Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Kuna wakati kama haki hakuna na wanapaswa kutoa haki awazitoi hizo haki ni lazima itumike nguvu ya ziada ili haki ipatikane. Kwahiyo msiseme ni machafuko ni katika harakati za kutafuta haki na usawa.
====================
Wazazi Mkoani Mtwara wametakiwa kuzungumza na vijana wao juu ya umuhimu wa kutunza amani kuanzia ngazi ya familia na kuepuka kurubuniwa na watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuhamasisha kuvuruga amani.
Hayo amebainisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP ) Suleiman Oktoba 21,2025 alipokuwa akitoa mada ya umuhimu wa kutunza amani kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu katika kipindi cha Mchakamchaka kinachorushwa kupitia redio Jamii Fm 90.5 ambayo ipo Kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara.
SACP Suleiman amesema hakuna uzoefu duniani kuwa vurugu au machafuko yamewahi kutatua migogoro, migogoro inatatuliwa kwa njia ya kistaarabu hivyo wananchi wa Mtwara wanatakiwa kuepuka ushawishi ambao utahatarisha amani kwa mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla.