Ozzanne Issakwisa
JF-Expert Member
- Mar 7, 2016
- 288
- 240
- Asubuhi unapaki gari katika mkao wa kuchomoka kirahisi.
- Una masaa zaidi ya mawili ya breakfast na lunch tu.
- Mida ya kazi upo active online hususani kwenye groups (kama Whatsapp) lakini weekend hutii mguu.
- Unapanga na kukusanya vitu vyako kama handbag na kuomba lift saa moja kabla ya muda wa kazi kuisha.
- Ikibaki nusu saa unaingia washroom.
- Robo saa kabla ya kutoka unaanza kujiweka vizuri, kama kufunga kamba viatu au kujipodoa.
- Dakika kumi zilizobaki wazitumia kuaga rafiki au kupanga ratiba ya huko nje.
- Juu ya mshare ushatoka nje ya geti.
- Ndani ya dk 5 toka utoke nje gari yako haionekani.
- Umezoea kwenda bar, club, harusini n.k. siku za kazi huku ukijua kesho unatakiwa kazini.