Kama unao mtaji wa kuanzisha kilimo_biashara ila huna msimamizi/patner sahihi mimi nipo tayari, tuunganishe nguvu tusonge mbele.

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Habari za jioni wakuu,
Mimi naamini katika kilimo katika kuufikia uhuru wa kipato. Nimekuwa na ndoto ya kuwa miongoni mwa wakulima mwenye mafanikio makubwa.


Changamoto pekee inayonikabili mpaka naandika uzi huu ni kutokuwa na mtaji wa kuanzisha kilimo chenye tija (ekari nyingi angalau kuanzia 20+) hivyo mchango wangu utakuwa ni muda, nguvu, maarifa na uaminifu katika mradi.

Naamini wapo wenye nia kama yangu, wenye kuamini katika kilimo kama mimi na wenye mtaji wa kutosha kuanzisha kilimo ila hawana muda wala watu sahihi wa kukisimamia. Mimi ni mtu sahihi kwakuwa ninakipenda kilimo. Sasa basi kama tunavyojua Mungu hawezi kukupa kila kitu ili unachokosa ukipate kwa wenzako, mimi muda wa kutosha ninao kuanzia mwanzo wa mchakato hadi mwisho.

Nipo Dar, nipo tayari kwenda mkoa wowote kulingana na mahitaji ya kilimo husika.

Makubaliano na mambo mengine mengi muhimu tutayajadili kwa kadri Mungu atakavyotubariki.

Kwa aliye tayari tuwasiliane tafadhali.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Una idea nzuri ila ubaya zaidi haupo field husika ...yaan unaogelea kilimo cha mpunga wakati upo tegeta nyuki ...ni vzr kuongelea kilimo ukiwa mashambani !
 
Back
Top Bottom