Mungu hataiacha nchi iingie kwenye umwagaji damu hata shetani akiwakalia utosini kuandika ujumbe wa uchochezi.
Mhe. Lema ninaposoma ujumbe wako hapo juu ninaona umejaa uchochezi. Ni ujumbe wa mtu aliyekata tamaa kama ulivyoandika mwenyewe. Aliyekata tamaa hawezi kutufaa kukaa kwenye nafasi ya uongozi maana sisi bado tunakiu kuiona Tanzania ikiwa na utulivu.
Kiongozi yeyote mwenye utu wa ndani lazima afikiri kutoa ushauri wa kujenga badala ya uchochezi kama unavyofanya. Unakemea propaganda kwa mkono wa kushoto halafu kwa mkono wa kulia unafanya. Ninaamini dhamira ba dhamiri yako vinashuhudia kwamba umeandika ujumbe katika hali ya kulipuka. Kama ulikuwa katika utulivu basi, Mungu achunguzaye mioyo akusaidie.
Nimesoma taarifa ya kifo cha mawazo ngaa kwa ufupi (
mwanzo | Mwananchi), nimebaki na maswali mengi. Moja, mwandishi anaposema Mawazo alichukua pikipiki na kuanza kukimbia, tujiulize alibaki amefanya nini hata akakimbia? Gari lililomkimbiza je, ni gari la Polisi au watu waliokuwa wakivutana naye? Au je, ni wananchi wenye hasira kali baada ya kuona pengine amefanya jambo lisilokubalika?
Pia, nimejiuliza, huyu anayeonekana ni mamluki kwenye kikao cha CHADEMA, ni nani aliyemruhusu kuingia? Utaratibu wa vikao vya siri vya ndani vya Chadema unaruhusu watu kuinglililotokea b Huyo aliyekuwa kwenye kikao na kuonekana mamluki je, ni mwanachama halali wa CHADEMA? NA kama ni mwanachama halali alipewa vipi nafasi ya uongozi kabla ya kujiridhisha kwamba si mamluki? Ni kwa nini taratibu za ndani za chama hazikutumika kumshughulikia mamluki na badala yake ugonvi ukaonekana ndiyo suluhisho hata Mawazo akakimbia?
Mhe. Lema, ninafikiri kabla haujaenda mbele kulaumu POLISI ulaumu mfumo mbovu ndani ya CHAMA CHAKO unaopelekea tatizo linapogundulika, e.g mamluki, kushindwa kulishughulikia kwa staha. Matokeo yake ndiyo hayo. Sasa, ninyi mmelea mfumo mbovu, tatizo likitokea unakimbilia kulaumu polisi. Hiyo ni tabia ya kuhamisha lawama kwa wengine.
Huyo ndugu yetu aliyeuawa ni Kiongozi mkubwa wa chama, Ngazi ya Mkoa. Je, alikuwa na akina nani anapoketi vikao vya ngazi ya kata? Je, kuna wengine ambao ni viongozi wa chama chako waliojeruhiwa na hao unaowatuhumu kwamba wamemwuua Mawazo??
Unapokwenda kumhusisha mkuu wa wilaya na kifo hicho, je unataka kuuaminisha umma wa watanzania kwamba amehusika???
Mhe. Lema, nafikiri uchochezi wa aina yako hauwezi kulisaidia taifa hili. Hatuwezi kuwa ni viongozi ambao tunaandika vitu na kuzungumza vitu vya kubuni na uchochezi.
Binafsi, ndipo nimemsikia kwa mara ya kwanza ndugu huyo aliyefariki, baada ya kusoma habari kupitia Mwananchi digital. Hivyo basi, niombe na nitoe wito kwa Watanzania na hasa viongozi, kujiepusha na matumizi mabaya ya nafasi za uongozi. Kauli ya kiongozi inaweza kupelekea uharibifu mkubwa inapotolewa pasipokupima. Mhe. Lema umenena habari za propaganda kwamba haziwezi kusaidia taifa. Sijajua kama umeelewa kwamba ulichoandika ndiyo hayo hayo ambayo unayalalamikia.