Kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM kufikisha mapendekezo dhidi ya Gwajima, Silaa na Polepole mbele ya Waziri Mkuu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Hatima ya wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole sasa iko mikononi mwa Waziri Mkuu.

Leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wabunge hao waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM na kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwanzoni mwa wiki Bunge lilipokea na kupitisha azimio la Bunge lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,Kinga Madaraka ya Bunge ambalo liliwatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge Askofu Gwajima na Silaa.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuwahoji wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM, Hassan Mtenga amesema kazi bado inaendelea.

"Sisi tumemaliza kazi yetu na mapendekezo yanapelekwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo iko chini ya Waziri Mkuu, wakimaliza basi itajulikana nini kinafuata," amesema Mtenga.

Kuhusu Polepole ambaye makosa yake hayakujadiliwa bungeni amesema tatizo lake ni kushabikia mtandaoni mambo yaliyokuwa yakifanywa na Askofu Gwajima.

Akizungumza kuhusu nini kitatokea kwa wabunge hao ambao tayari walishaadhibiwa kwa kutoshiriki mikutano ya Bunge (Gwajima na Silaa) amesema kamati uongozi itasema mwishoni mwa kazi yao wanayotaraji kuifanya wiki ijayo.
 
Tanzania, uhuru wa kutumia hiari ni jinai. Maana haiwezekani watu na akili zao wanakaa kamati kumjadili Polepole, Gwajima na Silaa juu vitu ambavyo hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Wangekaa kujadili tozo, ugaidi wa Mwanaccm mwenzao Hamza ingekaa poa zaidi. Yani kutafuta posho kwa mambo ya kipuuzi wako vizuri, imani yangu ni kuwa hizo kamati zao hawakai bure.
Watanzania amkeni, CCM imejaza vilaza na wachumia tumbo. Suluhisho bora ni kuikataa, maana haionyeshi dalili ya kubadilika wala jitihada za kutumia rasilimali zilizopo kuneemesha Watanzania wote.
 
Vipi tena mambo ya chama yanarudishwa bungeni? mbona Ndugai alisema watashughulikiwa na chama? kama ndio hivyo si bora Ndugai angeumaliza mchezo bungeni kuokoa muda.
 
Hivi hawa watu wana akili kweli....yaani pamoja na changamoto zote hizi zinazoikabili hii nchi wao wanaona huu upuuzi kama ni wa muhimu?...aisee
wangejua jinsi watu wanavyowaona ndezi bora wangetulia waendelee kula posho.
 
Vipi tena mambo ya chama yanarudishwa bungeni? mbona Ndugai alisema watashughulikiwa na chama? kama ndio hivyo si bora Ndugai angeumaliza mchezo bungeni kuokoa muda.
Hayajarudishwa bungeni...ila majaliwa ni mwenyekiti wa wabunge wa ccm na kamati iliyowahoji ni kamati ya maadili ya wa wabunge wa ccm
 
Tanzania, uhuru wa kutumia hiari ni jinai. Maana haiwezekani watu na akili zao wanakaa kamati kumjadili Polepole, Gwajima na Silaa juu vitu ambavyo hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Wangekaa kujadili tozo, ugaidi wa Mwanaccm mwenzao Hamza ingekaa poa zaidi. Yani kutafuta posho kwa mambo ya kipuuzi wako vizuri, imani yangu ni kuwa hizo kamati zao hawakai bure.
Watanzania amkeni, CCM imejaza vilaza na wachumia tumbo. Suluhisho bora ni kuikataa, maana haionyeshi dalili ya kubadilika wala jitihada za kutumia rasilimali zilizopo kuneemesha Watanzania wote.
Hawa jamaa bana...ni sawa na kusema barba cresit, caput nescit..yaani NDEVU ZINAKUWA LAKINI KICHWA KICHWA HAKIKUI KWA BUSARA!
 
Hatima ya wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole sasa iko mikononi mwa Waziri Mkuu.

Leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wabunge hao waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM na kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwanzoni mwa wiki Bunge lilipokea na kupitisha azimio la Bunge lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,Kinga Madaraka ya Bunge ambalo liliwatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge Askofu Gwajima na Silaa.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuwahoji wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM, Hassan Mtenga amesema kazi bado inaendelea.

"Sisi tumemaliza kazi yetu na mapendekezo yanapelekwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo iko chini ya Waziri Mkuu, wakimaliza basi itajulikana nini kinafuata," amesema Mtenga.

Kuhusu Polepole ambaye makosa yake hayakujadiliwa bungeni amesema tatizo lake ni kushabikia mtandaoni mambo yaliyokuwa yakifanywa na Askofu Gwajima.

Akizungumza kuhusu nini kitatokea kwa wabunge hao ambao tayari walishaadhibiwa kwa kutoshiriki mikutano ya Bunge (Gwajima na Silaa) amesema kamati uongozi itasema mwishoni mwa kazi yao wanayotaraji kuifanya wiki ijayo.
Yaani mimi naona kama hii serikali na ccm wake wanakula tu posho za bure kule mahakamani wanachezea ela za bure hakuna kesi huku bungeni ujinga ujinga kha
 
Badala wajadili hoja ya mwanachama wao mwandamizi aliekuwa gaidi wajue nini cha kufanya aibu kama hio isitokee tena, wanawajadili wakina gwajima wanao simamia kile walichokiamini ambacho hakina madhara kwa jamii kama ugaidi.
 
Hatima ya wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole sasa iko mikononi mwa Waziri Mkuu.

Leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wabunge hao waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM na kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwanzoni mwa wiki Bunge lilipokea na kupitisha azimio la Bunge lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,Kinga Madaraka ya Bunge ambalo liliwatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge Askofu Gwajima na Silaa.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuwahoji wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM, Hassan Mtenga amesema kazi bado inaendelea.

"Sisi tumemaliza kazi yetu na mapendekezo yanapelekwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo iko chini ya Waziri Mkuu, wakimaliza basi itajulikana nini kinafuata," amesema Mtenga.

Kuhusu Polepole ambaye makosa yake hayakujadiliwa bungeni amesema tatizo lake ni kushabikia mtandaoni mambo yaliyokuwa yakifanywa na Askofu Gwajima.

Akizungumza kuhusu nini kitatokea kwa wabunge hao ambao tayari walishaadhibiwa kwa kutoshiriki mikutano ya Bunge (Gwajima na Silaa) amesema kamati uongozi itasema mwishoni mwa kazi yao wanayotaraji kuifanya wiki ijayo.
Hatua waliyoifikia CCM kwa sasa hawana maana tena na hakuna mtanzania mwenye akili timamu atakichagua hicho chama na kuaminika kwa vyovyote vile.

Raia wa kawaida hatamheshimu kiongozi yeyote wa CCM kwa sasa hata kama jua likichomozea magharibi.

*The corrupt individuals have decided to demonstrate their fury vengeance against the pro-JPM philosophy & regime as a whole which will lead to its permanent split for the worst ever experienced since the existence of Tanzania.
 
Gwajiboy hawatamfanya kitu hao maccm. Wataishia kumpa karipio kali tu.

Wamguse waone Kama hawajanuka.
 
Wabunge akili zenu huwa zinamaji ya ukwaju kichwani..

Tozo
Pesa hakuna
Madawa hakuna
Ajira hakuna
Mafuta bei ipo juu

Wanakalia kujadili upumbavu...
Naona tunamisukule tu kule bungeni..
 
Hata huku Uraiani tuko busy na uzinduzi wa Jezi za Simba na Yanga

Bunge la Nchi yeyote ile lazima li reflect tabia ya Jamii husika
Bunge wanalochapana Makonde jua ndio tabia ya Jamii hiyo

Tabia ya Bunge leti ndio tabia ya Jamii yetu i.e Masihara, mizaha, vitu simple kuchukulia serious na vitu serious kuchukulia simple, Uchawi, Rushwa, Ubinafsi, Unafiki, urpokokaji n.k
Wabunge akili zenu huwa zinamaji ya ukwaju kichwani..

Tozo
Pesa hakuna
Madawa hakuna
Ajira hakuna
Mafuta bei ipo juu

Wanakalia kujadili upumbavu...
Naona tunamisukule tu kule bungeni..
 
Hatima ya wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole sasa iko mikononi mwa Waziri Mkuu.

Leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wabunge hao waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM na kuhojiwa kutokana na tuhuma zinazowakabili za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwanzoni mwa wiki Bunge lilipokea na kupitisha azimio la Bunge lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,Kinga Madaraka ya Bunge ambalo liliwatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge Askofu Gwajima na Silaa.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuwahoji wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya wabunge wa CCM, Hassan Mtenga amesema kazi bado inaendelea.

"Sisi tumemaliza kazi yetu na mapendekezo yanapelekwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo iko chini ya Waziri Mkuu, wakimaliza basi itajulikana nini kinafuata," amesema Mtenga.

Kuhusu Polepole ambaye makosa yake hayakujadiliwa bungeni amesema tatizo lake ni kushabikia mtandaoni mambo yaliyokuwa yakifanywa na Askofu Gwajima.

Akizungumza kuhusu nini kitatokea kwa wabunge hao ambao tayari walishaadhibiwa kwa kutoshiriki mikutano ya Bunge (Gwajima na Silaa) amesema kamati uongozi itasema mwishoni mwa kazi yao wanayotaraji kuifanya wiki ijayo.
Pole pole na gwajiboy ni lini walikuwa maccm, ccm bana wanaokoteza watu almradi waobekane Wana watu
 
Back
Top Bottom