Kama unataka kuolewa, basi fanya hivi…………… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama unataka kuolewa, basi fanya hivi……………

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 19, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280


  Kwanza anza kujipenda wewe mwenyewe. Kama wewe mwenyewe hujipendi, usitegemee kuwa wengine watakupenda. Ukimudu kujipenda, utamudu kumpenda kila mtu na suala la kuolewa na nani, linakuwa halina maana.

  Pili elewa majukumu yako. Ni vizuri kama mwanamke ulielelewa vyema kujua majukumu yako. Kwa kweli awe ni mwanamke au mwanaume, anatakiwa kujua majukumu yake mapema kabla hata ya ndoa ili kupunguza migongano baadaye.

  Tatu,
  wanaume wanapenda wanawake imara. Hawapendi mwanamke ambaye akiudhiwa kidogo tu kakimbilia kwa mtu kwenda kuomba msaada. Lazima uwe imara kukabiliana na masaibu ya maisha. Haina maana usiombe ushauri pale unapozidiwa. Hapana, unapozidiwa huna budi kuomba msaada.

  Nne wanaume wanaenda polepole na ni waangalifu linapokuja suala la kumpata mwenza wa maisha. Wanataka kwanza wamjue msichana ipasavyo, kabla hawajaamua kumuoa. Kwanza anaanza kwa kumpa mialiko ya kutoka naye ili kuweza kuichunguza tabia yake vizuri. Utaratibu huu wa wanaume ndio unaowakera wanawake ambao wanataka kuoana kwa harakaharaka. Waache wanaume wafanye utafiti wao kwani ni kwa faida yenu nyote wawili. Unavyozidi kumshinikiza mwanaume akuoe harakaharaka kabla hajakufahamu vizuri ataanza kukushuku. Unatakiwa usubiri mpaka aseme mwenyewe kwamba angependa kukuoa, hata hivyo unaweza kuanzisha mada ya ndoa kama muda wa mwaka mmoja umepita.

  Tano, onesha kujiamini. Unatakiwa kuwa ni mtu unayeweza kutatua matatizo yaliyo mbele yako. Wanaume wengi wanapenda wanawake wanaojiamini.

  Sita, unapoongea na mwanaume unayempenda, mwangalie machoni kwa mahaba fulani ambayo mwanaume huyo atajua kwamba unamtofautisha na wanaume wengine unaokuwa nao.

  Saba,
  onesha kumkubali na kuukubali uwezo alionao. Na kama analo jambo ambalo ni mtaalamu sana nalo, basi mwambie hivyo na kwamba unafurahia mafanikio yake.

  Nane, kuwa mchangamfu, na hata kama uchangamfu wako utaambatana na kuchekesha ni jambo muhimu sana na katika uhusiano. Usiwe mtu mwenye msimamo mkali kiasi cha mtu kuchagua mada za kuongelea akiwa na wewe. Kuwa mtu rahisi kuingilika.

  Tisa,
  wanawake ambao wana furaha muda wao wote wa maisha yao, wana mvuto kwa wanaume wote. Wanawake wa aina hii ni kama vile wanafurahia kuwa hai! Wanaishi kwa tabu wana furaha; wanaishi kwa raha wanafuraha!


  Kumi,
  mapenzi uliyo nayo moyoni kwa mwanaume huyo yaoneshe hivyo hivyo uwapo mbele yake kila unapokutana naye. Hiyo ndiyo gia kali sana ya kumteka mwanaume unayempenda na ambaye unataka awe mwenza wako wa baadaye.


  Kumi na moja,
  jifunze kuwa mnyenyekevu, mtu mnyenyekevu ni yule anayejishusha awapo mbele za watu. Ni mtu ambaye anaona shida zake ni za pili kuliko shida za wenzake.

  Kumi na mbili, usimkataliye mwanaume unayempenda kutoka naye, jiamini na jenga heshima ya mwili wako na hakikisha unaujali uhusiano wenu. Kutoka ni kwa ajili ya kujuana kiundani kuhusu maisha ya kila mmoja wenu na siyo zaidi ya hapo. Wapo wanaoamni kuwa kutoka maana yake ni kwenda kuonjana, si hivyo mwanamke, kuonjwa onjwa kunaweza kukusababishia ukampoteza huyo mpenzi wako kirahisi.

  Kumi na tatu, baadhi ya wanaume huchukua muda mrefu sana kuamua kukuambia kwamba wangependa kukuoa. Kama unampenda na unaona kwa tabia zake anakufaa kuwa mumeo mtarajiwa, basi endelea kuwa na subira. Kama anaonekana shauku aliyonayo kwako inazidi kupungua na anaanza kuleta visingizio hata baada ya muda mrefu kupita, huna budi kuanza kuangalia mustakabali wa uhusiano wenu. Kumbuka kwambamapenzi ya kweli hayaletwi na kushinikizana.

  Kumi na nne, mapenzi yanatakiwa yatoke pande zote mbili. Mwanaume akionesha kwamba anakupenda basi na wewe muoneshe kwamba unampenda, wala usifiche. Kuficha kwamba unampenda hakuwezi kukusaidia zaidi ya kumkimbiza mpenzi wako huyo.

  Kumi na tano,
  onesha mapenzi yasiyo na masharti, urafiki wa kweli ni wakati wa shida na raha. Mwanamke anatakiwa kuwa karibu na mpenzi wake wakati wa matatizo pia, na si kumtelekeza.

  Kumi na sita, weka malengo, suala la ndoa linatakiwa kuwekewa malengo kama jambo lolote la kimaisha. Maisha yanasonga mbele; anza sasa kujiandaa kwa ajili ya maisha yako ya baadaye ya kindoa.

  Kumi na saba, hakuna mwanaume anayetaka kufunga pingu za maisha na mwanamke mwingi wa mambo na anayejifanya kujulikana sana, hasa na wanaume, ukijifanya kuwachangamkia na kuwa karibu sana na wanaume wengine mbele ya mpenzi wako usitegemee kuvishwa pete ya ndoa, itakula kwako!

  Kumi na nane, ni jambo muhimu kujua sifa uzitakazo ambazo ungependa mumeo mtarajiwa awe nazo. Huo utakuwa ndio muongozo wako mkubwa.

  Kumi na tisa wanaume wengi wanapenda mwanamke mwenye maumbile na tabia ya kike.

  Ishirini, ni muhimu kujali mwili wako, wanaume wanavutiwa na wanawake warembo na wenye mvuto wa kimapenzi. Jipende na hakikisha unajiremba na kujipamba kwa staha na sio kujikandika vipodozi na mikorogo………. Utaharibu. Jitahidi kuwa natural, lakini tumia simple make ups ambazo hazitaubadili muonekano wako kwa kiasi kikubwa.
   
 2. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  duuh mkuu nimefurahia sana...hiyo imewakuta mabint weng sana hasa kujulikana na wanaume wengne,mi napenda sana mke mchangamfu,sifa zote nimezifurahia
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hongera sana kwa bandiko lako..
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Uhhhh!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  majukumu ya mwanamke ni yepi?
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Duh, Aisee hilo sikulikumbuka................ Ok, niliposema majukumu, nilikuwa namaanisha kwamba katika maisha ya ndoa, kati ya mume na mke kunakuwa na mgawanyiko wa majukumu kati ya baba na mama, sikutaka kuyataja kwa sababu majukumu yanatofautiana kati ya familia moja hadi nyingine........ hii ina maana gani, baba anayo majukumu yake kama baba na mama anayo majukumu yake kama mama katika suala zima la kujenga familia iliyo bora.
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  20 zote hizo kisa kupata mtu ambaye nitakuwa Housegirl wake kwa kumfulia, kumpikia, kumzalia watoto, kumfungulia mlango akirudi saa nane usiku akinuka mipombe, kuvumilia anapokoroma usiku, kuvumilia anapotoa siri zangu kwa nyumba ndogo, kuvumilia anappmtongoza Housegirl, anaponunua debe la mabeans while yeye na hawara zake wakitafuna minofu ya kiti moto, kuvumilia anappnidunda kisa nimemkoromea nyumba ndogo wake!! Pfew the list is too tiring!

