Kamati ya siasa Wilaya ya Mpwapwa (CCM ) fanyeni kazi zenu za Kikamati ya siasa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Hivi ni kamati hii ya siasa ya wilaya ya Mpwapwa (CCM )au ni ya wakati wa uchaguzi uliopita ndiyo iliyofanya Madudu? Hebu kwa weledi kabisa niambieni! Imekuwaje jimbo la uchaguzi la Mpwapwa lina madiwani hawazidi wanne?

Kwa weledi kabisa hebu kamati ya siasa niambieni kwa nini halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa inaongozwa na mwenyekiti MBEZIGWA ? Kweli diwani darasa la nne anaweza kuongoza halmashauri chini ya Mkurugenzi kama yule mnayemwona na watendaji wakuu wa idala kama wale mnaowaona?

Halmashauri ya wilaya nzima ina madiwani wasiozidi wanne kwa uchache :
1. Ina diwani Mh. George Simbachawene anakizi viwango vyote vya kazi ya udiwani
2. Ina diwani Honorati Pima anakizi viwango vyote vya udiwani
3.Ina diwani Mwachayeka anastahili
4. Ina diwani Vahaye anastahili.

Madiwani wote waliobaki ambao sijawataja na ni wajumbe wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Mpwapwa ni mizigo, mizigo, mizigo. Mbaya zaidi hata Mbunge wa jimbo la uchaguzi la Mpwapwa naye ni msalaba tena ni msalaba wa reli. Kuna madiwani mambulula wa kiwango cha kupitiliza, uje diwani Mahuwi ni mzigo balaa , uje diwani Fuime ni mzigo na eti ndiye makamo wa mwenyekiti wa halmashauri, madiwani wote wa viti maalum ni mzigo hawajui kazi hata moja ya diwani.

Tatizo la kamati ya siasa ya siasa ya wilaya ya Mpwapwa ni uwezo wao mdogo wa kufanya vetting na kuwaachia eti wananchi wachague, ukiwaachia wanachi wachague hata uchaguzi wa mwaka huu wanaweza wakamchagua mbunge aliyopo, lakini sasa je! Mbunge huyo anaweza tena kufanya kazi ya ubunge wakati kesha poteza kumbukumbu zote?

Ni kamti gani ya siasa hii au iliyopita iliwasaidia wanachi wa halmashauli ya wilaya Mpwapwa kuwachagua viongozi ambao hawana uwezo wa kubuni mikakati ya maendeleo na kuwa viongozi wa kulishwa manano na kupokea tu maagizo?

Sasa basi kamati ya siasa ya wilaya ya Mpwapwa iliyopo fanyeni kazi zenu za kikamati ya siasa.

Kuna madiwani wa kumwaga, kuna Yonna Mlungu,kuna Jacksoni Samwel (maombi matatu) mhandisi aliyebobea katika ujenzi wa madalaja na ninafikiri kamati ya siasa mnajua jimbo linataka nini sasa, kuna Dr. Hussen Mansoor mzamivu mtafiti masuala ya mbegu,madiwani mamejaa kata ya Gulwe kuna Tito Chiwanga, kuna Anna Kazige, mima usiseme kuna Mwl Mazengo na wengine.

Kamati ya siasa ya wilaya ya Mpwapwa fanyeni kazi zenu za kikamati, katika upande wa ubunge, Jimbo la Kibakwe kuna Mbunge Mh. George Simbachawene jimbo la Mpwapwa liko wazi hakuna mbunge kuna robot fulani hivyo sasa Kuna wabunge kadhaa watalajiwa wanaweza kuziba nafasi hiyo kamati muwawezeshe.

Kuna Mh. June Ibrahimu FUSSI mbunge mtaralajiwa mwana mama anafaa sana kuchukua nafasi hiyo, ni mama mjanja sana bingwa wa lobbing we angalia aliajiliwa kama afisa ugani wizara ya kilimo na mifugo enzi hizo lakini sasa ana shahada ya uzamii na afisa katika wizara ya mifugo na uvuvi, huyo mama akiwa mbunge anaweza kulobby nusu ya bajeti ya nchi na kuielekeza jimbo la Mpwapwa wabunge wenzake ka Ashantu Kijazi Mbunge wa Kondoa, Mh Ummy Mwaimu mbunge viti maalumu na Mh. Jennista Mhagama mbunge wa Peramiho wanabaki wanang`aa macho tu bajeti yote imechukuliwa nan Mh Fussi.

Kuna Dr. Hussein Mansoor anafaa sana kuchukua nafasi ya mbunge wa Mpwapwa kwa sababu matizo mengi atayajua kwa operation research maana yeye ni mtafiti mungu akupe nini?

Kamati ya siasa ya wilaya ya Mpwapwa fanyeni kazi zenu za kikamati, kazi ndiyo hiyo.
 
Hebu fikiria , ni wewe unasoma mada hii Kama ingekuwa imeandikwa na mwingine, ungeelewa kweli kilichoandikwa?
 
Ni Mara kadhaa nakuona unakuja hapa kumpigia kampeni Fussi, kuwa na tahadhari utamuharibia mwenzako. Afu siasa zako za kufanyia kwenye mitandao ni za kishamba. Hao unaowapigia kampeni wote wanaishi nje ya mpwapwa, wanakuja huko kipindi cha uchaguzi tu hawawezi kuisaidia mpwapwa na chochote.

Mwaka 2010 mlimpa Gregory Teu alikua msomi na alikua anaishi Dsm,Je alifanya nini cha maana? Heb tuwaache viongozi wa chama wafanye kazi yao wala sio kushinikiza kuwapitisha watu ambao wananchi hawawajui na hata chama wilaya hawawajui.
 
Back
Top Bottom