Kama vipi tuachane!

Kama vipi tuachane!

kama alikua tayari kuachana nae toka zamani,matusi ya nini?

kaka yako aendelee na maisha..Mungu atampa mwenza mwema

hapo pa matusi ndo tunashindwa kumuelewa aliposema tuachane alikuwa ana maana gani?hatumuelewi!
 
Wengine wanalilia wengine wanachezea vibiriti. Ngoja awaachie wanaweza.

Sasa cjui hao aliosema ma handsome wengi wenye pesa wanamtaka kila siku cjui sasa wako wapi muda wote huo ana haha peke yake?!
 
Du!!Pole sana ndugu,ndo changamoto za mapenzi huna budi kukabiliana nazo!!!!!Sidhani kama atamrudia tena,mana toka kitambo marafiki na ndugu walikuwa wanamshauri amwache kwa vituko vyake,lakini hakuwa tayari kumwacha,sasa kasalimu amri mwenyewe na kumwacha bila kushawishiwa na mtu yamemfika shingoni na harusi ilikaribia lakini ndo kamwacha!
missa mpe pole kaka mwambie abadili no na akate mawasiliano aafu kuna fursa huku Jf
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wana JF.

kuna kaka yangu katika ukoo,alikuwa na mchumba wamedumu kwa miaka 3,mwaka huu mwezi wa 6 tulitarajia kula mpunga mana maandalizi ya ndoa yao yalikwisha anza, na huko kijijini kwetu walishaanza kuchangishana.

Cha kusikitisha kila wanapokuwa na mgogoro mdada alikuwa anatoa kauli" kama vipi tuachane, mana mi ni mzuri na wanaume wengi ma handsome wenye pesa zao wananitaka''

Basi hiyo kauli ikawa inatumika kama silaha kila wanapopata mgogoro na kaka yangu,iwe makosa ni ya kaka au ya mdada basi kaka yangu akawa ni mtu wa kujishusha na kuomba yaishe hata kama makosa ni ya mdada!na hii ilitokana na ukweli kwamba kaka yetu alimpenda sana mpenzi wake na alikuwa tayari kunusuru penzi lake kwa namna yoyote ile mradi tu kuondoa malumbano!

Mbali na hayo yote kaka ametumia gharama nyingi sana kumfungulia miradi mbalimbali mpenziwe zikiwemo saloon za kike lakini mdada ndo kwanza anajinadi kwamba yule mwanaume hawezi kumuacha hata iweje mana kwake amekufa ameoza!

Sasa mwezi uliopita wakagombana kisa mdada kapiga cm kaka akiwa kazini halafu kaka hakupokea cm,baadae kaka akampigia cm kumweleza kwamba hakupokea cm muda ule alikuwa na kazi,basi kama kawaida ya mdada akaanzisha ugomvi na kusema kama vipi tuachane,kaka akaomba radhi ikashindikana,Basi kaka akakubali waachane kweli!


Basi siku kadhaa zikapita huku wakiwa wamechuniana,baadae mdada akarudi akasema anaomba msamaha hatorudia tena,kaka akasema amemsamehe ila hataki mapenzi naye tena na uchumba uishie hapo mana kadri wanavyokaribia ndoa ndo anazidisha vituko!

Mdada kusikia akasema kama hataki waendelee atamwonyesha kazi,basi baada ya cku mbili kaka akakamatwa,kuuliza sababu wanasema katishia kumuua mpenzi wake,jamani wanawake wengine,baadae mahakamani ikaonesha kazusha na hana ushahidi isitoshe yeye ndo alikuwa anatuma sms za matusi ya nguoni kwa kaka na ushahidi ulikuwepo,kesi imefutwa!!!!

sasa kesi imefutwa anaendelea kumtumia sms za matusi kaka hadi leo hii ninapoandika,sasa najiuliza jamani kama bado unampenda mpenzi wako kwa nini ukimbilie kusema tuachane kila mnapogombana?sasa uchumba umekwisha na mipango ya ndoa imesitishwa japo alikwisha lipiwa mahari zote! Hellow ladies and Gentlemen learn how to control your mouth!

Your brother is the true son of his father. Amefanya uamuzi mzuri sana wa kumpiga chini huyo ONYIBERIBE
 
Sasa cjui hao aliosema ma handsome wengi wenye pesa wanamtaka kila siku cjui sasa wako wapi muda wote huo ana haha peke yake?!
Hilo nalo neno. Labda alikuwa anajishaua na visharobaro vya mjini walokuwa wanamnunulia icecream maana vizuri wanapenda ila hawawezi kuoa.
 
akaolewe sasa na hao mahandsome wake, tena huyo akili zake zimejaa maji ya barafu umeme ukikatika hayauziki. maana yake kuwa akili zake ni hasara.

kweli kabisa,ujanja mwingi mbele giza!
 
Hilo nalo neno. Labda alikuwa anajishaua na visharobaro vya mjini walokuwa wanamnunulia icecream maana vizuri wanapenda ila hawawezi kuoa.

kweli bila shaka kuna visharobaro vilikuwa vinamzuzua na kumpa masifa kuwa ye ni mzuri bwana hawezi kosa mwanaume,alisahau kuwa mwanaume anaweza mpata lakini si mwenye mapenzi ya dhati ni mpitaji tu!
 
wanawake bwana! yaani yeye kuambiwa mzuri na.wanaomtamani akadhani hao ndo waoaji maskini mwee! kumbe si waoaji hao..alibeep sasa kapigiwa acha iwe fundisho ajifunze..wanawake mkipendwa pendekeni majivuno acheni..tena mwambie kaka abadili line na hayo mamiradi asiyaguse amwachie.ikiwezekana pete yake ya uchumba airudishe..
 
Your brother is the true son of his father. Amefanya uamuzi mzuri sana wa kumpiga chini huyo ONYIBERIBE

kweli kabisa hata sisi tunadhani kama angemuoa tu ingekula kwake mana angekuwa matesoni maisha yake yote!!mana mdada anapenda sana ugomvi hata kwa vijambo vidogo tu visivyo na maana na kusuluhishwa ndo hataki kabisa na anapenda aombwe msamaha hata kama ye ndo mwenye makosa,na msamaha wake ilikuwa inachukua muda mrefu kumsamehe mwenzake!
 
wanawake bwana! yaani yeye kuambiwa mzuri na.wanaomtamani akadhani hao ndo waoaji maskini mwee! kumbe si waoaji hao..alibeep sasa kapigiwa acha iwe fundisho ajifunze..wanawake mkipendwa pendekeni majivuno acheni..tena mwambie kaka abadili line na hayo mamiradi asiyaguse amwachie.ikiwezekana pete yake ya uchumba airudishe..

umejuaje?miradi kamwachia na mdada anajisifu kwa marafiki zake kuwa amepata miradi kibao kupitia mgongo wake!sasa aliposema arudishe pete ya uchumba kakataa anasema ataipeleka kwa sonara,basi kaka kamwachia akae nayo atajua mwenyewe kama anapeleka kwa sonara au wapi!yaani mdada ni mtemi huyo balaa!kaka namba ya cm hajabadili ila ame mblacklist na akituma sms zake za matusi hamjibu!
 
Kama anasema yeye mzuri, mbona mimi simfahamu?
Na nikimuona namkata kidizain flani halafu nachikichia zangu!
 
missa mpe pole kaka mwambie abadili no na akate mawasiliano aafu kuna fursa huku Jf

du!itabidi nimwambie aje ajaribu fursa huku jf mana ana malengo ya kuoa jamani!mwanamke atakayempata atafaidi sana!!!
 
Kama anasema yeye mzuri, mbona mimi simfahamu?
Na nikimuona namkata kidizain flani halafu nachikichia zangu!

umeona hee,angekuwa mzuri tungemuona kwenye noti za pesa!!!lakini hata kwenye sarafu hayupo!sasa huyo ndo mzuri kweli?
 
Missa shukrani sana kwa liwaya lako nzuri maana halina tofauti sana na mkasa ulionitokea, kweli wanawake hawajielewi wala hawajui thamani ya kupendwa na daima watalendelea kumegwa nakuachwa bila ndoa kwa tamaa zao za ajabu kukupatikia upya wa mapenzi na tamaa za mda mfupi kwa wanaume wasio na uhakika nao!!
 
Ukipanda magotini nakuacha,
ukipanda kifuani nakuacha,
ukipanda mabegani hamna shida nakuacha,

ukipanda kichwani hapana sikuachi, lazima nikushushe chini kabisa.

Hii ni sheria ya wanaume, haruhusiwi mtu yeyote yule kupanda kichwani.

Huyo dada amepanic.

Kula "like" la nguvu, thats how gentlemen behave
 
sio kabila moja,mkaka ana 32yrs na mdada 28yrs.

huyo mdada ni tahira sana,,28 bado unaleta mbwembwe!!!!me nilijua bado mbichi kma 23 hivi,,,naona dalili ya mtu kunywa sumu hapo
 
Back
Top Bottom