Kamanda Mawazo apata Mwana CCM mwingine

Kamanda Mawazo apata Mwana CCM mwingine

Fred Matuja

Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
5
Reaction score
4
Kutokana na juhudi za Kamanda Mawazo Alphonce alieko Mkoani Kagera kwa ajili ya M4C, jana jioni familia ya Kagasheki imehamia Chadema. Mdogo wa Waziri Hamis Kagasheki anaeitwa Mbubarak Kagasheki pamoja na nduguye mwengine walimkabidhi kadi zao za CCM kamanda Mawazokwenye uwanja wa Rwamishenye.

Hotuba ya Mawazo iliwafanya watu kutokwa na machozi ya uchungu dhidi ya mfumo uliopo. Diwani wa moja ya kata za mjini Bukoba alilia hadharani na kusema mara ya mwisho alilia machozi baada ya kusikia hotuba ya Mtikila. Kada mwingine toka CUF anaejulikana kama Zainabu nae alirudisha kadi yake. Mpaka saa moja kasoro watu waligoma kuondoka uwanjani.

Wananchi walimchangia Kamanda Mawazo takribani sh. 200,000. Leo hii, Mawazo na timu yake (Husna na Hamis) wanahamishia ziara Karagwe kwa ziara ya siku 5.
 
Si nilisikia kamanda Mboe kasema hapana kupokea raia kutoka ccm au?
 
Sasa la ajabu ni lipi? kwani kakako akiwa waziri na wewe ni waziri? au lazima ufuate misingi ya chama chake?
 
Amesema hawatapokea dakika za lala salama, yaani wale watakaokuwa wametemwa kwenye nafasi za kugombea kama Shibuda alivyojiunga!
Asante mkuu, tena huyu baba ni janga kwa CHADEMA na bora wamemgundua mapema!
 
Kamanda Mawazo Big Up. Biashara ni asubuhi mahesabu 2014 na 2015
Kutokana na juhudi
za Kamanda Mawazo Alphonce alieko Mkoani Kagera kwa ajili ya
M4C,

jana jioni familia ya Kagasheki
imehamia Chadema. Mdogo wa Waziri Hamis Kagasheki anaeitwa Mbubarak
Kagasheki pamoja na nduguye mwengine walimkabidhi kadi zao za CCM
kamanda Mawazokwenye uwanja wa Rwamishenyi.

Hotuba ya Mawazo iliwafanya watu
kutokwa na machozi ya uchungu dhidi ya mfumo uliopo.

Diwani wa moja ya kata za mjini
Bukoba alilia hadharani na kusema mara ya mwisho alilia machozi baada ya
kusikia hotuba ya Mtikila.

Kada mwingine toka CUF anaejulikana
kama Zainabu nae alirudisha kadi yake. Mpaka saa moja kasoro watu
waligoma kuondoka uwanjani.

Wananchi walimchangia Kamanda
Mawazo takribani sh. 200,000.

Leo hii, Mawazo na timu yake (Husna
na Hamis) wanahamishia ziara Karagwe kwa ziara ya siku
5.
 
Asante mkuu, tena huyu baba ni janga kwa CHADEMA na bora wamemgundua mapema!

Kama CCM wanataka wajiunge sasa hivi watapokelewa ila wakipigwa chini kwenye kura za maoni hawatapokelewa
 
Go kamanda,go go!!!Tupo sambamba kamanda Mawazo hakuna kulala mpaka kileleweke....
 
Hii ndiyo ile familia ambayo ilisemwa kuwa waliumbwa kutawa?The Kagashekis?CDM kuweni makini na hawa watu
 
kutokana na juhudi za kamanda mawazo alphonce alieko mkoani kagera kwa ajili ya m4c, jana jioni familia ya kagasheki imehamia chadema. Mdogo wa waziri hamis kagasheki anaeitwa mbubarak kagasheki pamoja na nduguye mwengine walimkabidhi kadi zao za ccm kamanda mawazokwenye uwanja wa rwamishenye.

hotuba ya mawazo iliwafanya watu kutokwa na machozi ya uchungu dhidi ya mfumo uliopo. diwani wa moja ya kata za mjini bukoba alilia hadharani na kusema mara ya mwisho alilia machozi baada ya kusikia hotuba ya mtikila. kada mwingine toka cuf anaejulikana kama zainabu nae alirudisha kadi yake. Mpaka saa moja kasoro watu waligoma kuondoka uwanjani.

wananchi walimchangia kamanda mawazo takribani sh. 200,000. leo hii, mawazo na timu yake (husna na hamis) wanahamishia ziara karagwe kwa ziara ya siku 5.
kamanda mawazo nakwamia kweli wewe ni kamanda wa kweli bila utani wapelekeshe hao magamba mpaka wote wahamie chadema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom