Kamati ya Lowassa yajitosa mgogoro na Malawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Lowassa yajitosa mgogoro na Malawi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 6, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Monday, 06 August 2012 14:42

  Fredy Azzah na Geofrey Nyang'oro
  SUALA la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Malawi na Tanzania, limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutaka kupewa maelezo juu ya mgogoro huo.
  Malawi na Tanzania zote zilipata uhuru kutoka kwa Uingereza na mipaka inayotambulika sasa kwa sehemu kubwa, ni ile ambayo iligawanywa wakati wa Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884/1885.
  Hata hivyo, ikiwa sasa ni takriban muongo mmoja tangu nchi hizo mbili zipate uhuru, Malawi katika siku za karibuni imeibua mjadala mzito unaotishia uhusiano wa kidiplomasia na eneo la mpakani na Tanzania, ikisema Ziwa Nyasa lote liko katika ardhi yake.
  Akizungumzia mgogoro huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo,Edward Lowasa alisema baada ya kupata taarifa rasmi ya hali ilivyo katika mpaka huo, itakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa tamko lake.
  “Tutatoa tamko letu baada ya kupata taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vinavyohusika, kwanza tujue hali ikoje, mambo kama haya hayaendi haraka,” alisema Lowassa.
  Lowassa hakusema taarifa hizo wameomba kutoka kwenye vyombo gani, badala yake alisisitiza kuwa wametaka vyombo vinavyohusika kuwapa taarifa rasmi juu ya suala hilo.

  JWTZ, wasomi wazungumzia
  Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania ( JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa lipo juu ya uwezo wake.
  “Hilo jambo lipo juu ya uwezo wangu, siwezi kulizungumzia tuna mipaka ya taarifa gani tunaweza kutoa kwa vyombo vya habari. Siyo kila jambo linatangazwa, mengine yanakwenda kimyakimya,” alisema na kusisitiza: “Siyo kila jambo tunalofanya ni lazima tuseme... mengine yana hasara zake.”
  Lakini, Mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, Profesa Abdallah Safari alisema suala la mipaka ya nchi linasimamiwa na sheria za kimataifa ambazo alisema lazima ziheshimike.
  Profesa Safari ambaye pia ni mwanasheria alisema sheria hizo za kimataifa zinaitambua mipaka iliyowekwa na wakoloni wakati wa Mkutano wa Berlin uliofanyika mwaka 1884, hivyo lazima kila nchi iheshimu.
  “Wakoloni walivyogawa mipaka, Tanzania na Malawi kwa upande wa Ziwa Nyasa ulikuwa ni katikati ya ziwa hilo na Malawi wanaelewa. Wanachofanya ni uchokozi tu wa kutafuta vita visivyokuwa na sababu,” alisema Profesa Safari na kuongeza:
  “Kuna wakati kulikuwa na mgogoro kama huu kati ya Libya na Chad. Kulikuwa kuna eneo lililokuwa na mafuta, Libya ikataka kulichukua lakini mwisho Chad ilikuja kushinda kwa sababu eneo lilikuwa lao kwa mujibu wa mipaka ya kikoloni. Kwa hiyo hata hili la kwetu mipaka rasmi ni ile iliyowekwa na mkoloni katikati ya Ziwa Nyasa,” alisema.
  Alisema katika baadhi ya mipaka iliyotenganishwa na mito, ipo baadhi ambayo huwa na tabia ya kuhama na kwenda upande mmoja, lakini tatizo kama hilo halipo kwa Ziwa Nyasa hivyo, Malawi haina sababu yoyote ya kuleta usumbufu.
  “Kwa maana hiyo, naweza kusema tu kuwa, Malawi wanachotafuta ni uchokozi kwa sababu hizi sheria za kimataifa wanazifahamu,” alisisitiza Profesa Safari.
  Kwa upande wake, Profesa Mwesiga Baregu ambaye amebobea katika eneo hilo la uhusiano wa kimataifa alisema ni vyema nchi zote zikaendelea kuzungumza na kumaliza suala hilo.
  Alionya nchi zote kutochukua hatua za kijeshi akisema mazungumzo ndiyo njia bora zaidi ya kumaliza suala hilo.
  “Nchi zote ziepuke hatua zozote za kutumia jeshi, kwa sababu hatua za kufanya hivyo zitakuwa na madhara siyo tu kwa Tanzania na Malawi ila katika nchi zote za SADC,” alisema Profesa Baregu.
  Profesa Baregu alisema endapo hakutakuwa na matunda katika mazungumzo kati ya Malawi na Tanzania, ni vyema suala hilo likafikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice- ICJ).

  “Jambo kama hili lilishatokea kati ya Cameroon na Nigeria, walikuwa wakigombea eneo lenye utajiri mkubwa tu wa mafuta, mgogoro ule ulimalizwa na ICJ ambapo Cameroon walionekana ndio wenye haki,” alisema.
  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alitaka mgogoro huo wa utatuliwe kwa njia ya majadiliano huku akisisitiza kuwa sheria za kimataifa zinapaswa kuzingatiwa.
  Profesa Lupumba alisema sheria ziko wazi kuwa nchi zinazotenganishwa na bahari au ziwa mpaka wake huwa katikati ya eneo la maji na kwamba kama hilo litazingatiwa hakuwezi kuwa na mgogoro tena baina ya pande hizo mbilii
   
 2. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Hawa Malawi mbona wanacheleweshwa kwanza ile sio nchi ni mkoa wa Tanzania. Angekuwa Nyerere tayar kashaturudishia mkoa wetu. Wanapaswa kupigwa barabaraa sababu wamerusha ndege zao za msaada nchini kwetu
   
 3. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  .............mtu akikugusa makalio hata kama hauna nguvu utajitutumua, ole wao Malawi na wale waliowatuma
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,584
  Trophy Points: 280
  Upumbavu kama huu kamwe ulikuwa hauwezi kutokea wakati wa Mwalimu...Eti kamati ya mambo ya nje, Ulinzi kutaka maelezo kuhusu mgogoro!!!! RIP Mwalimu.

  SUALA la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Malawi na Tanzania, limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutaka kupewa maelezo juu ya mgogoro huo.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  EL ni lazima atumie vyema kila nafasi anayoipata ili aonyeshwe kwenye Tv.
  Can u imagine wao kama ndio kamati ya Ulinzi wanataka maelezo ya nani?
  Mimi nadhani iitwe kamati ya 'Kupokea Maelezo' yanayohusiana na Ulinzi na mambo ya nje.
   
 6. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Vita sio suluhisho kwa kuwa mwisho wa yote maongezi ni lazima.
   
 7. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Nchi ikikosa uongozi thabiti ata sisimizi nao watasumbua tu.. hawa tuliowatoa kwenye kimasomaso cha ukoloni leo wanataka kujua mipaka zaidi ya sisi!!! Natumai kama hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya busara zaidi basi mturuhusu wenye nia thabiti na nchi hii tuwashike maka..lio hawa jamaa wa Malawi (Nyasa Land). Tatizo Mkulu anacheka cheka saaaaaaaaana ata kwenye mambo mazito kama haya
   
 8. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Huyu mama - Rais wa Malawi iaonekana anatumiwa ili biashara ya silaha ifanyike. Nadhani hajui Banda nini kilimkuta mpaka akaacha chokochoko miaka ya 70. Huyu mama anatapatapa, kesha kubali ushoga wakati waliomtangulia waliukataa, kisa misaada naameipata. Mabepari wanataka kumtumia ili mwisho wa siku nchi yetu ianze kununua silaha kwa malipo ya madini hasa uranium. Wazungu wameona wakitupatia dola uchumi wetu utakuwa mzuri hivyo ni bora waanzishe vita.
  Kuhusu utafiti wa mafuta wanaofanya pia ni kigezo, wazungu wameona tumeanza kuwa makini upande wa mafuta na rasilimali, wanataka mafuta yawe Malawi ili wafaidike.
  Serikali ifanye uchunguzi Who is behind this chokochoko? Malawi peke yake haina ubavu....!
   
 9. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  EL anakunyima usingizi teh teh teh naona Povu halikukauki
   
 10. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  sasa nimeanza kumwamini EL km la Mto Nile alilimaliza hili lisingechukua siku hata moja kwake, aangalie tatizo ni nini hasa mbona hata Ramani zinawaweka mbele waMalawi kuhusu hili Ziwa Nyasa? nani anatakiwa azibadil ili mpaka urudi katikati ya ziwa
   

  Attached Files:

 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Miaka yote aliyokaa madarakani mbona hakutatuwa huu mgogoro? kilimshinda nini? wacheni kusifia mambo yasiyosifika.

  Nna uhakika Kikwete na uzoefu wake wa Diplomasia za Kimataifa ataweka tena rikodi nyingine ya uongozi wake mahiri kwa kutatuwa hili tatizo. Sina wasi wasi kabisa na Kikwete kabisa kwenye mambo haya.
   
 12. c

  chama JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Zomba,
  Mwalimu na Banda walikuwa mahasimu wakubwa hilo linaeleweka cha zaidi wote waliheshimu mipaka na ndiyo sababu kuu tumekuwa karibu na amani muda wote hizi chokochoko anazozileta huyu mama hakuna atakeyeweza kuzivumilia mh. Kikwete anafahamu wazi ardhi ya Tanzania haipo kuchezewa na mtu yeyote yule; italindwa kwa nguvu zote !!

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 13. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Imani bwana, wakati mwingine ni mbaya sana. Eti Kikwete, kikwete, kikwete!!! Mbona nchi imeyumba namna hii kama mlevi wa gongo!!!!! Hakika watu aina ya zombe ndiyo mnaoendelea kuipeleka shimoni nchii hii kwa kumpa rahisi sifa zisizo na mbele wala nyuma. Kama kuna kosa ambalo watanzania watajutia katika historia ya nchi hii ni kumchagua nanii kuwa mkuu wa nchi.
   
 14. C

  Choi Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kuna Mmalawi mmoja tulienda naye semina ughaibuni, akaulizwa anatokea wapi akasema Malawi, na kila mtu akawa anashangaa hajawahi kuisikia hiyo nchi, swali lililofuatia kuna nini maarufu huko Malawi ambacho akikitaja watu watapata picha, hakuwa na cha kusema. mwishowe akasema tuko kusini mwa Tanzania, hapo kila mtu akasema ahhh. Baadaye akawa anasikitika sana kuwa kila anapojitambulisha inamlazimu kutaja Tanzania ili ajulikane ametoka wapi! sasa mimi naona hao Malawi pamoja na uchokozi wanatafuta umaarufu pia
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,103
  Likes Received: 6,565
  Trophy Points: 280
  wanatuzungusha tu, watakuwa walishauza hilo eneo siku nyingi,
  sisi tunabaki kushangaa tu.

   
Loading...