Kamanda alipowambia laleni na silaha hamkumuelewa?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Nimepata maono ya kiuhakika kabisa ni pale kamanda mmoja wa jeshi la polisi alipowaeleza wananchi kuwa inakuwaje mtu unalala nyumbani kwako unakosa hata panga.

Sasa nafahamu alishanusa harufu mbaya na kwamba sasa ni wakati wa ubaya ubaya kufa au kupona kila mtu ajilinde kivyake,akimaanisha tusitegemee polisi kivile.

Baada ya tafakari naona ile kauli ya mtu mzima dawa au mzee dawa, kamanda hakukosea kabisa, kwa cheo alicho nacho hawezi kutamka open kuwa kuna mbinu za watu kuvamiwa usiku au mchana ,mnatakiwa wananchi mkuu anapotoa kauli tata basi fikirieni mara mbili mbili,inakuwaje Mkuu anatoa kauli ya watu walale na silaha?

Wananchi ni bora ujumbe wa kamanda huyu ukawaingia Watanzania wote na kumuelewa kwa kina na anaposema nimebaini huwa anatoa ujumbe usiomoja kwa moja unaweza kusoma kwenye macho yake ,kuwa anaashiria jambo.

Sasa hata nikipata bomu nitalala nalo majambazi lazima mtu afe nao ,wanagonga na kuondoka na magunia ya karafuu saa nane za usiku askari gani hao ?Kama ningekuwa na guruneti mtu anaondoka nao kihamza tu.
 
Hii wamaasai na jamii yote ya wafugaji wanaizingatia sana, polisi hawawezi kuwepo kila mahali kwa wakati, kuna polisi jamii na kila mwanajamii ni victim au participant.
 
Ukiwa na mali ya maana na wakakuonea huruma, korolofomu itahusika, utaamka mchana mwenyewe kutokea sakafuni.
 
Silaha nyingine zaidi ya panga hii hapa," Chukua pilipili pondaponda Kisha koroga kwenye maji kiasi, iweke kwenye kopo au jagi Kisha ulipolala iweke karibu. Jambazi au kibaka akikuingilia ndani mmwagie usoni, hata kama alikuwa kabeba panga au bunduki ataitupa tuu kwa ule muwasho wa macho, Kisha unamkamata kirahisi na unajichagulia pa kupiga.
 
Mkuu, Heche (akiwa Mb) aliomba tupewe bunduki kwa ajili ya kujilinda sababu uwezo tunao na hatuhitaji Polisi, badala yake ikaanzishwa Kanda Maalumu ya Polisi.

Ukuryani tunatamani kutembea na silaha kama wafanyavyo Wamasai lakini tunakatazwa. Unakumbushwa kuwa na hata angalau panga nyumbani kwako kama silaha ya kujilinda, halafu unahoji?

Kweli wanaume wa Dar ni janga la Kitaifa
 
Mkuu, Heche (akiwa Mb) aliomba tupewe bunduki kwa ajili ya kujilinda sababu uwezo tunao na hatuhitaji Polisi, badala yake ikaanzishwa Kanda Maalumu ya Polisi.
Ukuryani tunatamani kutembea na silaha kama wafanyavyo Wamasai lakini tunakatazwa. Unakumbushwa kuwa na hata angalau panga nyumbani kwako kama silaha ya kujilinda, halafu unahoji?
Kweli wanaume wa Dar ni janga la Kitaifa
Aliyekufundisha kuwa panga ni silaha,inakubidi umlaani sana,au ni mfumo duni wa elimi uliopo unakupelekea kuamini kwamba panga ni silaha.
 
Back
Top Bottom