Kama unampenda utamvumilia

Kama unampenda utamvumilia

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
373
Reaction score
467
KAMA KWELI UNAMPENDA MVUMILIE
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷

Wahenga walisema mvumilivu hula mbivu.Ndoa nyingi za mababu na mabibi zetu zilidumu sana mpaka kufikia hatua ya kufa na kuzikana .
Lakini ndoa nyingi za siku hizi hazidumu miongoni mwa chanzo kikubwa cha matatizo ni wanandoa kukosa kuvumiliana.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷

Katika safari ya mapenzi wanandoa hupitia vipindi mbalimbali,Kuna vipindi vya furaha, vipindi vya udhuni na misukosuko. Hali hii utokana na changamoto nyingi sana wanazozipitia wanandoa.

Moja ya changamoto kubwa wanayopitia wanawanake ni changamoto ya kutokupata mtoto ,wanawake ambao hawajabahatika kupata watoto, wengi wao hupata tabu sana kwenye ndoa zao hunyanyaswa ,husimangwa na waume zao na hata hufikia kuchukiwa na familia ya upande wa mume.

🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Ushauri wangu kwako mume ambaye mkeo upo naye kwa kipindi kirefu cha ndoa yenu na hamjabahatika kupata watoto
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
:Kwanza unatakiwa utambue kuwa watoto ni viumbe na mwenye kuumba viumbe ni Mwenyezi Mungu kwa hiyo pamoja na jitihada za kibinadamu lakini pia Msichoke kumuomba Mungu kwa nguvu zote kwani Mungu ni Mwenye kujibu Maombi ya waja wake.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Pili ni muhimu kwenda kufanya vipimo ili igundulike chanzo cha tatizo husika ni nini ili kupata ufumbuzi, kuna matatizo mengi yanatibika ,kuliko kukazania kumpa lawama mwanamke na kumsimanga kwani hauwezijua kiini cha tatizo huenda tatizo likawa lipo kwako au likawepo kwa wote.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Tatu mpe faraja mkeo na jitahidi kuwa sehemu ya furaha yake huku mkiwa na matarajio yaliyo mema juu yenu kwakuwa katika maisha ya duniani kuamua kukata tamaa ni sababu kuu ya kutokufanikiwa , endapo mtakuwa pamoja katika kila hatua na katika kila hali mtaoongeza matumaini ya kufanikisha malengo yenu na Mungu atawajalia.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷

Na kwa upande wa pili nawashauri dada zangu wawe wavumilivu kwa waume zao wanapopitia changamoto ya kuwa na kipato duni au kukosa kazi.
Kama uliolewa na mwanaume akiwa na hali nzuri ya kiuchumi ikatokea akafilisika au kufukuzwa kazi au likatokea jambo lolote likapelekea uchumi wake kuyumba nakushauri usikimbilie kudai talaka.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Kwanza Muombee kwa Mungu sana Mumeo funga na kusali kwa ajili yake kwakuwa Riziki anayetoa ni Mungu nahuo ni mtihani kwenu muombe Mungu sana ili muuvuke salama kwani siku zote dua ya Mke kwa Mumewe hujibiwa kwa haraka.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Pili usimcheat na kumsaliti mumeo eti kwa sababu tu kuna baadhi ya mahitaji unayakosa toka kwake kuwa mvumilivu na usikubali kuuza utu wako kwa tamaa ya pesa kumbuka malipo ni hapa hapa duniani na majuto yatakuwa ndio malipo yako.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Tatu ni vyema mkapanga bajeti kulingana na hali ya kipato pia ukiwa kama wanamke ni vizuri kumshauri mumeo ili akuruhusu kufanya japo biashara ndogondogo ili kusaidia kuongeza kipato na kukidhi mahitaji yenu.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Mwisho mpe faraja Mumeo na usimuoneshee dharau wala kebehi kwani siku zote Mke mwema humfanya mwanamme masikini ajihisi tajiri.
Penye furaha na amani ndipo penye mapenzi ya kweli mapenzi sio pesa japo ikisokena ladha ya mapenzi hupungua kama mwanamke jasiri jitahidi uirejeshe hyo ladha ya mapenzi kwa mumeo.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Mapenzi ya kweli hutoka moyoni mwenyekupenda kweli huwa mvumilivu katika kila hali ,mwenye mapenzi ya kweli siku zote hayupo tayari kumpoteza ampendaye.subira inamalipo mema siku zote.
 
Zamani wanawake hawakupewa nafasi ya kusoma hivyo wengi wao walilazimika kuvumilia ndoa kwakuwa hawakuwa na namna yeyote ile ya kuwafanya waweze kujitegemea lakini kiuhalisia wapo ambao hawakuwa na mapenzi ya dhati na ndoa zao zikabebwa na ujinga na ile hali ya kukuzwa na kuaminishwa kumuogopa mwanaume
 
πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚ mkuu ungekuwa unaandikia pen ningekuambia acha kupoteza wino, dunia ya sasa watu wamekengeuka upendo hamna kimebaki mapenzi na maigizo tu kila siku ndoa zinavunjika .wanaume na wanawake wanaishi kwa kukomoana wanaume wanapanga yao na wanawake hivyo hivyo, yani nivurugu tu mpaka wanasayansi wameamua kutengeneza doll, Samantha yani shida tupu tunakoelekea ni kubaya .mimi nikaaga peke yangu nikiwaza mambo ya yanayo tukia nasemaga bora kiama kiwahi tu, wa mbinguni waende mbinguni na sisi wa motoni tuende motoni πŸ˜‚πŸ€£ maana hali sio shwali kabisa
 
Back
Top Bottom