Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 251
- 638
Leo ni kumbukizi ya siku ya wanawake duniani, tunafurahia sana uwepo wa siku hii kwa kuwa mambo mengi yameendelea na yanaendelea kufanyika mfano:- sheria gandamizi zilizokuwepo zamani dhidi ya mwanamke leo hii hazipo.
Zamani mwanamke akiolewa ndoa halali kabisa na ikatokea mumewe amefariki au wameachana badi mwanamke anaondoka mikono mitupu na hakuna atakapokimbilia kuweza kusikilizwa.
Lakini leo hii kwa maboresho ya kisheria yaliyofanyika mwaka 1983 yanamtambua mwanamke kama mchangiaji mkubwa katika upatikanaji wa mali yeye pamoja na mumewe kwenye ndoa. Mchango huo ni pamoja na kupika, kulea watoto, na kufanya kazi za nyumbani; hivyo ikitokea ndoa imevunjika au mumewe kufariki nae kupewa haki ya kumiliki mali walizochuma na mumewe.
Haya ni maboresho bora sana ya kisheria yanayolinda haki za mwanamke tofauti na zamani, lakini pia kwa sasa wanawake wengi wanafanya kazi, wanamiliki biashara, wawekezaji, na wanachangamkia na kupata fursa sawa kabisa na wanaume.
Ninachotaka kuwakumbusha wanawake ni kwamba; haijalishi umetoka familia gani, haijalishi umepitia mabaya kiasi gani, hukusoma au ulisoma. Kinachojalisha unataka kuwa na maisha ya aina gani hapo baadae.
Maisha unayotaka kuwa nayo yanaanza kutengenezwa leo hii. Unataka kupata mume bora, anza kwa kuwa bora wewe. Unataka kumiliki nyumba anza kutafuta na kuweka hela leo hii, unataka kuwa mfanyabishara mkubwa anza sasa.
Hakuna anaeweza kubadili yaliopita ila tunao uwezo wa kutengeneza yajayo yanayofurahisha. Yaliopita achana nayo yalishapita, hayawezi badilika acha yabaki kama funzo tu kwako. Cha msingi anza kupanga na kutekeleza mikakati itakayokufikisha kule unataka.
"LEO" ni zawadi kubwa sana uliyonayo, Mungu kakupa hio fursa itumie ipasavyo, hii ndio point ya msingi kwangu wanawake. Pambana sana ujinasue kutoka kwenye umasikini. Umasikini si jambo zuri, umasikini hupelekea wanawake kujiuza, umasikini hupelekea wanawake kuwa wanyonge na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
PAMBANA MWANAMKE
Mwanamke ni kujifunza, mwanamke soma vitabu, kuza ubongo, mwanamke ni kuwa na jicho la fursa.
Leo ni siku ya Wanawake nami nichukue fursa kuwatakia wanawake wote wapambanaji.
HAPPY WOMEN'S DAY
NOTE: Imeandikwa na MALAIKA wa MALAIKA: na kuhaririwa na MTUACHE LTD