Kamanda Kova apiga stop maandamano ya Libya - Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kova apiga stop maandamano ya Libya - Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by POMPO, Mar 24, 2011.

 1. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jumuia ya ma imamu iliyokuwa imeandaa maandamo makubwa ya kupinga uvamizi wa nchi za magharibi nchini Libya, ambayo yalikuwa yafanyike kesho ljumaa yamepigwa STOP na Kova

  Chanzo: TBC habari
   
 2. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Something is Wrong somewhere "Naona watu sasa kila kitu ni kuandamana,How can you protest on something that not even Libyan themselves are protesting for??" I would bet they don't have a clue on what is going on in Libya.

  I personally have 2 friends in Libya and They are all supporting the invasion as they have been oppressed enough not even the Arab league is protesting, We must be realistic and not pessmistic!!
   
 3. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No comment
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  matatizo ya kuto kutafakari kitu, wengine wakiwekewa pilau ni mbele kwa mbele hakuna kufikiria
   
 5. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mambo haya wakati mwingine sielewi kabisa........ labda ni udini
   
 6. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uzuri wa hawa jamaa upatikanaji wao kirahisi. Ukiwatangazia usiku huu kwamba kesho saa kumi na mbili asubuhi kuna maandamano ya kumuunga mkono Osama bin Laden na maandamano yataanzia Manzese na kuishia Kidongo chekundu utaona attendance yao. Utashangaa wapo barabarani kibao na mabango yao.

  Wengine wanaandamana wakiwa na hasira lakini ukiwauliza wanadai nini watakwambia tumechoka kuonewa na serikali!!!!

  Mambo hayo!
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ofcourse Mkuu, walipanga after swala ya ljumaa, but wamekubaliwa wafanye mkutano hapo biafra kino.
   
 8. w

  wakwetu 2 Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  nikweli kabisa tena unaweza kuwapata wengi ila wakiambiwa waandameni kupinga mambo mabaya ndani ya nchi watasema uchochezi na uvunjifu wa aman, sijui nini

  :angry:
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mufti Iddi Simba alidai maandamano ya CHADEMA kudai haki za watanzania kuna ajenda ya siri............Mungu amfichi mnafiki, leo hii mnadai maandamano ya kupinga Libya kuvamiwa....Mufti nakuuliza:

  1. Una uchungu na Walibya kuliko Watanzania?
  2. Una maslahi gani na Libya mpaka ukubali kuandamana kwa niaba yao?
  3. Waliwaomba mbona wao wanafurahia uvamizi wa nchi za magharibi?
  Mnatuchefua, ni watanzania wenzetu lakini sometimes MNAKERA MH!
   
 10. k

  kikule Senior Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  gadaf kawasaidia hvyo kawajengea msikiti hvyo hakuna kuhoji mamabaya yake
  Inasikitisha kuumia kwa ajil ya watu ambao wanafurahia kuondolewa kwa dictator
   
 11. P

  Percival JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mie nakubaliana nawe kabisa kuwa watu lazima wajikomboe na tawala za madikteta kama yanayotokea huko Libya, lakini pia naamini watu wawe na uhuru wa kutoa rai zao kwa maandamano ya amani hata kama hao watu wana rai tofauti na zetu.

  Hawa makamanda wa usalama lazma waelewe kua enzi za ubabe na kunyanyasa watu zinafikia ukingoni. Angalia huko Misri hao polisi waliokuwa wananyanyasa na kutesa watu wanavyo andamwa na wananchi sasa.
   
 12. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ni haki ya kidemokrasia...
   
 13. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ndo mlengo wao. Hata kama ni pesa haramu ukiwasaidia watakwabudu.
   
 14. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tunajua janja ya kupigwa marufuku maadamano ya aina yoyote hapa dar.?
  Waache wabane wataachia wenyewe.
   
 15. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Gaddafi alipoua raia zake kwa kuwalipua kwa makombora ya kurushwa na ndege hakuna aliyeandamana kupinga! Ama kweli akili ni nywele!
   
 16. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hawa awakumbuki siku Idi Amini DADA alipotuvamia na kutumia Askari wa LIBYA kutupiga leo eti Tunataka kuandamana ili tufanyaje????????? Huyu mtu mpuuzi sana anauwa watu wake anaambiwa analeta ujinga lazima akomeshwe na Badfo ataendelea kutumia Watu wake kama ngao lakini atatoka tu madarakani. mimi ni mmoja wa askari niliepigana vita mwaka 1978/79 sasa mnataka kuleta nini je wangeshinda leo mngewashabikia hawa Waganda na mashoga zao LIBYA???????????
   
 17. k

  kayumba JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwanini azuie maandamano yao, au kuna mambo ya inteligensia.

  Si haki ya Kova kuamua ni nani aandamane na ni nani asiandamane. Sijui kwanini viongozi wa Afrika hawajifunzi?

  Ipo siku tutakuja kuona minyukano baada ya polisi kuzuia maandamano ya vyama vya siasa na taasisi zisizo za serikali na za kidini.

  Hatukujifunza Arusha, Tunisia, Misri...............
   
 18. L

  Leornado JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Gadafi alikuwa amewaahidi kitu sasa wanaona mambo yanakuwa ndivyo sivyo, na msaada hawajapewa.
   
 19. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lakini si wana haki ya kikatiba ya ku express mawazo ( feelings zao) hata kama watawala au hata wananchi wengine hawazipendi? Waachwe wanaandamane!!
   
 20. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hawa wanaoandamana Libya, Yemeni, Bahrain, Syria, Saudi Arabia nk. wanawaona ni wajinga? Wananchi wa Egypt na Tunisia walipowatimua marais wao kwa kuandamana tunawaona wajinga?

  Nyinyi mashehe ubwabwa wa Bongo mnakereka na nini? Kwa hiyo ninyi mna uchungu wa hizo nchi kuliko raia wazawa?

  Ama kweli baadhi ya waislaam ni mbumbumbu wa bendera fata upepo! Hapa TZ tukiwaambieni twendeni tukaandamane mitaani kwa kudai haki zetu za msingi.....mnasema ooooh hapa kuna udini na hawamtaki Kikwete kwa vile ni muislaam. Sasa wenzenu wa nchi za Arabu wote ni waislaam na wameamua kuandamana kwa kudai haki zao za kimsingi hadi kieleweke.... halafu nyie mnasema mnataka kuingia barabarani kuwapinga.

  AMKENI NYIE WATU NA ACHENI UJUHA.....Yaani mnajifedhehesha sana kuliko mnavyojua! duuh
   
Loading...