Kamata kamata Dar kwenye no entry Road

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Toka juzi katkati ya jiji la Dar hasa mitaa ya makunganya, jamhuri karibu na roundabout ya Bharklesa, Bilcanas na kwingineko kulikuwa tafrani kubwa baada ya kuanza operation ya kukamata magari yaliyokuwa yana pita no entry road sign. Hizi alama nakumbuka ziliwekwa kitambo zikawa kama zilikosewa maana nyingine hadi zilizibwa kuonyesha kuwazijaanza kutumika.

Hata jana askari niliyeongea naye alikiri kuwa nyingine ziliwekwa kimakosa. Kwa ujumla ni kama zilikuwa zimetelekezwa kwani nilikuwa nayashuhudia hata magari ya kawaida ya polisi yakizitumia njia hizo.

Ghafla juzi operation kubwa ikaanza na kuacha vilio vikubwa kwani ulikuwa unaandikiwa makosa mawili la kuingia no entry Road na kufanya eti blockage kwa magari mengine. Kwa kweli kulikuwa na kama kukomoana hivi kwani kuandikiwa makosa mawili kulionyesha wazi kuwa lengo si kutoa taadhali bali kuna agenda nyuma yake. Mtu mmoja nilimsikia akisema " Ukisikia kuwa hali ya uchumi sio nzuri Tz muelewe.

Je, wewe umelipokea vipi jambo hili?
 
Ni vyema tukakubali kupambana na hali tuliyonayo kwa sasa. Hata iweje huna kwa kulilia ukasikilizwa so pambana tu na hali
 
I am a victim as well, nilikamattwa na hao xxwa, I hate them and I feel happy when I see them fixed
 
Hata wenye magari ya mtumba yaliyotumika miaka zaidi ya 20 nao wanatakiwa "waishi Kama mashetani " tumewasikia....

Parking pekee Elfu tano

Speed hadi laki mbili
Hujafanya service hujanunua mafuta hujalipa Insurance, yet hawaridhiki.......
Hii nchi kuna watu wana chuki Sana na maisha ya wengine.......
 
aisee mnaoishi dar kwa kweli naona kama mko jehanamu, sio wa mikoani tunapeta tu, na hawa trafic wangekuwa na uwezo wa kukaa angani wakawashia tochi yao na ndege basi sidhani kama ndege zingeruka, ila sema uwezo hawana manake mapato yanavyokusanywa unakamuliwa kila kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom