Kamati ya Sheria Ndogo ya Bunge

Wajumbe wake wapya ni Dr. Chamuliho, Dr. Kalemani, na Cde. Polepole. Powers za kamati hii ni zipi?
Ogopa sana umeingia tu ubunge mara ya kwanza ukateuliwa kuwa waziri au naibu then baaadaaaeee sana ukavuliwa uwaziri na kuwa mbunge wa kawaida unateseka sana akili, yaani unarudishwa nyuma ni bora ulisota kwenye ubunge.....then ukateuliwa uwaziri then ukatumbuliwa tena...

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kazi za hiyo kamati ni zipi?
Kazi ya Kamati ni kupitisha sheria ndogo za mamlaka za serikali za mitaa.

Sheria ndogo hizo kimsingi ndio sheria kuu zinazotawala na kuongoza maisha ya watanzania, kwani ndio zinazotumika kila mahali hapa nchini (kila Halmashauri). Minadani (ushuru na ufanyikaji wa mnada), masokoni (ushuru wa meza, ushuru wa kuingiza gari la mazao sokoni) na mitaani (kuratibu uzoaji wa taka, ushuru wa maegesho ya magari, ada za upimaji afya wa watoa huduma za vyakula, salon nk,)

Kwa hiyo hii ni Kamati Muhimu sana pengine kuliko kamati nyingine zote za bunge. Inahitaji wajumbe makini, wasomi na wachambuzi maana wakipitisha kizembe sheria ndogo wanakuwa wameleta maumivu moja kwa moja kwetu wananchi. Kamati hii imewahi kuwa na wajumbe kama Tundu Lissu, Ngeleja na manguli wengine wa sheria.

Kama kinachozungumzwa ni mtonyo, kamati hiyo ina ziara za kufa mtu. Wanazungukia Halmashauri zote nchini kuangalia tu sheria ndogo zipoje.
 
Tundu Lissu ni Mwanasheria, huyu Polepole ni mtu wa " DS" ( Development Studies)! Hivyo kwenye kamati ya Sheria Polepole ni a mere fixture tu!
Wanaobeza Polepole kupelekwa Kamati Ndogo ya Sheria ya Bunge hawaijui nguvu ha hiyo Kamati. Na pia hawajui ya kwamba kwa kipindi chote Tundu Lissu alichokaa bungeni alikuwa Mjumbe wa Kamati hiyo! Sasa, kama wanafikiri Polepole ameshushwa thamani, basi wajue pia kumbe haya Tundu Lissu hakuwa lolotekiwa mjumbe wa kamati hii.
 
Back
Top Bottom