Kamata Kamata ya CHADEMA Mbeya yashika kasi

Kamata Kamata ya CHADEMA Mbeya yashika kasi

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Kamata kamata ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwasweka ndani, inaendelea kushika kasi mkoani Mbeya baada ya Katibu wa chama hicho Wilaya ya Rungwe, Award Karonga kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa kiongozi huyo alikamatwa juzi kwa tuhuma mbalimbali za jinai ikiwemo uchochezi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Karonga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Hamasa Taifa wa CHADEMA alikamatwa na maofisa wa polisi akiwa katika Mtaa wa Katumba uliopo Kata ya Ibigi wilayani humo.
Imeeleza kuwa upelelezi wa tuhuma za kiongozi huyo unakamilishwa, ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Vijijini wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Getruda Japhet kwa tuhuma za uchochezi.
chanzo :Nipashe
 
Wahuni wote lazima wabanwe na washughulikiwe kisheria
 
Nyie ccm hamjitambui mwisho wenu umekaribia.
 
Back
Top Bottom