Kamanda Halima Mdee kutikisa Bukoba Mjini leo

RWAMAIGI

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
361
Reaction score
105
Wadau,
Pamoja na sekeseke dhidi ya polisi aliyokutana nayo kamanda Mdee m/kiti wa BAWACHA tatifa na timu yake leo wanaendelea kutimua vumbi mkoani Kagera na sasa wako Bukoba mjini tiyari kuwasha moto katika viwanja vya Uhuru maarufu kama viwanja vya Mayunga.

Shamlashamla za kumpokea Mdee zimeanza mapema asubuhi,huku katika vijiwe mbalimbali watu wakitathimini na kupongeza uwezo wa CHADEMA wa kutengeneza wanasiasa wazuri.Hasa wakizingatia jinsi Mdee alivyoyatikisa magamba na polisi wake kote alikopita.

Wadau tutaendelea kuwajuza yanayoendelea na walioko karibu,karibu tuhudhulie kwa wingi.


 
Mdee anayapandisha pressure sana maccm, nasikia Tibaijuka yupo hoii hajielewi

Ziara ya Mdee Bukoba, majibu yake tutayaona 2015. Na kwenye uchaguzi wa serikari ya mtaa Dec.

Yale mama ya maccm huwa hayana ziara eh!

Go on Mdee with ur time
 
Ninapopata taarifa kama hizi moyo wangu unakuwa na furaha sana....Viva Halima Mdee, Viva Chadema...Viva..UKAWA...

2015...............CCM.............................MUST.....................................GO
 
wanamsimika nani kama mbunge bukoba mjini? maana bk imedorola kwa ugomvi wa watu wawili!
 
Mdeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee !!!!!!!!!!!!!!!!!! Chapa kazi dada Mungu atalipa tu. Usishawishike na vijisenti vya mifisadi vimewatafuna Zitto, Mwampamba, Shonza hatuwasikii tena.
 
wanamsimika nani kama mbunge bukoba mjini? maana bk imedorola kwa ugomvi wa watu wawili!

Huyu mama atachika mwenyewe! Watoto mtawapata halafu uchaguzi 2015 CCM ushindi 71 na UKAWA 29. Amini ama usiamini hayo ndo matokeo yenu.
 
Huyu mama atachika mwenyewe! Watoto mtawapata halafu uchaguzi 2015 CCM ushindi 71 na UKAWA 29. Amini ama usiamini hayo ndo matokeo yenu.
Ndio mulivyojipanga na wachina wenu muonyeni mwenyekiti wenu ataisia mitaroni na kuchomekwa majiti watanzania sio wale wa kale
 
Chadema wapo karibu sana kuishinda ccm,hii ni nchi yetu sote......mkituibia safari hii....basi nasi tutaanza kuwaibia
 
HISTORIA YA KURA ZA URAIS TANZANIA 1995 - 2010
Mwaka 1995 jumla ya kura za wapinzani zilikuwa 2,486,323, sawa na asilimia 38.17. Uchaguzi uliofuata wa mwaka 2000 wapinzani walipata jumla ya kura 2,309,123, sawa na asilimia 28.26 na kupungua zaidi mwaka 2005 walipopata kura 2,241,525 (sawa na asilimia 19.72. Mwaka 2010, upinzani ulipata kura 3,121,136. Ingawa kwa asilimia, kura hizo zilikuwa asilimia 37.16 pungufu ya asilimia za uchaguzi wa 1995, idadi ya kura za wapinzani ilikuwa kubwa kwa tofauti ya zaidi ya kura 700,000.

Kwa trend hiyo mwaka 2015 upinzani watashuka tena kwa takribani asilimia 13 au 11 kutokana na vurugu zilizosheheni katika chama cha Chadema na CUF. Zitto Kabwe na kundi lake na Hamad Rashid na kundile wote hawa watasababisha negative performance ktk matokeo ya ubunge na urais.

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Hivi kule Bukoba,ofisi za CHADEMA mkoa wa kagera zipo sehemu gani? ndugu RWAMAIGI nasikia hawana ofisi wanakutana bar ni kweli?
 
Last edited by a moderator:
:llama:HIZO NDIYO MBIYO ZA CCM IWE KTK UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA AU UCHAGUZI MKUU!

KINANA NA NAPE WAMEKITENDEA HAKI CCM. CHAMA KIMERUDISHA IMANI KWA WANANCHI SASA TUNATEGEMEA KUVUNA ASILIMIA 87 AU 88
 
Njia zenu zote za kajambazi tunazijua
 
Hivi kule Bukoba,ofisi za CHADEMA mkoa wa kagera zipo sehemu gani? ndugu RWAMAIGI nasikia hawana ofisi wanakutana bar ni kweli?

Huwa wanakutana kwenye Q-Bar hapo mjini. Jamaa hawa hawana ofc na fedha wanazochangishana zinaishia kukodi helkopita (chopa).
 
Njia zenu zote za kajambazi tunazijua

Sie wenyewe tunapenda njia zetu mzijue ili mjifunze kutowahadaa umma. Sisi ni watekelezaji ndo maana wananchi hutupigia kura nyingi za kishindo. Hapa Kagera chini ya REA tumepeleka UMEME hadi ngazi ya kitongoji sasa wewe Chedema utawaambia nini wahaya wakuelewe?

NGUVU YA CCM NDO UIMARA WA NCHI!
 
ndo natokea bk kila kijiwe walikuwa wanamjadili mdee japo kihaya hakipandi ila nilikuwa nasikia jina mdee mdee nikajua tayari dawa imewaingia
 
Safi sana Dada Mdee endelea kuchapa kazi.Katika mkutano wako wa Bukoba Mjini usisahau kuwaeleza wananchi jinsi serekali ya CCM ilivyokumbatia rushwa hadi wafadhali wamesusa kuchangia bajeti.Pia usisahau kuwaambia wananchi umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura tayari kwa uchaguzi wa wenyeviti wa serekali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

Mungu akujalie afya nje kamanda Halima Mdee.Wanawake wanaweza wakipewa fursa.
 
Ningetamani uwepo MDAHALO WA WENYEVITI WA WANAWAKE WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA' Hasahasa.. HALIMA MDEE vs SOPHIA SIMBA tuwapime na kutathmini uwezo na utayari wao wa kuwasaidia wakinamama wa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…