Kama wewe sio Freemason basi hujui chochote kuhusu Mungu wala ulimwengu

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,111
27,096
Miaka kadhaa iliyopita nilitangaza hapa JF adhima yangu kufanya utafiti kuhusu uchawi na imani za siri.

Safari yangu katika tafiti kuhusu uchawi ilinifikisha kwa Mungu wa Kabili, mganga wa Jadi anaetajwa kama mganga mwenye nguvu kubwa za kiganga kuliko waganga wote wanaopatikana katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki kati na Kusini mwa Afrika.

Nianze kwa kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mungu wa Kabili kusema ukweli ameniongoza vizuri sana na kunipa mwanga halisi kuhusu masuala yote yanayo husiana na uganga, uchawi, ulozi, imani za jadi, upagani, imani za kale na imani za siri.

Nirudi kwenye mada yangu kuhusu imani za siri.Dokta Mungu wa Kabili alinieleza kwa kina kuhusu vikundi mbalimbali vya siri duniani ambavyo vinatajwa kuwa na mafundisho ya kiimani ya siri ambayo hujulikana tu kwa memba wao. Vikundi hivyo ni kama Freemasons na Rosecrucians kwa kutaja vichache. Nijikite kwa Freemasons. Mungu wa Kabili aliniambia mambo mengi sana ya kushangaza kuhusu Freemasons.

Kwa ufupi kabisa mambo nillyo jifunza kuhusu Freemasons ni kama ifuatavyo;

1.Freemasons wanafundishwa kuhusu Mungu aliye uumba ulimwengu na namna ya kuishi hapa duniani katika namna impendezayo yeye.Watu wa dini zote wangefundishwa kuhusu Mungu katika namna wanayo fundishwa Freemasons basi dunia ingekuwa sehemu nzuri sana ya kuishi.Mafundisho ya Freemasons kuhusu Mungu yanamchambua Mungu vizuri sana.

2.Freemasons wanafundishwa kuhusu ulimwengu, wanadamu na vitu vyote vilivyo ndani yake vinavyo onekana na visivyo onekana katika namna ambayo watu wa imani nyinginezo hawafundishwi.

3.Freemasons hawaamini kabisa katika black magic kwa hiyo ile dhana ya kwamba eti ukitaka utajiri nenda kajiunge Freemason umtoe kafara nduguyo ni dhana Potofu kutoka kwa watu wasio na ufahamu wowote kuhusu what freemasonry is.

4. Mfumo wa mafundisho ya freemasonry umenifanya nigundue kitu kimoja kwamba dini ya ukweli ni lazima iwe ya siri. Siri hiyo ndiyo inayo wapa waasisi wa dini au imani hiyo kuwa na nguvu dhidi ya watu wengine.

5.Kitu kingine nimegundua kwamba upako wa uhakika unapatikana kwa kujua siri zilizofichwa nyuma ya uwepo wa mambo yasiyo julikana.
 
Unajua mwenyewe nimefanya research sana kuhusu Freemansory nikaja kugundua kuwa wanachokijua wengi kuhusu hawa jamaa sio kweli na ni upotoshaji tu.

Freemasons sio watu kama wanavyofikiriwa ila ni moja kati ya secret societies ambazo zina maamuzi na impact kubwa sana katika matukio yanayoendelea duniani kila uchwao
 
i hope kama ningekuwa nimekuletea hile video yao nadhani ungeacha kuwapotosha watu humu
pili sitaki kuamini neno la mungu linatakiwa liwe siri juu ya wanadam aliyowaumba wew jamaa sio mtu zuri shame on you kwanz umekaa kiongo sanaa uandishi wa ovyo
Unajua kwenye bible imeandikwa " Kumcha Mungu ndio chanzo cha maarifa" yani knowledge .And the true knowledge is the one that help you to acquire, maintain and protect power.

Mind u wazungu sio wajinga kiasi hicho wakwambie kila kitu kuhusu Mungu aliye wapa maarifa yaliyo wafanya wawe na nguvu za kuutawala ulimwengu. Wakupe siri zao ili na wewe uwe kama wao.Unacho kijua kuhusu Mungu ni kile kilicho achiwa na kukusudiwa kijulikana kwa wale tu wanao stahili kupotoshwa.

But kiukweli kabisa u don't no nothing about the creator
 
Wewe unaweza kuwa Freemason.

Lakini kuna Freemason wa Freemason.

Mungu hayupo.

Kama unabisha thibitisha yupo.

" I know that which thou no not "
Unataka nikithibitishie ili na wewe upate maarifa kama niliyo pata Mimi? Unasema Mungu hayupo kwa sababu dhana yako kuhusu Mungu imekuwa limited kwenye mafundisho ya dini zile " kubwa" mbili ambao hawajui chochote kuhusu Mungu.

Study freemasonry and it will be scientifically and alchemically proved to you about the creator of the universe.

Otherwise ukitaka niprove kuhusu uchawi naweza hata sasa hivi kwa kukutumia wewe mwenyewe kama case study
 
Unajua kwenye bible imeandikwa " Kumcha Mungu ndio chanzo cha maarifa" yani knowledge .And the true knowledge is the one that help you yo acquire, maintain and protect power.Mind u wazungu sio wajinga kiasi hicho wakwambie kila kitu kuhusu Mungu aliye wapa maarifa yaliyo wafanya wawe na nguvu za kuutawala ulimwengu. Wakupe siri zao ili na wewe uwe kama wao.Unacho kijua kuhusu Mungu ni kile kilicho achiwa na kukusudiwa kijulikana kwa wale tu wanao stahili kupotoshwa.But kiukweli kabisa u don't no nothing about the creator
tatizo umeshindwa kutofautisha wao kumjua mungu na kujua dini na taratibu zake
 
Back
Top Bottom