Kama ZITTO angekuwa M/kiti CHADEMA

Baada ya kuona mwelekeo wake ni kama haeleweki ndani ya chama,na jinsi anavyoongelewa na watu ndani na nje ya Jf.(1)Hivi angekuwa mwenyekiti Cdm ingekuwaje kwa sasa?(2)Anafanya hayo kama kidonda cha kukosa uenyekiti au ndiyo moyo wake ulivyo?WAKUU naombeni mnisaidie


Tumechoka kuongelea majungu. WanaJF hebu tujaribu kuzungumzia mambo ya msingi{critical issues} tuachane na mambo ya kinafiki na umbea wa kumuongelea mtu kila siku. Wengine bila kumtaja ZK hawawezi kulala usingizi.Yapo matatizo mengi ambayo yanaikabili nchi yetu, kwa nini tusitumie kuyajadili? kuliko kuzungumzia assumptions za kama kama kama Zitto ange.....Tafuta jukwaa lingine la kujadili majungu yako.
 
Alioleta hii post hapa na mnaochangia utumbo wa uchagga na uzitto wote ni maadui wa CDM. CDM kuweni makini na watu wa namna hii wanataka kuwaamisha watu kuwa CDM ina ugomvi mkubwa wa kikabila/kidini
 
Lakini dogo matata huyooo! akitoka huyo na chama kimekufa, watabakia wachaga pekeyao. Labda kama ile chacha
samahani naomba kuuliza Sugu,Silinde,Baregu,Msigwa,Slaa,MWAMPAMBA nk ni wachaga,mbona tunaongea v2 kama sio wasomi,kwa sababu viongozi wa juu wa ccm,ni waislamu je ccm ni ya waislam?FIKIRI
 
samahani naomba kuuliza Sugu,Silinde,Baregu,Msigwa,Slaa,MWAMPAMBA nk ni wachaga,mbona tunaongea v2 kama sio wasomi,kwa sababu viongozi wa juu wa ccm,ni waislamu je ccm ni ya waislam?FIKIRI

Kijallo,
Ongeza na jina la Zitto mwenyewe. Ni naibu Katibu Mkuu whilst siyo mchagga.
Ila hawezi kuwa chairman wa CDM kwa sababu his privailing behaviour leaves a lot to be answered.
Ninamshauri aende kwenye kazi anayoipenda kutoka moyoni mwake - UALIMU.
 
Lakini dogo matata huyooo! akitoka huyo na chama kimekufa, watabakia wachaga pekeyao. Labda kama ile chacha
Hv mbona nawe unaongeaga mambo murwa kbs lakini leo umesema pumba tupu? Ama siku nyingine kichwa kinahama. Ina maana Chadema kinamilikiwa oa Wacgagga
 
Baada ya kuona mwelekeo wake ni kama haeleweki ndani ya chama,na jinsi anavyoongelewa na watu ndani na nje ya Jf.(1)Hivi angekuwa mwenyekiti Cdm ingekuwaje kwa sasa?(2)Anafanya hayo kama kidonda cha kukosa uenyekiti au ndiyo moyo wake ulivyo?WAKUU naombeni mnisaidie

Zitto ameshajisahau na kudhani wananchi wataendelea kuwa wajinga miaka yote. Walimuunga mkono wakati wa kashfa ya Buzwagi kwa kuwa walijua anapambana kwa dhati lakini yeye akadhani anaungwa mkono kwa sababu ya ushawishi wake (wa maneno) kwa wananchi. Nashukuru Mungu CDM walimnyima nafasi hiyo.
 
Jamani jamani great thinkers this is low for you!!sioni sababu ya kudiscuss topic kama hii.haina maana kabisa zaidi ya kutaka tu kumsema Zitto kwa mabaya yote tuyapendayo?Zitto fisadi,Zitto msaliti,Zitto kanunuliwa,Zitto this Zitto that!!!!nimegundua kuwa hapa JF kuna watu wengi sana wasio na imani na Zitto ama basi tu wanamchukia for reasons that i wont know.lakini basi hii isiwe sababu ya kumuanzishia thread kila kukicha ili tu kumchafua!!!kweli wanasema baya moja hufunika mazuri yote kwani naamini Zitto amelifanyia taifa hili mazuri mengi tu zaidi ya mabaya lakini daima ni mabaya tu hukumbukwa!Kwani Zitto si binadamu???na biadamu hukosea.no one is perfect!sioni kama ni sahihi kuendelea kumhukumu Zitto kila kukicha especially hapa JF kwa sababu tu tunajisikia kufanya hivyo?hivi mnaomsema Zitto nyie ni wasafi katika nafasi zenu???ama Tanzania hii ni Zitto tu ndio mwenye kasoro na viongozi wengine wooote ni wasafi???tafakari na ujiulize kama unatenda haki ama unafurahisha tu nafsi kwa kumchafua mwenzio!!!
 
Habarini za asubuhi wanajamvi! Napenda nipate mawazo na maoni yenu kuhusu: Ingekuwa na hali gani CDM kama zitto angekuwa m/kiti wake toka 2009? naomba tujadili kwa busara,matusi yasipewe nafasi.
 
Habarini za asubuhi wanajamvi! Napenda nipate mawazo na maoni yenu kuhusu: Ingekuwa na hali gani CDM kama zitto angekuwa m/kiti wake toka 2009? naomba tujadili kwa busara,matusi yasipewe nafasi.

Mi na ona CDM ingekuwa kama TLP vile
 
Baadhi ya vjana wa CHADEMA ndio hupelekea Zitto kutumika na CCM, Chuki zao dhidi ya Zitto ndio chanzo cha yote, yaani, kuna watu kwa makusudi wanajaribu kutumia mitandao kumchafua zitto, sijui kwa faida ya nani?

CCM wanajifanya kama wanaunga mkono upande unaokosolewa, ili mradi sisi tunaokosoa tuwaone wale tunaowakosoa si wenzetu kisa tu wanaungwa mkono na ccm, na hili wamefanikiwa sana. Kwani sasa hivi watu washaanza kusema ukiona mtu anakubali na CCM basi mtu huyo dhaifu, huu ni ujinga ulikithiri unaongozwa na chuki binafsi na katu CHADEMA haitakuwa imara endapo tukiendeleza chuki hizi kwa wanaCHADEMA wenzetu.
 
ukweli ni kwamba mbowe kama mwenyekiti hana tatizo na mtu yeyote ubaya wa chadema ni watu wanaomzunguka mwenyekiti wao wengi wapo kwa ajili ya kumfitinisha kumpelekea majungu na hata kumshauri vibaya ili mradi mambo yao yaende sawa hawajali maslahi ya watanzania na imanibyao kwa chama kama mkombozi kutoka katika mikono ya ccm,wapo wengi humu kila mmoja anatumia utambulisho zaidi ya moja wanaweka hoja na kujijibu wenyewe wanafikiri siasa za mtandaoni zitawafikia watu wa vijijini wasio na ufahamu wa mitandao ya kijamii
 
Daahh huweziamini hawa ndio wanajiita wasomi wasikuizi wako kwamanufaa ya matumbo yao na familia zao basi!!!!!!!!! nasi wananchi wanyonge kama enzi za mwalimu inasikitisha sana TANZANIA YA LEO
 
Back
Top Bottom