VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kunatumika nguvu kubwa ya maneno na matendo kuhusu kutaka kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,Freeman Mbowe. Mbowe alipotajwa na Makonda na kuitwa Central Police,alikosoa uhalali wa kutajwa na kuitwa kwake kule Dodoma. Hakwenda.
Akataka utaratibu wa kisheria ufuatwe. Utaratibu wenyewe ni mwepesi tu,ni kuandika wito wa kumwita kwake na kumfikishia. Basi. Wapi pagumu katika utaratibu huo? Mambo ya kumwita mtanzania kupitia runinga na kumwaga mikwara ya kutosha na kutisha si madogo.
Hakuna anayepinga mtanzania au mgeni yeyote kukamatwa au kuitwa na kuhojiwa. Kila mmoja wetu anatamani utaratibu ufuate. Kwanini media itumike hadi kufunika utaratibu? Kwani,kuna ajenda gani dhidi ya Mbowe wa CHADEMA? Kadiri mikwara inavyozidi ndivyo inference ya kwamba hakuna jema inavyopata mshiko.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam