Kama unaumia ukiombwa pesa na Mpenzi wako akiwa na shida, Je, utafurahia akisaidiwa na 'baharia' mwingine?

Wanaume mmeumbiwa majukumu.acheni kuyakwepa
Hela ya vocha tu mwenzio kachacha unakimbia kulea familia akibeba mimba utaweza? Na huko jukumu pia wengi mnakimbia kwa kukataa mimba.
Utamnyima hela lakini jua ukimuoa utamtunza.ukishindwa watamchukua wenzio wamtunze.
Hata katiba ya nchi kuhusu ndoa unasema mojawapo ya haki ya mke katika ndoa ni kutunzwa na mme wake.

Wanawake angalieni wanaume mnaotoka nao.mwanaume akiwa mbinafsi kwa kidogo usitarajie akawa mkarimu kwa kikubwa.

Epuka mwanaume mkimbiaji majukumu,atakucost!
 
Hivi kwenye ndoa kuna uzoefu?

Mimi najua kila mtu anabeba zigo lake mwenyewe

Wengine walibeba sura halafu zinawasumbua

Wengine walibeba wowo au makalio yanawatokea puani

Wengine walioa vimbaumbau sura ngumu miguu kama chaga wanaishi kwa furaha na amani tele na ndoa zipo imara

Wengine walio miguu ya bia wana raha na amani

Tatizo ndoa kila mtu anabeba tatizo lake hakuna uzoefu
 
Wanaume mmeumbiwa majukumu.acheni kuyakwepa
Hela ya vocha tu mwenzio kachacha unakimbia kulea familia akibeba mimba utaweza? Na huko jukumu pia wengi mnakimbia kwa kukataa mimba.
Utamnyima hela lakini jua ukimuoa utamtunza.ukishindwa watamchukua wenzio wamtunze.
Hata katiba ya nchi kuhusu ndoa unasema mojawapo ya haki ya mke katika ndoa ni kutunzwa na mme wake.

Wanawake angalieni wanaume mnaotoka nao.mwanaume akiwa mbinafsi kwa kidogo usitarajie akawa mkarimu kwa kikubwa.

Epuka mwanaume mkimbiaji majukumu,atakucost!
Hakuna chakukimbia wala kukwepa, wanawake wanachukulia mahusiano kama ajira hivyo mwanaume anatakiwa kulipa mshahara ili apate huduma...
Ishakua biashara isiyo rasmi..

Mi naweza nikakupenda namna unavyojipenda kwa mitindo ya nywele full kubadili viwalo, mcheshi na wakati nakufuata unanihakikishia huna mtu..

Inakuaje ukiwa na mimi hivyo vitu vinakua ni jukumu langu kiasi nikishindwa mapenzi Yanakua basi?

All in all hakuna mwanaume asiyependa kumuhudumia mwenza wake, tatizo ni namana gani anatakiwa kumuhudumia, binafsi sikai au kuishi na wewe huduma zangu ni kwa mapenzi yangu... na wala si wajibu. Ukitaka niwajibike njoo kwangu tuyajue maisha yalivyo kwa pamoja siku sina hela nitakopa unga tupike tule.
 
Shida ipi ya kuomba Kwa mwanaume mwingine? Vocha?Pesa ya kula?Ya saloon?

Maisha ya sasa kila mwanamke anatakiwa ajitahidi amudu mahitaji yake ya msingi
Mume au Boyfriend ajazie panapo pungua..

Kama mwanamke ana mahitaji ambayo yeye mwenyewe hajitoshi na mumewe au bf nae hatoshi.. anahitaji mtu wa tatu kumsaidia..

Na amtunuku huyo wa tatu mapenzi?
Na WA tatu akishindwa? Anatafuta wa wa nne?.. tofauti yake na kahaba iko wapi?
 
Back
Top Bottom