Kama wewe ni mwalimu soma hapa ni muhimu.

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
0
Ni miaka mingi kada ya uwalimu imekuwa ikidharauliwa kwa muda mrefu nchini kwetu. Hii imepelekea mwalimu kudharaulika sana ndani ya jamii japo amekuwa mtu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu. Mshahara wa mwalimu umekuwa haukizi mahitaji ya mwalimu na hivyo kuwa mtu wa kukata tamaa sana kimaisha. Kutokana na mwalimu kukata tamaa kutokana na mazingiza ya kazi kuwa magumu imepelekea elimu ya Taifa kushuka kila siku huku viongozi wa taifa letu wakipigia chapuo idadi ya madarasa, na kuacha kuzungumzia ubora wa elimu nchini huku wakipeleka watoto wao nje ya nchi na kuwaacha watoto wa wakulima na wafugaji wa nchi wakiikosa haki yao ya kupata elimu bora. Kama waalimu wa nchi hii tunalo jukumu la kuitetea elimu ya taifa letu wenyewe na sio kutegemea chama cha waalimu CWT ambacho kimeonyesha dhahiri kuwa hakina nia ya dhati ya kurejesha heshima ya walimu nchini. Waalimu ili kufanikiwa katika hili tunatakiwa kupambana na maadui watatu wakubwa ambao ni:-1.WOGA 2.CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) 3.SERIKALI. Tutafanikiwa endapo tutashirikiana sote kwa pamoja na kw3a umoja. Cha kufanya tunatakiwa kuwaunganisha waalimu wote nchini tuwe na kauli moja pasipo woga wala hofu.Ninahitaji kupata namba za simu kutoka waalimu pande zote za Tanzania ili tuunganishe nguvu ya pamoja kupigania maslahi na hadhi ya mwalimu nchini.Tukiungana kwa pamoja tunaweza. Nipatie namba yako kwenye inbox yangu ili tuwasiliane na tuunganishe nguvu. KWA PAMOJA BILA WOGA TUNAWEZA.
 

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
2,000
Wee mutu ni njaa tu hizo zinakusumbua, haya ndo mambo ya watu wenye mawazo finyu ambao wasipofanikiwa wanafikiria ni mtu au kundi la watu ndo wamewafanya wasifanikiwe. Adui mkubwa na no 1 kwenye mafanikio yako ni wewe mwenyewe na siyo CWT wala serikali wala mwl mkuu wala nani, ni woga wako mwenyewe wa kushindwa kujaribu kitu tofauti. Be creative and think critically
siku zote naamini katika kufanya kile ambacho kinaweza kukuletea maendeleo na siyo kugombana na mwajili. nimwahi kuajiriwa mara 5 na nimeacha kazi mara 4, kwa sasa mi ni mwl lakini nimefanikiwa sana na naifurahia taaluma hii mupya ninayofanya. so please kama unaona unaonewa usi sploil wenzio we acha kazi tafuta ile ambayo unaona ina maslahi zaidi, waajiri mbona wengi tu tena wenye mishahara mikubwa
embu tuache waalimu tupumuweeeeeeeeeeee
 

mwalimumwema

Member
Dec 7, 2012
16
0
Sio maadui watatu tu Mwalimu: # 4 ni JAMII YA WATANZANIA.

Watanzania hasa wa kipato cha chini ambao ndio waathirika wakuu wa elimu mbovu wamekuwa wakwanza kuwadharau walimu na taaluma nzima ya ualimu. Ni ajabu unamshauri mwalimu atafute namna ya kujikimu na ualimu uwe ziada then unategemea mwanao apate elimu bora toka kwa mwalimu huyo huyo. Nashauri watanzania tubadilike, matatizo ya walimu yanatuhusu sana kwa namna moja ama nyingine.

Kuwashauri walimu waidharau na kuitelekeza fani ya ualimu ni sawa na kumshauri baba mwenye nyumba aitelekeze familia yake ambayo ameitengeneza kwa gharama kubwa kuanzia kutafuta mchumba, kuoa na kuzaa watoto. Ni ushauri mzuri kuwekeza kwenye shughuli nyingine za kujipatia kipato kama uchumi binafsi wa mwalimu, na wengi wamekuwa wakifanya hivyo na imesaidia sana LAKINI (behind the scene) tunashuhudia matokeo mabaya ya wanafunzi darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita. Hayo yote pamoja na mambo mengineni matokeo ya poor concentration among teachers in and out of the four walls of the classroom.

Sasa hivi unaweza kuona walimu wametulia tu wameshagundua jitihada zao na matatizo yao hakuna anayeyaona si serikali wala jamii ya watanzania, kwa mtazamo wangu naona kuna mgomo baridi katika fani ya ualimu.
 

My Mud

Senior Member
Oct 5, 2012
109
195
Sio maadui watatu tu
Mwalimu: # 4 ni JAMII YA WATANZANIA.

Watanzania hasa wa kipato cha chini ambao ndio waathirika wakuu wa elimu
mbovu wamekuwa wakwanza kuwadharau walimu na taaluma nzima ya ualimu.
Ni ajabu unamshauri mwalimu atafute namna ya kujikimu na ualimu uwe
ziada then unategemea mwanao apate elimu bora toka kwa mwalimu huyo
huyo. Nashauri watanzania tubadilike, matatizo ya walimu yanatuhusu sana
kwa namna moja ama nyingine.

Kuwashauri walimu waidharau na kuitelekeza fani ya ualimu ni sawa na
kumshauri baba mwenye nyumba aitelekeze familia yake ambayo
ameitengeneza kwa gharama kubwa kuanzia kutafuta mchumba, kuoa na kuzaa
watoto. Ni ushauri mzuri kuwekeza kwenye shughuli nyingine za kujipatia
kipato kama uchumi binafsi wa mwalimu, na wengi wamekuwa wakifanya hivyo
na imesaidia sana LAKINI (behind the scene) tunashuhudia matokeo
mabaya ya wanafunzi darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.
Hayo yote pamoja na mambo mengineni matokeo ya poor concentration among
teachers in and out of the four walls of the classroom.

Sasa hivi unaweza kuona walimu wametulia tu wameshagundua jitihada zao
na matatizo yao hakuna anayeyaona si serikali wala jamii ya watanzania,
kwa mtazamo wangu naona kuna mgomo baridi katika fani ya ualimu.

kabisa kuna silence mgomo hata baba riz1 analitambua hilo.
 

Gilly

Member
Aug 6, 2009
87
95
My Mud
kabisa kuna silence mgomo hata baba riz1 analitambua hilo

Mkuu, uzuri wa walimu ni waelewa wazuri tu. Sasa hivi hawajali. Si juzi tu wameikimbia shule huko Rufiji na kuiacha imefungwa na kumfanya DC ahahe kuitisha Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa lengo la kufanya suluhisho na wazazi? Suluhisho gani ikiwa walimu walidhalilishwa na wanafunzi wao? Unahitaji kuwa mwendawazimu kumsamehe mwanafunzi wako aliyekubaka na kisha ukamfundisha vizuri. Na mwalimu mwendawazimu haruhusiwi kufundisha kwa sababu ni hatari kwa usalama wa mwanafunzi. Upo Mkuu? Patamu hapo?
 

gbrother

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
408
195
Wee mutu ni njaa tu hizo zinakusumbua, haya ndo mambo ya watu wenye mawazo finyu ambao wasipofanikiwa wanafikiria ni mtu au kundi la watu ndo wamewafanya wasifanikiwe. Adui mkubwa na no 1 kwenye mafanikio yako ni wewe mwenyewe na siyo CWT wala serikali wala mwl mkuu wala nani, ni woga wako mwenyewe wa kushindwa kujaribu kitu tofauti. Be creative and think critically
siku zote naamini katika kufanya kile ambacho kinaweza kukuletea maendeleo na siyo kugombana na mwajili. nimwahi kuajiriwa mara 5 na nimeacha kazi mara 4, kwa sasa mi ni mwl lakini nimefanikiwa sana na naifurahia taaluma hii mupya ninayofanya. so please kama unaona unaonewa usi sploil wenzio we acha kazi tafuta ile ambayo unaona ina maslahi zaidi, waajiri mbona wengi tu tena wenye mishahara mikubwa
embu tuache waalimu tupumuweeeeeeeeeeee

nadhani una fikra finyu na kichwa kilichojaa ubinafsi ambao ni hatari kubwa sana, na inawezekana kabisa unauhadaa umma wa wanaj-f kwa eti nawe ulikuwa mwl, maana kama ndivyo sidhani kama ungekuwa na nguvu na povu jingi la kuwatetea hawa cwt,
kuwa great thinker kaka/dada
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom