jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 19,127
- 35,986
Nipe uzoefu wako kwa dsm..soko la nguruwe liko wapi?Nilikuwa natumia gari ndogo mkuu, sana sana kirikuu
Nawakusanya kwa siku kama mbili au tatu halafu napiga simu Mwanza wanaleta gari
Changamoto unaweza ukanunua nguruwe kwenye nyumba kumi maeneo tofauti gari ikija mnaanza kupita nyumba moja mpaka ya mwisho tunapakia tunaondoka
Pia ukishawalipia wakati unasubiri usafiri
mwenye mji anakwambia gharama za kuwalisha ni zako mpaka utakapokuja kuwachukua.
Kirikuu inakaa wastani wa nguruwe 12 wodogo na 9 wakubwa
Kibali ilikua tunakata Buselesele
kila nguruwe Tsh1000
Kila nguruwe nilikuwa naweza kupata faida ya Tsh 50,000 ila sehemu kubwa ya faida inaliwa na usafiri.
#MaendeleoHayanaChama