Kama unataka kuishi maisha marefu na yenye afya mpaka uwaone wajukuu zako Fanya mambo haya

Hedika

Member
Jan 16, 2018
17
35
Kwa kawaida hakuna Mtu ambaye hapendi kuishi maisha marefu lakini tu watu hawajui ni namna gani ya kufanya ili wayaishi hayo maisha marefu mpaka waseme ahsante MUNGU sasa waweza kutimiza mapenzi yako.
Katika kitabu cha zaburi kwa wale wakristo kimeandika miaka ya MTU ni miaka 70 na kama unanguvu ni miaka 80.
Je nawezaje kuifikia miaka iliyoandikwa katika biblia?
Kwa kawaida makosa unayofanya katika umri flani hukuhukumu katika umri flani. Umri wetu umegawanyika katika vipindi tofauti tofauti yaani utoto, ujana moto, ujana tuli, makamo na uzee. Katika hivi vipindi kipindi cha utoto mtu huwa katika uangalizi mzuri kabisa wa mzazi na makosa ambayo hufanywa na mzazi katika kipindi hiki ndio humrejerea mtoto katika umri wa utoto au ujana moto na kumpelekea kushindwa kufikia miaka iliyotajwa katika kitabu kitakatifu. Mfano kama mama hatampa mtoto chakula safi au kama hatamlaza mtoto katika chandarua mtoto atapata maradhi na atakufa katika umri wa utoto. Lakini pia mzazi kama hatamfundisha mtoto wake maadili mema atapelekea mtoto Huyo kuwa na maadili mabovu ambayo yatamfanya ashindwe kuvuka umri wa ujana kwani watoto wengi waliokuwa na maadili mabovu huishia maisha yao katika umri wa ujana na kama akijaliwa kupata ushauri mzuri ndipo huweza kunusurika. Mfano wa tabia mbaya ambazo huibuka kutokana na makezi mabovu ni kama umalaya, wizi na matumizi ya madawa ya kulevya. Mambo haya humfanya Mtu ashindwe kufikia umri wa uzee.

Mtoto aliyelelewa katika malezi bora akifika katika umri wa ujana moto au ujana tuli huweza kuachana na familia na kuanza maisha yake katika umri huu ndipo mtu huandaa umri wake wa makamo ili kuweza kufikia umri huu kitu kikubwa kimoja ambacho ni muhim sana kwake ni kuepuka mitindo mibovu ya maisha kama vyakula vinywaji mavazi vipodozi na hata tabia kwani kama ukiendekeza tabia za kula mafuta mengi kutokufanya mazoezi ulevi hasa wa pombe Kali na uzinzi miaka 50 hutaifikia tutakuzika katika umri wa 30-45 kwa magonjwa ya presha, sukari, Kansa na hata UKIMWI. Hivyo ukiepuka mambo tajwa hapo juu unapokelewa na akina mzee baba na kula bata umri wa makamo. Baada ya kuvuka 40's kama umevuka bila kubeba maradhi tajwa hapo juu we anza kula vizuri tu nakuhakikishia 70 inakuhusu na baada ya sabini sasa ili uguse 80 uwe unawatoto wa kukutunza kukujali upate furaha unaweza ukakuta unagonga 100. Kama. Mzahaa.

Zingatia katika maelezo yangu nimejikita zaidi katika nia yako ya kutaka kufikia miaka hiyo ni kujitunza na kuishi vizuri ukijua kuwamwili makosa yako ndio hukumu ya umri wako wa kuishi. Mambo kama ajali, majanga na maamuzi hasi kama kujiua nimeweka pembeni.

Kama ukitaka kujua ukweli juu ya hili nchi maskini tunakufa katika umri mdogo yaani ukitembea mitaani unaweza kukutana maelfu ya watu ila kati yao wazee hawazidi 50 hivi hawa wengine huishia wapi hufa katika umri wa ujana . jitunze uufurahie uumbaji wa MUNGU.

Nawatakieni jumapili njema.
Mwl hedika
 
Una point hapa,sasa uzee wenyewe uwe wa afya basi sio unaishi maisha marefu lkn ya mateso, full kuumwa!ila nimekuelewa kiongozi
 
Tokea Ngosha aingie madarakani kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya FREEmind, umri wa kuishi umepungua mno tena kwa kasi ya ajabu
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Tangu mwaka 2015 hadi mwaka jana 2017 mimi nimeishi takribani miaka 6 . January hii tu nimeishi miaka 3 yaani hadi natamani usiku usiingie .
 
Mkuu we sasa unafaidi miaka 3 in one month!!!!!!
 
Ukweli mtupu umenena mkuu, asante kwa ujumbe mzuri hasa kwetu sisi vijana.
 
Kuna mtu alikwenda kwa Dr ili apate ushauri, afanye nini ili aweze kuishi miaka 100? Dr akamwambia "Usinywe pombe, usivute sigara wala usifanye ngono!" Kwakuwa jamaa alikuwa mlevi na fuska mzuri, alishtuka sana akamuuliza tena Dr, "Dah, kwahiyo nikiacha vitu hivyo ndio nitaishi miaka 100? Dr akamjibu "Utajihisi kuishi miaka 100!"
 
Back
Top Bottom