Samboko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2011
- 5,417
- 8,047
Ni stori ya kweli. Mkeo ni mjamzito wa miezi nane amekuaga anaenda kwa nduguzake, wewe ukabaki home umepumzika baadae ukiwa unasikiliza redio unamsikia mkeo live kwenye redio anabishana na wanaume wawili kua mimba aliyonayo si ya kwao kama alivyokua amewaambie hapo awali bali ni yako na wakabishana sana kila mwanaume akitoa ushaid wake na mmoja wao alikua akisoma nae chuo, na ukweli ni kua wote alitembeanao bila kuvaa kinga na mkeo anakiri wote alifanyanao mapenzi maana kila mmoja alidai mimba ni yake Je? Ungekua ni wewe ndio mme wake na huyo mwanamke ungechukua uamuzi gani? Ukizingatia wewe ulimuoa baada ya kukuambia ana mimba yako. Chanzo cha stori ni Clouds fm kwenye kipindi cha njia panda, kwa waliofuatilia tupo pamoja.