Kama vipi tuachane!

Kama vipi tuachane!

Huyo bora kaachwa mapema maana ata angeolewa ingekuwa mtihani mwanzo mwisho, Amestahili kuachwa mpe pongezi kaka yetu na mwambie atampata mdada mwenye mwema na atakaemuheshimu akasahau vituko vya huyo mwanakwenda
 
the same is happening to me. I posted it here this week, though mine is complicated but nampongeza kaka yako na asirudi nyuma.

Du!!Pole sana ndugu,ndo changamoto za mapenzi huna budi kukabiliana nazo!!!!!Sidhani kama atamrudia tena,mana toka kitambo marafiki na ndugu walikuwa wanamshauri amwache kwa vituko vyake,lakini hakuwa tayari kumwacha,sasa kasalimu amri mwenyewe na kumwacha bila kushawishiwa na mtu yamemfika shingoni na harusi ilikaribia lakini ndo kamwacha!
 
Huyo bora kaachwa mapema maana ata angeolewa ingekuwa mtihani mwanzo mwisho, Amestahili kuachwa mpe pongezi kaka yetu na mwambie atampata mdada mwenye mwema na atakaemuheshimu akasahau vituko vya huyo mwanakwenda

kweli kabisa angetutesa sana,maana kuachwa tu kaanza kukandia hadi kijijini kwetu eti kubaya nyumba za miti!!!!!!jamani!
 
Huyo dada hakujua ule msemo....."kila kizuri kina mwenyewe"...? Alidhani yeye ni mzuri bila kuwepo mtu anayemfanya kuwa mzuri ambaye alikuwa huyo kaka?? Ha ha ha ha haaa! aende kijijini aone jinsi mabinti warembo walivyokosa wanaume kisa hawana vianzio vya kuwafanya waonekane wazuri! Akina dada kazi kwenu, mpo wengi kweli!
 
wanasaikolojia wanasema neno la kama vipi tuachane ni neno baya sana la kumtishia mpenzi wako wa aina yeyote. Si zuri kulitamka hata kama linapitapita kichwani kwani majuto yake huwa ni mjukuu.
 
yaani katika mahusiano ukiweza kuwa makini na kauli zako tu, mtaishi vema.
 
Kamwaga mboga, mwenzake kamwaga ugali na kuanua jamvi
 
Tatizo moja ambalo lipo kwa wasichana ni kubweteka hapa na maanisha kwamba anapo sikia anaambiwa na wana ume kuwa yeye ni mzuri basi anajiona kuwa yeye ndo yeye na hakuna mwingine haangalii kuwa yule anayemwambia anamalengo gani na ni nani Dada alibweteka hakujua kuwa waliokuwa wanamsifia na kumtongoza walikuwa wanamtamani na hakulijua hilo sasa matokeo yake ndo hayo...Bro wako abadili mawasiliano mana huyo hakuwa na upendo wa dhati alikuwa mguu mmoja ndani mwingine nje sasa katoa wandani nje kakutana na simba karudi ndani tena anakutana na chui duhh....
 
wanasaikolojia wanasema neno la kama vipi tuachane ni neno baya sana la kumtishia mpenzi wako wa aina yeyote. Si zuri kulitamka hata kama linapitapita kichwani kwani majuto yake huwa ni mjukuu.

ye alidhani anamrusha roho kaka yetu kisa anampenda na kila siku ye ndo anajishusha!
 
Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu. (Yakobo 4:6 )
God resists the proud, but gives grace to the humble (
James 4:6&#8211😉
 
Tatizo moja ambalo lipo kwa wasichana ni kubweteka hapa na maanisha kwamba anapo sikia anaambiwa na wana ume kuwa yeye ni mzuri basi anajiona kuwa yeye ndo yeye na hakuna mwingine haangalii kuwa yule anayemwambia anamalengo gani na ni nani Dada alibweteka hakujua kuwa waliokuwa wanamsifia na kumtongoza walikuwa wanamtamani na hakulijua hilo sasa matokeo yake ndo hayo...Bro wako abadili mawasiliano mana huyo hakuwa na upendo wa dhati alikuwa mguu mmoja ndani mwingine nje sasa katoa wandani nje kakutana na simba karudi ndani tena anakutana na chui duhh....

hata sisi tumeshauri abadili line,mana naskia kaanza kukodi bajaji anakwenda kazini kwa kaka anakaa chini ya ghorofa na kuchunguza kila anachofanya kaka anapokuwa kazini na kaka anapoondoka na yeye huondoka na bajaji yake aliyokodi!kweli kachanganyikiwa sana,haamini kilichotokea mana harusi imevurugika kiutani!
 
Shosti alijua ameshinda bingo! Hii dawa nzuri sana.
 
kama alikua tayari kuachana nae toka zamani,matusi ya nini?

kaka yako aendelee na maisha..Mungu atampa mwenza mwema
 
hata mimi sipendi utani "tuachane" itakula kwako mazima.....
 
akaolewe sasa na hao mahandsome wake, tena huyo akili zake zimejaa maji ya barafu umeme ukikatika hayauziki. maana yake kuwa akili zake ni hasara.
 
Back
Top Bottom