Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,227
KAMA UNAJALI UTAMWAMBIA UKWELI HUTOACHA APOTEE
Moja ya vitu vinavyotufanya tunaendelea kuwepo duniani kama binadamu ni kujali. Ndio tunajali sana kuhusu sisi wenyewe na hata wale wanaotuzunguka.
Tunapenda kuona tupo kwenye hali salama na hata wale wa karibu yetu pia tunapenda kuona wapo salama.
Lakini kujali huku pia kunakuja na hasara zake, kuna kujali ambapo kunakuumiza wewe mwenyewe au wale ambao wanakuzunguka.
Leo tutaangalia kujali ambapo kunawaumiza wale ambao ni wa karibu yetu.
Tuseme labda kuna mtu wako wa karibu, ndugu, mtoto, mwenza au rafiki na amekuja kwako ana mpango wa kufanya jambo fulani kubwa kwenye maisha yake. Na wewe kwa unavyomfahamu unaona kabisa hawezi. Hivyo kwa kuwa unamjali unamwambia ukweli, hiki unachotaka kufanya hutaweza au kitakushinda.
Umemwambia hilo kwa nia njema kabisa, kwa sababu unamjali, kwa sababu hutaki kumwona akipata shida au kuingia kwenye changamoto, unastahili hongera! Si ndio?
Japo unajali, lakini hapa umemuumiza sana huyu mtu. Umemuumiza kiasi kikubwa sana na hataweza kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yake. Na vile ulivyo mtu wa karibu kwa uliyemwambia, basi anaamini sana maneno yako.
UNAWEZAJE KUTUMIA KUJALI KWAKO KUMSAIDIA MTU WA KARIBU YAKO?
Baada ya yeye kukuambia mpango mkubwa alionao, hebu taka kujua zaidi ni kiasi gani amejipanga.
Mwambie akueleze vizuri ni jinsi gani atakavyosonga mbele kama mambo hayatakwenda kama alivyopanga. Na kulingana na majibu yake utajua amejipanga kiasi gani.
Na mwishoni, angalia ni jinsi gani inawezekana kwake, ni maeneo gani muhimu azingatie.
Halafu mpe moyo afanye, mhamasishe asonge mbele hata kama atakutana na changamoto.
Lakini vipi akishindwa?
Si nitaonekana sikumtahadharisha mapema?
Ndio atashindwa, tena mara nyingi tu. Hapana, hutaonekana kwamba hukumtahadharisha.
Na kushindwa huku ni faida kwake, kwa sababu atajifunza zaidi.
Atakuwa mbali zaidi kuliko ambavyo angeacha kufanya kabisa.
Na kama amejitoa kweli, ni rahisi kwake kutokea hapo kwenye kushindwa, kuliko kuanzia mwanzo kabisa.
Kujali kwako kusiwe kikwazo cha wengine kushindwa kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yako. bali kuwe hamasa ya watu kuchukua hatua zaidi.