Baada ya wabunge kutaka ongezeko la posho kutoka 300,000 hadi 500,000/= kwa siku. Serikali imewaonea huruma watumishi wake ambao nao husafiri kwenda Dodoma na kulipwa posho ya malazi ya chini kabisa huwafanya kuishi maisha ya kubangaiza kwa kulala Guest za vichochoroni. Kutokana na Wabunge kuutangazia umma kuwa posho ya laki 3 haitoshelezi kwa siku kwa waheshimiwa Serikali pia imeamua kubalisha waraka wake wa posho ambao utaanza kutumika Machi 2014. Ambapo Mtumishi aliyekuwa akipata posho ya 45,000/= mfano Dereva na Mhudumu wa Ofisi sasa atakuwa anapata 80,000/= na wale Maafisa waliokuwa wanapata 65,000 na 80,000 watakuwa wanapata posho ya Tsh 120,000/= kwa siku hii ni kuwafanya waweze kumudu gharama za maisha wanapokuwa wamesafiri kikazi.