Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje chini ya uenyekiti wa Edward Lowassa ipo ziarani Morocco.Waheshimiwa wetu hawa wakiwa huko wametoa msimamo unaofanana na ule wa Morocco lakini unaokinzana na ule wa serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la Sahara Magharibi.
Kamati ya mambo ya nje imetoa msimamo na kudai Tanzania inaunga mkono Morocoo katika harakati zake kwa Sahara Magharibi wakati inavyofahamika ni kwamba Tanzania kwa maana ya serikali haiiungi mkono morocco kwenye suala hilo.
Swali:Je kamati ya bunge ya mambo ya nje inayo mamlaka ya kutoa msimamo kwa niaba ya serikali?kama hapana kuna ushawishi gani wamekumbana nao waheshimiwa hawa wakiwa huko morocco kiasi cha kuwalevya na kuamua kutoa msimamo huo ambao ni Tofauti na msimamo wa serikali?
Jibu la swali lako ni rahisi sana. Hawana mamlaka hiyo na ushawishi pekee ni fedha walizopewa. Timing ya safari yao na choice ya nchi ya Morocco haikuwa ya bahati mbaya. Hawa jamaa wamethibitisha kwamba hawan integrity na nitashangaa kama Serikali haitawashukia ku-denounce upuuzi huu na hata kupendekeza Bunge liwawajibishe kwa kuiuza nchi kwa vipande thelathini vya fedha.