  Ningezingatia yote hayo hata zaidi ya 20 kama kungekuwa na gurantee kuwa mwanaume atabaki kama alivyokuwa wakati wa kuchumbiana au wa honey moon! Lkn wengi wao Mke ni kwa ajili ya kujenga familia lkn NN ni kwa ajili ya romance na mapenzi moto moto!
   
 8. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante baba,kwa uzi mzuri na wenye kujenga.
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu, Kama hawajakuelewa kazi kwao maana wengine wanataka kusafisha nyota wakati siraha ni wao wenyewe.
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kama majukumu "hayapo wazi" basi sidhani kama mtu akiyajua yake inaweza kuwa sababu ya kuolewa.
   
 11. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana Kaunga............ila nimesikitikitishwa na mtazamo wako kuhusu ndoa.......yaani kwako wewe ni about hapo red....mhhhh!!! Kuna kitu fulani nimejifunza, what you expect is what you get......nakushauri badili mtazamo wako...................na muombe Mungu atakupa mume mwema.

  Ubarikiwe.
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Ni kweli,lakini now days watu hawako real!
   
 13. C

  CYPRIAN MKALI Senior Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  you are very right, tukumbuke pia ni jukumu la mwanamke pia kujiridhisha na huyo aliyompenda kwa kipindi cha kuchunguzana.sasa ukikuta mumeo anatoa siri zako nje basi ujue hukuwa makini kumsoma kwani kama kichwa chake kimetulia hayo unayoyasema inakuwa ngumu uizingatia wanaume upenda kusolve matatizo yao wenyewe na ikishindikana wanapiga chini bila ya kwenda kwa balozi.
  amini ni wako peke yako ili kulinda ndoa yako, sasa ukiamini ni wa wote ina maana hutatimiza majukumu yako vizuri na hivyo suala la ndoa bora utalisikia tu kwa majirani. maisha sio magumu ila mwenyewe ndo unaweza yafanya yawe magumu!!!!
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ameeeeeeeeen
   
 15. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu safi sana hii!!
   
 16. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,665
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Ooh! Kaunga uko deep, umewajua wanaume kweli kweli.....
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  KK; sitafuti mume wa pili! Ninachojaribu kuelezea ni kwamba a lot is expected about a woman as if yeye pekee first and foremost ndiye pekee muhitaji wa ndoa; pili yeye ndiye anayewajibika kulinda ndoa and hence ni yeye anayepaswa kulaumiwa isipowork out.

  Rejea nyuzi nyingi jinsi gani wanaume wengi wanavyosupport wenzao wanavyofanya madudu! Na hata sisi twasipport na kuanza kuwasema wanawake wenzetu kuwa wamesababisha; it is so pathetic!

  Kuna nyuzi ngapi za kuwafunda wanaume ili wawe waume bora?

  I spoke for women in general not because of me? Na kama unaona nazisisha chumvi tufanye kautafiti kadogo humu2 ndani kama hayo ya kwenye red hayatokei!
   
 18. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Swadakta. Hasa Na. 4 inakimbiza sana watu.
   
 19. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kama ungeijua dhana ya kuoa na kuolewa labda usingepata tabu ya kuwaza hayo uyawazayo...........
  Look...........
  1.Mwanamke anasubiri kutongozwa au sijui niseme kuposwa na mwanaume
  2. Anasubiri kulipiwa mahari na mwanaume
  3. Anasubiri kuolewa na mwanaume
  4. Anaondoka kwao na kuhamia kwa mwanaume na kuanzisha familia

  Mlolongo ni mrefu sana........ hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba pia wanaume wanapaswa kufundwa kuhusu kum-handle mwanamke na ndio maana hapo zamani kulikuwa na jando na Unyago, lakini kiuhalisia mwanamke ndiye anayewajibika kwa kiasi kikubwa kumvutia mwanaume ili aolewe na pia kulinda uhusiano huo tofauti na wanaume kwa sababu mwisho wa siku yeye ndiye muathirika....haya mambo yamekaa ki-mfumo Dume na nimekuwa nikiandika hapa karibu kila siku.....................

  -
   
Loading...