MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,612
- 21,346
Leo tuliofanikiwa kuwepo gerezani tumeshangazwa sana na moyo kushtuka paah baada ya kumuona mh rais Magufuli akiendesha gari la mwendokasi.
Mara ya kwanza tulidhani anaingia ndani kupiga picha lkn ghafla tukamuona amekaa kiti cha dereva na kuanza kuendesha.
Kamanda wa usalama barabarani tunaomba unieleweshe haya yafuatayo na ikiwezekana kuchukua sheria mara moja (maana alisema hata Gari LA rais likivunja sheria linaruhusiwa kukamatwa)
- Ni lini rais amekata leseni daraja C inayompa uwezo wa kuendesha magari ya abiria?
- Kwanini alitembea na spidi inayokadiriwa kufika 45 mpaka 51km/h kwenye sehemu yenye msongamano mkubwa wa watu kama pale kituoni?
- Ni kwanini aliyafanya yote haya mbele ya askari wengi wa usalama barabarani na hamna hata mmoja aliyechukua hatua.
H.Mchange