Kamati ya Zitto kumweka kitimoto gavana wa BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Zitto kumweka kitimoto gavana wa BoT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 19, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,875
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Na Sadick Mtulya
  Mwananchi
  Januari 19, 2010  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imepanga keshokutwa kuwa siku ya kumwita gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ajieleze kuhusu matumizi ya Sh 2.5bilioni kujenga nyumba mbili za kuishi.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa POAC, Ester Kilasi zimeeleza kuwa Profesa Ndulu ataitwa katika kamati hiyo baada ya wajumbe wake kufanya ziara eneo la mradi kulikojengwa nyumba hizo.

  Kilasi aliliambia gazeti hili jana kuwa ziara hiyo itafanyika kwa siku mbili; leo na kesho.

  "POAC imemwita Profesa Ndulu Alhamisi hii (kesho kutwa) ili atupe maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba anayoishi na za manaibu gavana wake," alisema Kilasi na kuongeza: "Lakini kabla ya kupata maelezo hayo kamati imeamua kufanya ziara ya kuzungukia na kuangalia hali halisi ya mradi wa ujenzi wa nyumba hizo tujiridhishe." alisema.

  Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kwamba Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe ambaye yuko masomoni Ujerumani amelazimika kurudi nchini kusimamia sakata hilo.

  Kamati hiyo itakutana na Profesa Ndulu siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo.

  Mkulo aliliambia gazeti hili Ijumaa iliyopita kuwa ripoti ya kamati hiyo imekwishawasilishwa kwake na yeye ameanza kuipitia kabla ya kuitoa hadharani.

  "Nikitoka hapa ninakwenda kuisoma ripoti niliyoiagiza kuhusu matumizi ya fedha yaliyotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya gavana na manaibu gavana," alisema Mkulo na kuongeza:

  "Hizi tuhuma ni nzito na zinamhusu mtu nyeti wa serikali, hivyo itachukua muda kidogo kutoa majibu ya ripoti niliyonayo."

  Mkulo alifafanua kuwa amechelewa kuitoa ripoti hiyo kutokana na kuhusika kwa vyombo vingine nyeti vya serikali katika uchunguzi wake.

  "Nikimaliza kuisoma ripoti hii, nitalazimika nishauriane na washauri wangu na kisha nivishirikishe vyombo vingine nyeti vya serikali," alisema

  Kwa mara ya kwanza taarifa ya matumizi ya fedha katika ujenzi wa nyumba hizo ziliripotiwa na gazeti hili, lakini baadaye BoT ilitoa ufafanuzi ikieleza kuwa nyumba hizo zilijengwa baada ya kufuatwa taratibu zote za zabuni.

  Kabla BoT kujibu tuhuma hizo, Profesa Ndulu alikiri kutumika kwa kiasi hicho cha fedha, lakini akafafanua kuwa fedha ilitumika kujenga upya nyumba hizo na siyo kuzikarabati.

  Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu, ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema, alilalamika gavana huyo.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  This commitee is nothing but sheer political expediency, watch this space closely and you will tell me.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Co-sign
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Yes, watchdog without teeth is wastage of time! we all know Gavana Kafisadi! the commitee will prove the same thing! then what? PCCB , polisi , ikulu, ACG, n.k they are relaxing!
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha ajabu hii ni nchi ya tume zisizo na majibu.Waziri wa fedha anajibu hizi ni tuhuma nzito lakini kwa kuwa huyu ni mtu muhimu nitachelewa kutoa ripoti hadharani na anaona haya majibu ni mazuri tu.

  Kwa majibu hayo tu inaonyesha ni jinsi gani hayupo makini, mtaji wa kuanzishia benki watu wanajengea nyumba ya kuishi? Wanapewa na offer ya kuundiwa tume?

  KWELI TANZANIA TAMBARARE!!

  Haya wapiga kura tutasubiri hiyo ripoti tuone kama itakuwa na chochote cha maana zaidi ya siasa as usual.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ulaji mwingine huo kwa wanakamati, maana hakuna vikao bila malipo ya vikao (Allowance)
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Mbunge ambaye ni mwenyekiti wa kamati hii yko masomoni Ujerumani?

  Inawezekanaje? Inamaana ame abscond parliamentary duties kabla ya kipindi kuisha? Huku sasa kama si kupanda punda wawili ni nini?

  By the time tunawarudisha hawa wabunge kutoka masomoni na kuwalipa per diem zao tutakuwa tushatumia hela za kutoha kujenganyumba nyingine.
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Not Zito again. Ameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye mitambo ya Dowans, personal e-mails etc. na inaonekana huwa anachemka wakati fulani. I do not know may be the Fisadi's wamemtishia maisha yake.
   
 9. s

  saidhorizons Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  The argument by the Guardian (Jan 19th) that the Bank of Tanzania Governor has “brought a lot of respect and dignity to the Bank’s standing nationally or internationally” or the notion that the Bank was spending upward of Tshs 113 Million annually as housing allowance for the Governor is as irrelevant as it sophomoric. The issue under discussion is whether the Governor and the BOT board have shown questionable judgment in authorizing the expenditure of Tshs 1.4 Billion for building the Governor's official residence that some construction experts here in JF have suggested should cost no more than Tshs 600 Million!

  It would equally fair to make the same argument if, for example, the head of the TRA who arguably brings more money to the government of Tanzania treasury than the Governor, decides to emulate the Governor’s example and embark on a spending binge of equally epic proportions that is fuelled by the availability of easy money from the government coffers. The Governor should be held to the same accountability and ethical standards as any chief executives responsible for running a sensitive government institution that must protect the government's meager assets.

  The Governor is well aware of the widespread anger that is simmering beneath the surface after EPA and the Twin Towers mega scandals and should therefore stop pretending to live in a bubble and come clean. The taxpayer, who ultimately guarantees this lavish and decadent lifestyle, should not be considered an endless cash cow, and neither should the treasury be treated as a personal bank account for the few privileged movers and shakers.

  Come to think of it, there is an apparent conflict of interest when the CEO (in this case the Governor) of a company (in this case the BOT) is also the Chairman of the Company Board of Directors which has oversight responsibility for the Bank. This is the time and place for our Members of Parliament to examine and remedy such an unhealthy arrangement with greater urgency.
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naona una bifu na zitto, kamati ya bunge ikishachaguliwa ni mpaka kipindi chake kiishe kwa hiyo atabaki huko mpaka muda wake halali wa kutumikia kamati utakapokwisha..like it or not

  Kwenye mitamby Dowans zitto hakukosea kitu zaidi ya kutoa solution short and long term kutegemeana na parameters zilizopo ..hatimaye waziri Ngeleja ndio mwenye dhamana ya kufanya kitu sahihi na siyo zitto.

  Kamati hii ni muhimu kujua upuuzi wa Ndullu another high profile corrupt individual shame on him
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kwenye hiyo kamati hakuna wa kumuweka kitimoto gavana, wanaohusika hawawezi ku-afford siri kutoka!

  Respect.

  FMEs!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,875
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMES, Hizi Kamati butu zinatafuna pesa tu na hazina meno kabisa ya kuuma. Angalia kamati ya Mwakyembe hadi hii leo mapendekezo yake mengi bado hayajatekelezwa na ile kamati ya madini ni hivyo hivyo. Sidhani kama kutakuwa na jipya hapa zaidi ya kulipana sitting allowances na Ndullu kuendelea kupeta pale BoT
   
 13. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Kamati butu!! Exactly! PCCB Butu, Polisi butu to President butu!!
  Zitto at least you will pocket a whopping USD 20,000 (for a round trip) to attend this I think even more. Your other fellows almost similar figures. This country is up for a grab; and it is for the dogs. Forgive and forget!! Let us live!
   
 14. w

  wasp JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na kamati ya Mabomu Mbagala. Leo hii wananchi hawajapewa kilichojiri kwenye hiyo ripoti ingawa Waziri wa Ulinzi alisema atajiuzulu ikiwa kulikuwa na uzembe.

  Acheni kamati ziundwe watu wale shamba la bibi bila kunawa kwa ari mpya nguvu mpya na spidi mpya.
   
 15. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,896
  Likes Received: 1,657
  Trophy Points: 280
  Tumechoka!
   
 16. O

  Omumura JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tumechoka na vitimoto vyenu visivyoisha!
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  mbaya zaidi kila siku zinaundwa tume tu lakini majibu yake hatuyaoni
  Huu nao ni ufisadi mwingine
   
 18. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  You have said a lot no more comments from me, than just to say is time for Tanzanian leaders to live as other Tanzanians. Sometimes is shame and unbelievable that a security guard is earning more than the one he/she is guarding.
   
 19. E

  Edo JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hili la BoT, nyumba ya Gavana, nadhani wataalamu wa fani ya ujenzi wamelisemea, sidhani kama hiyo kamati na ripoti za Mh Mkullo zitakuja na jambo jipya-humo hakuna ufisadi wala rushwa. Tatizo ni uelewa/ mtazamo wa baadhi yetu/ watu, mtu/yeye akijenga nyumba yeye mwenyewe anakuwa architect, engineer, QS, client, financier na mwishowe anakamilisha ujenzi wa nyumba isiyokuwa na viwango, kisha anasema naye kajenga nyumba kama ya Gavana lakini ametumia gharama ndogo. Ukitumia wataalam, kama inavyotakiwa, utaona hizo gharama zinalandana na kazi iliyofanyika na ina ubora stahiki. Kwa hiyo sioni hizo ripoti za uchunguzi kuja na kitu kipya tofauti na maoni ya kitaalamu ! Tunapoteza muda na kusumbua watu waache kuzalisha mali waende kujibu majungu !
   
 20. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ndullu kisha sema kuwa ana nyumba kama hiyo marekani kama Ballali nae alivyokuwa na nyumba huko huko na kaishia kuzikwa huko!! Sasa inaelekea hawa jamaa hatima ya maisha yao ni huko huko majuu hapa wanakuja kutuibia tu!!
   
Loading...