Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Posts
2,970
Reaction score
871
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.

Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA. Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga. Nawasilisha.
 
Asante kwa taarifa Regia, tunategemea hekima,umakini na utashi mkubwa katika mchakato wa kumpata mwakilishi. Ikumbukwe kua uchaguzi huu ni kipimo cha mabadiliko na ukuaji wa nguvu ya chama baada ya uchaguzi wa mwaka jana na kasi ya kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
 
Dada sisi bado tupo na pia I hope kuwa Jimbo litakwenda kwa CHADEMA na Mungu akusaidie sana katika harakati hizi na nawatakia kila la kheri katika kupitisha jina la Mgombea ubunge huyu
 
Asante Regia kwa taarifa. Nje ya mada hii sisi wananchi tumesononeshwa sana na kuumia mno na kauli ya mbunge mwenzenu Mh Shibuda. Yaani nilitamani kupiga simu yangu kwenye screen wakati huyu mbunge akichangia mambo ambayo yanaonekana wazi wazi kuwa si mwenzetu kabisa. si mimi tu ila wananchi wengi wapenda haki na usawa wameumia sana.

Nakuomba Regia fikisha suala hili mbele ya kamati kuu, sisi tunapendekeza mtu huyu apumzishwe maana si mwenzetu. ni vyema tukatibu ndonda leo badala ya kulifuga cause linaweza lisitibike tena badala yake kama lipo mguuni basi lazima ukatwe kuokoa maisha. sisi hatutaki tufike huko.

Fikisha ujumbe wa hao wapiganaji-- tunawaombea mafanikio. najua wananchi wakakuwa barabarani kila mnapita cause mmebeba sura ya Tanzania mpya - Tanzania yenye Tumaini Jipya. Mungu awababariki sana tupo pamoja nanyi kwenye sara na dua zetu. Peoples Poweeeer.
 
Kuwa makini sana maana magamba wameweka Kamishina wa Nishati kugombea jimbo na as we speak amepata kura 588 kati ya 928 zilizopigwa. Ikumbukwe huyu ni Jamaa wa akina Jairo so vibahasha vyaweza kutembea kwa sana..
 
thanx kwa taarifa ! endelea kutupa update za huko kadri utakavyoona inafaa ili tuzid kufuatilia uchaguzi huo muhimu kwa chama na kwa wakazi wa Igunga
 
Dada Regia, mimi binafsi nina wasiwasi na common sense na reasoning capacity ya Magale Shibuda, inaonekana kasi yetu haiwezi ni bora apumzishwe hata kama ni kupoteza kiti cha ubunge na jimbo la maswa kwa ujumla.
 
Asante Mhe. Regia, nimeipenda sana hii comment "Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA", nimezipenda sana hizi dalili, maana uchaguzi mdogo wa Busanda na Biharamulo, sio tuu ni dalili za awali, bali ilikuwa mwanzo mwisho, Chadema iyatwae majimbo yale, ila matokeo sote tunayajua!. Matokeo ya Igunga ndicho kipimo cha 2015!.
 
vp rostam naskia hapokei simu ya mwenyekiti wake? na yeye ndio alikuwa ananunua fulana, vp kwa msimamo huu wa RA magamba watatoka kweli?
 
Kuna thread humu inasema mgombea wa cdm ameshachaguliwa. Nadhani kinachoenda kufanyika Igunga ni taratibu tu za kichama ili kumuidhinisha!

Kikubwa ninachowaomba cc ni kuweka mkakati wa nguvu na kujipanga vema ili kuwakabili ccm na cuf maana dalili zinaonesha kunaweza kukatokea kugawana kura na mambo yakawa kama Tarime! Mnatakiwa kujipanga kwelikweli!

I wish U all the best!
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.


WEWE Regia mTema umechanganyikiwa, Igunga utaisikia hewani na usizani kelelel za chura zinamzuia mbuzi kunywa maji.

Igunga itabaki kuwa jimbo la ccm na kama kutoka kwa rostam kumewafanya mzani jimbo liko wazi mmechelewa jimbo linawenyewe.
 
hebu kaeni hukohuko Iginga na mumfukuze yule kinyesi Shibuda
 
Kila la kheri makamanda. Ila huzuni yangu pekee ni pale ninapokumbuka kwamba ndani ya basi letu la mageuzi kuna kitu kinachoitwa Shibuda, hasira inanipanda ila kwa furaha naona mlango ulio wazi mbele.

Safari ya kutoka misri ikuelekea nchi ya ahadi imeanza, haijalishi kuna watu wamejiunga na wapambanaji huku wakiwa na ndoto za unyapara wao wa huko misri. Ni jambo lililowazi kwamba hata kama hawakuchinjiwa baharini, basi watamezwa na ardhi jangwani.

Ushauri wangu kwa makamanda ni huu, Shibuda hakuna haja ya kumwendea haraka, fanyeni kumchomekea tu kidogo kidogo kwani yeye mwenyewe ataitoa gari yake njiani na kuelekea bondeni huku akiiacha chadema imara barabarani. Asipewe dhamana yoyote ndani ya chama, tafadhali zingatieni hilo.
 
Imani ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo bayana na mambo yooote yasiyoonekana, Kwa sasa utamu wa mambo na siasa unaanza.

Mungu atupe njia kwa kweli
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Igunga ni jimbo jipya la cdm since siku ile rostam anaachia ngazi na mamia ya wana ccm igunga kurudisaha kadi za uanachama wa ccm.viva cahdema the leading political party in tanzania
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.

Kwa mujibu wa habari za uhakika ni kwamba chadema itashika nafasi ya
tatu katika uchaguzi huo, na kama chadema isipo simamisha mgombea
basi cuf itashinda lakini kwa kua vyama vya upinzani vinaenda kugawana
nusu ya nyama huko igunga, basi mzee kafumu ataingia mjengoni kwa mbwembwe sana.
 
Kuna thread humu inasema mgombea wa cdm ameshachaguliwa. Nadhani kinachoenda kufanyika Igunga ni taratibu tu za kichama ili kumuidhinisha! Kikubwa ninachowaomba cc ni kuweka mkakati wa nguvu na kujipanga vema ili kuwakabili ccm na cuf maana dalili zinaonesha kunaweza kukatokea kugawana kura na mambo yakawa kama Tarime! Mnatakiwa kujipanga kwelikweli!

I wish U all the best!
Kiutaratibu mgombea akishapita kwenye kura za maoni lazima jina lake lijadiliwe na kamati kuu ya chama.Kilichomo kwenye hiyo thread ni matokeo ya kura za maoni.Kamati kuu ndo mamlaka ya mwisho kutaja jina la mgombea.

Hata kama mara nyingi aliyeongoza ndiye ambae hupendekezwa na kamati kuu lakini bado hatuwezi kujustify hivyo.
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.

aksante sana dada Regia! pokea heshima zangu nyingi. tunaatarajia kuwa uamuzi wa kwenda kufanyia kikao igunga ni jitihada za kujaribu kupunguza uchakachuaji wa wagombea....tunatarajia uteuzi utakaokubalika na wengi..

Mungu awatangulie!
 
Back
Top Bottom