Elections 2010 Kama ungekuwa mgombea urais 2010-2015 sera yako ya elimu ingekuwa nini?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kwa kutambua umhimu wa elimu katika maendeleo ya binadamu, na kwa kutambua umhimu wa makuzi na ujenzi wa tabia ya mtu katika umri mdogo. Ningepata nafasi ya kuwa rais wa Tanzania kwa miaka 5 ijayo ningependa kufanya yafuatayo kwenye mfumo wa elimu wa nchi hii.
  • Ningehakikisha nabadirisha mfumo wa elimu kutoka katika mtazamo wa kupambana na ukoloni wa kisiasa na kuwa wa kupambana na adui na mkoloni mpya ambaye ni umasiki, ningefuta vitabu vyote vya fasihi vya akina Ngugi, Chinua Achebe, n.k, ambavyo vilikuwa vinasomwa enzi zile na badala yake kuweka vitabu vyenye mwelekeo na mtazamo wa akina Napoleon Hill, Jack Canfield, na vingine vya aina hiyo
  • Kuhakikisha kuwa mfumo wa elimu unamwandaa mwanafunzi kupambana na maisha na kuwahamsisha kufikiri zaidi katika kutatua changamoto za jamii zao kwa kuwa kitu pekee ambacho hakuna mtu mwingine anaweza kuwanyang'anya ni akili zao na namna wanavyozitumia.
  • Mfumo huo ungelihakikisha kuwa kila mwanafunzi anayesoma sayansi anasoma ili alete nafuu ya namna watu wake wanavyoishi, kila mwanafunzi anayesoma sanaa anafanya hivyo ili alete tofauti katika jamii yake. Ningehakikisha kuwa mfumo wetu wa elimu unaacha kuandaa vibarua, wajakazi na wategemezi bali unaandaa watu wa kufikiri zaidi (thinkers) ili kusudi wakipata kazi wasiwe wategemezi wa kusubiri waambiwe nini cha kufanya bali watu wanaotafuta nini kifanyike ili kazi waliyopewa inafanyika kwa ustadi na ufasaha zaidi.
  • Ningeweka mfumo wa elimu unaowahamasisha watoto kuchukia wale wote wanaopata mafanikio kwa hila na dhuluma, na kuwapa hamasa ya kutafuta watu waliofanikiwa kwa kusaidia jamii zao katika fani wanayotaka kufanya pindi wakimaliza masomo ili wawe mifano yao (their idols)
  • Ningehakikisha kuwa wadau wote wanashirikishwa katika kutafuta namna bora zaidi ya kuyafikia malengo yangu ili kwamba Tanzania ya 2025 iwe Tanzania ya mfano, iwe Tanzania isiyotegemea mikopo ya wahisani ili kulipa mishahara ya watumishi wake, ili Tanzania hiyo iwe kisiwa cha amani ambapo kila mwananchi ana fursa sawa katika kujipatia riziki yake. Ili nchi yangu isiagize tena bidhaa feki kwa sababu wananchi wake hawatawakubali wale wote wanaotafuta riziki kwa hila na dhuluma kwa kuwauzia wenzao bidhaa zisizo na ubora sitahiki, wasichanganye tena mafuta ya taa na dizeli ili kuwaibia wenzao na kuwaharibia wenzao.
Naombo kuwakilisha.... ilani yako ni ipi?
 
Back
Top Bottom