo, na kumtaka kuridhia maamuzi ya bodi ya TANAPA. Alisema asipofanya hivyo, kamati itawasilisha taarifa kwa spika ili kufikishwa katika kikao cha bunge.
  Kwa upande wake, mjumbe wa bodi ya TANAPA, Dk. Marcelina Chijoriga, alisema watahakikisha wanatekeleza maelekezo ya kamati ili kuboresha sekta ya utalii nchini.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Bongo bana kila kitu siasa tuuuuu, lini mtaweza tenganisha haya mambo jamani? wanasiasa wanaiua hii nchi plse!!!
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Maamuzi mabovu yapoteza bilioni 20/- za serikali


  Na Tumaini Makene

  KITENDO cha Wizara ya Maliasili na Utalii kuingilia maamuzi ya Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kimeligharimu taifa takribani sh. bilioni 20 ambazo
  zingepatikana kupitia tozo kutoka kwa hoteli za kitalii nchini katika mwaka wa fedha 2009/10.

  Maamuzi ya Bodi ya TANAPA yaliyoingiliwa na uongozi wa wizara hiyo yalikuwa ni kushusha viwango vya malipo wanayostahili kulipa wawekezaji wa hoteli hizo, kutoka dola 20-50, hadi dola 3-15, hali ambayo pia imesababisha kushuka kwa mapato kutoka bilioni 21 kwa mwaka kufikia bilioni 1.5.

  Hayo yaliibuliwa jana katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambapo baadhi ya wabunge walihoji sababu ya kushuka kwa mapato ya shirika hilo, kama ilivyooneshwa katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Hii itakuwa mara ya pili kwa wizara hiyo kupindisha mambo, kwa maslahi ya wawekezaji wa sekta ya utalii, badala ya maslahi mapana ya taifa.

  Aliyeanza kuibua hoja hiyo iliyozua mjadala, alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Mwibara, Bw. Kangi Lugola, akisema kuwa ripoti ya CAG imebainisha TANAPA wanatoza ada ndogo kwa wawekezaji wa hoteli za kitalii ndani ya mbuga za taifa, hivyo kushusha mapato ya shirika hilo la umma na taifa kwa ujumla.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Bw. Allan Kijazi alijibu kuwa awali Bodi ya TANAPA iliweka viwango vya malipo kwa wawekezaji hao kwa ada ya dola 20-50, lakini wamiliki wa hoteli kupitia chama chao (HAT) walizipinga.

  Kwa mujibu wa Bw. Kijazi, pingamizi hilo lilikubalika kwa waziri, hivyo akaamua kuingilia na kuwaagiza TANAPA, kuacha kutoza kodi hizo mpya, badala yake washushe viwango hivyo, mpaka dola 3-15.

  Alisema kuwa wao hawana budi kutekeleza agizo la waziri mwenye dhamana, badala ya uamuzi wa bodi.

  Wabunge kadhaa waliochangia walihoji mamlaka aliyonayo waziri wa wizara husika kuingilia maamuzi ya bodi ambayo inahusisha wataalamu katika suala la kupandisha tozo kwa wawekezaji hao.

  Akizungumza na Majira nje ya kikao, Mwenyekiti wa POAC, Bw. Kabwe Zitto, alisema kuwa sheria zinazosimamia mashirika ya umma bado zina utata, hasa katika majukumu ya waziri, kwani zinamruhusu kuliagiza shirika, nalo linapaswa kufuata maagizo hayo, lakini akahoji;

  "Sasa nini maana ya kuwa na bodi yenye wataalamu, ambayo imeteuliwa na kuaminiwa na waziri huyo huyo...sasa tumebatilisha uamuzi huo wa waziri, kuanzia sasa TANAPA watatoza ada kama ilivyoelekezwa na bodi...we are sending a message to all ministers (huu ni ujumbe kwa mawaziri wote) kuwa wafanye kazi wakijua kuna chombo kinawaangalia na kuwasimamia kama inavyoelekezwa katika ibara ya 63 ya katiba".

  Akizungumza katika kikao hicho, mmoja wa wajumbe wa bodi ya shirika hilo, Dkt. Macelina Chijoliga, alisema kuwa watafayanyia kazi maamuzi ya kamati hiyo ya POAC, kwa nia ya kuboresha sekta ya utalii nchini inufaishe taifa.

  Wakati huo huo, wabunge katika Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, wameonekana kutoa tahadhari juu dhamira ya dhati kwa nchi wanachama katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakisema kuwa maslahi ya Tanzania na Watanzania yanapaswa kupewa uzito unaostahili.

  Takribani wabunge wote waliochangia katika mjadala wa jana ambapo kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Bw. Edward Lowassa, ilikuwa ikipokea na kujadili taarifa ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki, walionekana kuhoji namna gani Tanzania itaweza kunufaika na ushirikiano huo, hasa katika hatua ya soko la pamoja.

  Bw. Lowassa alihoji suala la wageni wanaonunua ardhi 'kwa fujo' hasa katika maeneo ya Mkoa wa Arusha na mingine ya jirani, wakati suala hilo halimo katika moja ya makubaliano ya jumuiya hiyo. Alitaka kupata ufafanuzi pia kutoka kwa wabunge hao iwapo hatua ya shirikisho la kisiasa kwa jumuiya hiyo inawezekana.

  Bw. Lowassa pia alihoji kwa nini Kenya wanajenga uwanja wa ndege mkubwa karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), hali ambayo imekuwa ikisemwa kuwa 'itahatarisha' hatma ya KIA, wakati nchi hiyo ilipaswa kuzingatia kuwa nchi hizo mbili ziko ndani ya ushirikiano.

  "Naona sasa hivi wananunua viwanja vingi tu huko jirani zetu sasa...lakini pia kama tuko katika ushirikiano pamoja ya nini kuwa na uwanja wa ndege karibu na KIA, na wengi wa wanaharakati wanaopinga unjezi wa barabara ya Serengeti ni Wakenya," alisema Bw. Lowassa.

  Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Isarel Natse alitaka kujua namna gani wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania walivyo makini katika kuhakikisha maslahi ya nchi yao yanazingatiwa wanapokuwa katika vikao vya bunge hilo, akisema Tanzania inapaswa kuwa makini 'tusije tukajikuta tunashikwa masikio', akisema nchi zingine zinaonekana kujipanga vilivyo.

  Mbunge wa Ilala (CCM), Bw. Mussa Zungu alitaka kujua ilikuwaje Kenya kama mmoja wa nchi wanachama wa EAC, ilipinga na kisha ikafanya kampeni ya kuhamasisha nchi zingine ziipinge Tanzania kuuza pembe za ndovu mwaka jana, kisha imekuwa ikihamasisha wanaharakati kupinga ujenzi wa mahoteli ya kitalii na barabara katika maeneo ya mbuga za Tanzania.

  Suala jingine lililotatiza kikao hicho ni upashaji habari kwa umma mkubwa wa Watanzania juu ya fursa zilizopo na namna gani mambo yanaendeshwa katika ushirikiano wa jumuiya hiyo, hali iliyomfanya Bw. John Chiligati kusema 'iko siku tutajikuta ndani ya shirikisho la kisiasa bila hata kujua'.

  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dkt. Fortinatus Masha, alisema kuwa manung'uniko na hoja zote walizotoa wabunge wa bunge la Tanzania zilikuwa ni za kweli, ingawa zingine zilielekezwa mahali sahihi (kwa wabunge hao) lakini nyingi zilipaswa kuulizwa kwa serikali, akisema mambo mengi yamekuwa yakiamuliwa na serikali za nchi wanachama kabla hayajafikishwa katika bunge hilo.
  [​IMG]
   
 10. b

  bulunga JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  We need more hotels, hilo kupandisha rates makes us expensive, hatuna ubunifu, angalia TRA sources za mapatao kila siku ni kupandisha kodi ya bia hawataki kutafuta sources zingine, wenye mahoteli wana taka ku monopolizes biashara ya hotels kwa kupinga wawekezaji wengine
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Mwangunga atupiwa tuhuma nzito

  Imeandikwa na Shadrack Sagati; Tarehe: 24th March 2011 @ 22:45 Imesomwa na watu: 320; Jumla ya maoni: 0





  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAOC), imemtuhumu aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, kuwa alishiriki kulikosesha mapato Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa kuwa aliwabeba wawekezaji wa hoteli zilizo0o katika hifadhi za taifa.

  Kamati hiyo ambayo ipo chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) imebatilisha maamuzi hayo ya waziri waliyosema kuwa yalikuwa na dalili za ufisadi.

  Waziri huyo alitengua uamuzi ya Bodi ya Tanapa iliyokuwa imepitisha viwango vya ada vinavyotozwa kutoka kwa wamiliki wa hoteli zilizo katika hifadhi hiyo viwe katika kiwango kisichobadilika.

  Licha ya kuwa waziri hana mamlaka ya kuingilia uamuzi ya Bodi ya Tanapa kuhusu upangaji wa viwango hivyo vya ada, inadaiwa kuwa Mwangunga alijipa mamlaka na kuiamuru Bodi hiyo kubatilisha viwango hivyo na itoze viwango vinavyobadilika kutokana na idadi ya wateja.

  Uamuzi huo wa Mwangunga umelikosesha shirika hilo Sh bilioni 21, baada ya kuambulia Sh bilioni 2.4 tu kama ada kutoka kwa wamiliki wa hoteli katika mwaka wa fedha 2008/09.

  Kamati hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa sheria haimruhusu Waziri wa Maliasili na Utalii kuingilia maamuzi ya Bodi ya Tanapa, hivyo maelekezo aliyoyatoa kwa Bodi hiyo na kukaziwa katika barua iliyoandikwa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara yake ya kukazia maagizo yake, yalikuwa ni batili.

  Kamati hiyo ilielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Modestus Lilungulu, kuwa Mwangunga alibatilisha uamuzi huo baada ya wenye hoteli kupitia chama chao (HAT), kwenda kumlalamikia kuwa viwango vilivyopendekezwa na Bodi hiyo vilikuwa vikubwa.

  Bodi ya Tanapa ilipendekeza viwango vitakavyokuwa vinalipwa na wenye hoteli hao kama ada iwe kati ya dola 20 hadi 45 kutokana na viwango vya malazi walivyovitangaza kwenye tovuti zao.

  "Kamati imeshutushwa na maamuzi ya waziri ambayo hayakujali maslahi ya Serikali kwani yalipunguza mapato ya Tanapa hivyo tunayabadilisha kuanzia sasa," alisema Zitto.

  Zitto aliiagiza Bodi ya Tanapa kukaa tena na kupitisha viwango ambavyo vilipitishwa wakati ule kwa kuwa vilikuwa havijaanza kutumika kabla ya waziri kuwaingilia kiutendaji.

  Alisema , watamwita Waziri na kumueleza hatua hiyo na kumhoji kwa nini alikiuka viwango vya Bodi.

  Ezekiel Maige ambaye mwaka 2009 alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, ndiye Waziri wa wizara hiyo sasa.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Is it Mwangunga or Maige behind this scam?
   
 13. b

  bulunga JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  We need more hotels, hilo la kupandisha rates makes us expensive, hatuna ubunifu, angalia TRA sources za mapatao kila siku ni kupandisha kodi ya bia hawataki kutafuta sources zingine, wenye mahoteli wana taka ku monopolizes biashara ya hotels kwa kupinga wawekezaji wengine, tuna mbuga kubwa ,nzuri sana na wanyama wengi lakini mapatao yetu kwenye mbuga ni aibu ukilinganisha na jirani zetu,huduma zetu katika mahotel huwezi kuamini kuwa hizo ni hoteli starndards zetu ni za chini
   
 14. k

  kashwagala Senior Member

  #14
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii nchi ni kama tumelaaniwa vile! Mbunge wa Shinyanga mjini nae anasema ana ushahidi ndege nyingi za wawekezaji wa madini hasa wa bariadi zinaruka moja kwa moja kutoka maeneo hayo kuelekea Nairobi badala ya kwanza kupitia uwanja wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya check up,anasema ana uhakika hawa jamaa wanatuibia madini mengi sana.Jibu alilopewa ni kuwa TRA ipo pale na kwamba ndege zote hizo zilisha fanyiwa check na maofisa wa TRA.

  Siasa siasa siasa.....sijui kama tutafika!
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  IMEBAINIKA kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alipitisha maamuzi ya kifisadi yaliyosababisha serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) lipoteze jumla ya sh bilioni 19.5 kama sehemu ya kodi inayopaswa kukusanywa kila mwaka kwa wawekezaji wa hoteli za kitalii.
  Hayo yalibainika jana mara baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) chini ya mwenyekiti wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kuhoji sababu iliyoifanya TANAPA kukusanya fedha kidogo kwa hoteli zilizo kwenye hifadhi za taifa.
  Akiibua hoja hiyo mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonyesha kuwa TANAPA wamekuwa wakitoza ada kidogo kwa wawekezaji wa hoteli na kuonekana kushuka kwa mapato ya serikali hadi kufikia sh bilioni 1.5 kwa mwaka badala ya sh bilioni 21 zilizotarajiwa kukusanywa kama kodi kutoka kwenye hoteli hizo.
  Akijibu hoja hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, alisema awali bodi ya TANAPA chini ya mwenyekiti wake, Modestus Lilungulu, ilipandisha viwango vya malipo kwa wawekezaji wa hoteli ndani ya mbuga za taifa, viwango ambavyo vingeiwezesha serikali kupata mapato ya sh bilioni 21 kwa mwaka lakini uamuzi huo ulipingwa na Chama cha Wamiliki wa Hoteli hizo (HAT).
  Alieleza kuwa wamiliki hao waliwasilisha ombi lao kwa waziri mwezi Novemba mwaka jana wakimtaka aingilie kati na kusitisha viwango vya kodi vilivyokuwa vimewekwa na TANAPA na kutaka watozwe viwango vya chini, ombi ambalo lilikubaliwa na waziri huyo.
  Waliieleza kamati hiyo ya Bunge kuwa waziri huyo hatimaye aliagiza TANAPA kuacha kukusanya mapato kwa kodi mpya na badala yake wawatoze wawekezaji hao kwa kiwango cha chini.
  “Sisi tunatekeleza agizo la waziri mwenye dhamana na hivi sasa tunawatoza dola za Marekani tano hadi 13 badala dola 20 hadi 50 iliyopitishwa na bodi ya TANAPA na hatuna budi kufanya hivyo kama tulivyoelekezwa na waziri,” alisema Kijazi.
  Majibu hayo yaliibua hoja nzito kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo ambao walihoji waziri ana mamlaka gani kisheria ya kuingilia maamuzi ya TANAPA hata kusababisha serikali ipoteze mapato yake?
  Wakichangia mjadala huo Mbunge wa Ludewa (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe, na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, walitaka kujua ni sheria ipi iliyompa nguvu Waziri Maige kuingilia maamuzi ya Bodi ya TANAPA.
  “Hapa kuna haja gani ya kuwa na bodi …ni bora kuwa na idara ambayo itakuwa iko chini yake lakini kwa hili tunahitaji tupate maelezo ya kina; bodi ni chombo kizito na kina sheria zake, kwa nini waziri akiingilie?”
  “Leo nchi inapoteza bilioni 21 huku Watanzania wakiendelea kuporwa rasilimali zao na za nchi yao… hakika waziri hana nguvu za kisheria katika hili,” alisema Filikunjombe.
  Hatua hiyo ilimfanya mwanasheria wa TANAPA kusimama kila mara kutafuta vifungu vya kisheria vinavyompa waziri mamlaka lakini havikupatikana.
  Mjadala huo hatimaye ulipelekea mwenyekiti wa kamati hiyo kujadiliana kwa kina na wajumbe wake na kutoka na azimio la kutengua uamuzi huo wa Waziri Maige kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
  “Kamati inafuta maamuzi ya waziri kuhusu agizo lake na barua ya katibu mkuu kwa mujibu ya ibara 63 kifungu cha Pili ya Sheria za Bunge na ibara ya 8 ya Katiba ambayo imeipa Bunge nguvu ya kisheria na tunaitaka TANAPA ipange utararibu mzuri ili kulinda rasilimali za Watanzania kupitia sekta ya utalii.”
  “Bodi ya TANAPA ilipokea maamuzi kinyume cha sheria kutoka kwa waziri na barua aliyoandika katibu mkuu Novemba 2010, ili kusisitiza maamuzi hayo tunaitengua,” alisema Zitto.
  Sambamba na kufuta uamuzi huo wa waziri, kamati yake iliitaka TANAPA kurekebisha viwango hivyo vya malipo na kuandaa viwango vipya vitakavyozingatia maslahi ya taifa.
  Alisema kamati itakutana na Waziri Maige bungeni na kumueleza maamuzi yake na kumtaka kupitisha maamuzi ya bodi ya TANAPA na kama asipofanya hivyo kamati hiyo itawasilisha taarifa kwa Spika ili kufikishwa katika kikao cha Bunge.
  Zitto na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliyaelezea maamuzi ya waziri huyo kuwa yamegubikwa na mazingira ya rushwa kwani isingekuwa rahisi kushusha viwango vya kodi kwa wawekezaji hao bila kuwa na maslahi yake.
  Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya TANAPA, Dk. Macelina Chijoliga, alisema watahakikisha wanafanyia kazi maamuzi ya kamati hiyo ya Bunge kwa kufuata maelekezo muhimu ili kuboresha sekta ya utalii nchini. Alisema kama wizara isingeingilia uamuzi huo wangefanikiwa kukusanya hadi sh bilioni 40 kwa mwaka lakini kutokana na hatua hiyo wamekuwa wakirudi nyuma. “Awali tulikuwa tunakusanya bilioni 1.5 hadi 2.5 mara baada ya bodi yetu kuridhia viwango vipya tulijiwekea lengo la kukunya zaidi lakini kwa kuwa haya ni maagizo basi hatuna budi kuyafuata na kuyafanyia kazi kama kamati ilivyoagiza,” alisema Dk. Chijoliga.
   
Loading...