Kamanda Godbless Lema Kuongea na Wananchi wa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Godbless Lema Kuongea na Wananchi wa Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, May 24, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kamanda Godbless Lema ameitisha mkutano leo tarehe 25- 05-2011 utakaofanyika maeneo ya Arusha by night...
  ====
  je habari za Kiinterejensia zitaruhusu mkutano huo....
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  KAULI YA KATIBU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

  VITENDO VYA JESHI LA POLISI KWA RAIA

  NA

  KUKAMATWA KWA WABUNGE WA CHADEMA


  Katibu wa Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA nalaani vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha mauji ya raia na kukwepa kufanya uchunguzi kamili na huru kuhusu wahusika wa vifo hivyo na kuingilia haki za msingi za jamaa za marehemu na wananchi wa eneo husika kushiriki katika maziko ya wakazi wenzao na hatimaye kupatiwa haki nyingine zinazostahili kutokana na madhila yaliyotokea.

  Aidha nakemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwakamata wabunge wa CHADEMA, Tundu Lissu na Esther Matiko wakiwa katika kazi ya kuwatumikia wananchi na natoa mwito waachiwe mara moja; wao pamoja na wote waliokamatwa nao.

  Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba aliitwa na wahanga wa tukio husika pamoja na chama kwenda kusimamia haki za msingi za familia za marehemu baada ya polisi kukataa kufanya uchunguzi na pia kuminya mazingira ya haki kupatikana.

  Akiwa katika kutekeleza wajibu huo, jana (23 Mei 2011) alitaarifiwa na familia za marehemu na wananchi wengine kwamba polisi ina mpango wa kuchukua miili ya marehemu usiku na kuipeleka kusikojulikana na kuombwa kuungana nao katika kuwapa huduma za kisheria katika hatua zote. Aliambatana na familia za marehemu, wananchi na viongozi wa chama kufuatilia suala hilo ndipo alipokamatwa yeye na wengine na kuwekwa rumande kuanzia jana mpaka hivi sasa.

  Esther Matiku ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Mara anayetokea Tarime akiwa katika eneo lake la kazi leo (24/05/2011) alijulishwa na wananchi wa Nyamongo kwamba maiti ambazo walizichukua polisi kwa nguvu zingine wamezitelekeza njiani na kuitwa kwa ajili ya kushuhudia na kuchukua hatua zinazostahili kwa niaba ya wananchi. Akiwa katika kushughulikia suala hilo naye alikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande mpaka hivi sasa.


  Ifahamike kwamba matukio ya Nyamongo na Tarime kwa ujumla ni matokeo ya uongozi wa serikali kushindwa kusimamia vizuri sekta ya madini ikiwemo kuacha kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati wa miaka kadhaa sasa kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na mikataba vinavyofanywa na kampuni Barick Africa Gold na vile vinavyofanywa na polisi na vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wengine wa kiserikali wanaonufaika na hali hiyo yenye athari kwa wananchi katika maisha yao kutokana na mauji, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa mapato ya umma na watanzania wa eneo husika kutokunufaika kwa rasilimali.

  Naungana mkono na wananchi na wadau wote waliotoa mwito kufanyika kwa uchunguzi huru wa vifo (inquest) ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na kwa nafasi yangu nyingine kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitatoa tamko karibuni lenye kueleza kwa kina udhaifu wa serikali ulivyosababisha mauji hayo na kutaka wahusika akiwemo waziri kuwajibika.

  Aidha, kwa mara nyingine narudia tena kutoa pole kwa familia za marehemu ambao wanapitia kipindi kigumu wakati huu kutokana na matukio yanayoendelea; Mwenyezi Mungu awape uvumilivu wa kusimamia haki na ukweli kwa mustakabali wa taifa.

  Imetolewa tarehe 24 Mei 2011 na:

  John Mnyika (Mb)
  Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
  Na Wabunge wa CHADEMA
   
 3. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  aluta continua...viva cdm
   
 4. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nchi yangu naipenda ila viongozi magamba ndio wanayoipoteza ila kama sio kesho basi tuungane kwa pamoja kuleta uhuru wa kweli!
  Viva chadema
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kutojiamini polisi waliokuwa mapumziko imelazimika kukatisha ili kwenda kuongeza nguvu kukabiliana na nguvu ya CHADEMA kama kutatokea vurumai....
   
 6. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutujuza mkuu mkutano utafanyika saa ngapi?
   
 7. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutujuza mkuu mkutano utafanyika saa ngapi?
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Chadema huwa wanafanya mikutano bila ya vurugu ila polisi siku zote kwa kutii amri za CCM huanza vurugu wakitaka sababu yaa kuipaka chadema matope .This is wrong na mwisho wa siku itafika mahali polisi watashindwa kuwakabili wananchi maana wanachoka na tabia hizo.
   
 9. N

  Nanu JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Katika mkutano huo tafadhali kusiwepo na maneno ya uchochezi bali mbunge aongee na wapiga kura wake kuhusu "update" ya utatuzi wa kero zinazowakabili kutokana na jinsi alivyojinadi wakati wa kampeni. Muhimu ni kuhakikisha wananchi wa Arusha maendeleo yao yanaharakishwa na haki yao inalindwa ipasavyo! Kusiwepo na maneno yoyote ya uchochezi!!!
   
 10. O

  Omr JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tarime imeshakua dili kwa wanasiasa njaa, haya kafanyeni mikutano yenu isiokua na maana
   
 11. t

  tufikiri Senior Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unavyompa airtime huyu jamaa, angekuwa na uwezo km wa Zitto sijui ungefanyaje? maana hata km anaenda kuanzisha vurugu Vyuoni, Tarime nk lazima mumrushe humu JF. Au na wewe ni mwana ule MTANDAO?
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkutano utaanza saa ngapi Mkuu! na hapo Arusha by Night mbona hakuna uwanja?
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Nakuunga mkono kwa asilimia kadhaa. Namuomba Mbunge wetu mpendwa leo ongea kawaida na hata kama una maneno ya uchungu kutokana na kudhulumiwa basi ongea pale mwishoni kisha waombe wapiga kura wako watawanyike bila kufanya vurumai au kutukana polisi kwani najua wana chuki kubwa na polisi.

  Ila wawe mkao wa kujihami kwani polisi ni wachokozi na huo uchokozi kama ukitokea wasivumiliwe kabisa. Nasema hivi kwa sababu tangu yalipotokea mauaji tarehe 5/1/2011 hatujaweza kuongea kwa uhuru na Mbunge wetu kwani polisi wamekuwa wakileta za kuleta bila kujua kwamba wanachelewesha maendeleo ya jimbo letu.
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,122
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa njaa???? unamjua Lema au unamsikia kwenye redio anaweza kukulisha bure na ukutunzia mkeo maisha yako yote.
   
 15. O

  Omr JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahahaha, ndio maana unajipendekeza kwake,naona wewe ndio unae tunziwa mke... kijana umesahau sisi ni wamagamba?
   
 16. h

  hans79 JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  tuchangiapo jambo tufanye tafakar ili kuwapa uelewa walewasiojua,hatuna viongoz makin ambao wataondoa uonevu wa askar kwa raia wema
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Saa nane...
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Najua inakukera, Unatamani nimrushe Nape....Lol
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Photo-0032.jpg
  Photo-0038.jpg
   
 20. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Hili tamko lingepewa tread yake, hapa kama linachanganya habari na kushindikana kuichangia
   
Loading...