Nimekuwa nikimsikiliza huyu jamaa, akiwa anafanya mahojiano mbalimbali. Iwe na BBC, DW, na pia vyombo vya habari vya hapa nyumbani. Uongeaji wake huwa wanikosha sana.
Jamaa ametulia, anaongea 'point' tu, kila mtu hutamani kumsikiliza. Ninaamini haya matukio ya ujambazi Dar es Salaam yataisha kabla hakujacha.
Watu kama hawa tukiwa CCP walikuwa wana pass out angalau na kirungu kimoja, hususani cha ukakamavu.
Ukiwaacha Thobias Andengenye na Diwani Athumani, Sirro atakuwa Bonge la IGP.
Wale watu wa umri wangu na kunizidi wanajua kwamba enzi hizo mtu akipata habari kwamba Rais anatarajia kumteua mtu fulani katika nafasi ya juu, akitaka kumharibia ni kuandika hadharani kwamba (mfano) fulani anatarajia kuteuliwa kuwa waziri wa elimu. Hiyo ilitosha kwa mtarajiwa kukosa sifa. Sasa kama kweli mnampenda huyo mnayemtaja aje siku moja awe Boss basi kuweni na vifua vya kuhifadhi siri msije mkamharibia bila sababu ya msingi. Kama anafanya kazi nzuri Rais atamgundua kwa sababu urais ni taasisi kubwa yenye nyezo kutosha kuona kila kinachofanyika kila siku iendayo kwa Mungu. Nani alijua kama Makonda angekuwa mkuu wa mkoa tena Dar es Salaam. Mwacheni Kamanda apige kazi halafu vyombo husika vitamuibua.
Aliwahi sifiwa hadi na Gazeti la Mwanahalisi, kwa kuzima mapigano ya wakulima na wafugaji huko Ikwiriri.