Kama walishindwa ni af | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama walishindwa ni af

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ibrah, Sep 7, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  KAtika redio za kimataifa zinazopendwa nchini ni Idhaa ya Kiswahili ya BBC LOndon. Kwa kweli tangu aondoke tido mhando kama Mkuu wa Idhaa hiyo, viwango vyao vimeporomoka sana na ingawa husikiliza BBC Idhaa ya Kiswahili kila siku bado sivutiwi na utendaji wao wa kazi hasa Watangazaji wao wa siku hizi huko London n Nariobi.

  Kuna baadhi ya watangazaji wa Idhaa hiyo ambao lugha yao ya kwanza si Kiswahili na hutumia Kiswahili kibovu (simaanishi lafudhi bali broken swahili). Kama ingekuwa ni Wawakilishi wao wa nchi za Uganda, Somalia au Kongo nisingeshangaa lakini ni baadhi yao ni Waajiriwa kabisa hapo HQ London!

  Kero nyingne ni tabia iliyozuka siku hiozi ya Idhaa hii kuturushia matangazo yalliyorekodiwa siku moja au mbili. Mfano ni kipindi cha michezo siku moja kabla ya mechi ya Man Utd na Arsenal ambacho walikirusha tena siku ya jumatatu asubuhi! Kwa kwel;i walini-bore sana. Yaani walishindwa kuandaa kipindi! Ni afadhali wasingekuwa na kipindi cha mihezo siku hiyo kuliko kutuambia @kesho kutakuwa na mechi kali baina ya MAn U na Arsenal wakati mechi ilichezwa jana!
   
Loading...