Kama una mpenzi wako na anajua una biashara ila hakuna hata siku moja umemsikia akikwambia baby pole sana...

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
Kama una mpenzi wako na anajua una biashara ila hakuna hata siku moja umemsikia akikwambia baby pole sana najua biashara yako inaathirika sana na hili janga la corona. Nakuombea mwenyeezi Mungu akupe moyo wa uvumilivu.

Ama hajawahi kuonyesha huruma yoyote kwa biashara yako ama shuhuli yako zaidi ya yeye kuwaza anapataje pesa kwako.

Basi ndugu una mtihani mkubwa sana kufikia kitu kinaitwa mafanikio. Kuna mapungufu unapaswa kuyavumilia ila asieonesha kuguswa na athari ya majange kwenye mishe zako huyo hafai hata kuwa rafiki sio tu mpenzi.

Nashukuru shemeji yenu kila mara anasema dah sasa dear na hii corona biashara inadorora si unapitia magumu sana, pole dear Mungu akupitishe salama.

Kama wewe huambiwi delete fasta mapenzi sio kuburudishana ila kujaliana. Afu hawa wasiojali chochote kwenye biashara zako au mishe zako ndio wanatakaga ujali hadi birthday zao. Hata chembe ya aibu hawana.

Jamani ikikugusa pole sijakusudia kumlenga mtu ila lengo langu kila mtu ajirekebishe ili kujenga mafanikio kwa kila kijana wa kitanzania. #miamiatz #KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi #UstawiKwaWote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna binti niliwahi mshirikisha mpango Wa kama million 2 hivi. Nilimwambia hizi pesa nahitaji kuzizungusha ili tukioana tusipate taabu.
Nikampa detail za miradi 5 hivi ambayo kila mwezi laki tatu hatukosi.

Alichijibu "nimekuelewa sana na mipango yako nimeona ni mizuri, suala la mradi upi utekelezwe lipo na wewe mwenyewe. Mimi ninunulie simu ya laki 2.5 tu mengine utajua mwenyewe."

Aisee niliona hapa sina future wife wala wife material, nikaachana nae.
 
Good

Sio chai hiii?!! 😂😂😂😂
 
Mnawasema tu wanawake..jamani kizazi hiki Mungu aepushie..wanaume mmekia vitonga kupita neno lenyewe Kitonga! Mnawasingizia sana wadada lakini amini amin nakuambia wanaume wengi wa sasa hv wanaomb kuliko kawaida!
men unamwelezea deal fulani yeye anachojali kukuchomoa hela zako ..badala ya kukusaport!
 
Nina demu amaizing Sana, yaan Ni wa kitofauti. Nakiri kabisa hata ikitokea tukatemana, atakaemuoa hatajutia.

Read my signature below

WANA JAMII FORUMS, TUSIFANYE MAKOSA TENA OCT 2020

Signature yako imenibariki mkuu
 
Kuna binti niliwahi mshirikisha mpango Wa kama million 2 hivi. Nilimwambia hizi pesa nahitaji kuzizungusha ili tukioana tusipate taabu.
Nikampa detail za miradi 5 hivi ambayo kila mwezi laki tatu hatukosi.

Alichijibu "nimekuelewa sana na mipango yako nimeona ni mizuri, suala la mradi upi utekelezwe lipo na wewe mwenyewe. Mimi ninunulie simu ya laki 2.5 tu mengine utajua mwenyewe."

Aisee niliona hapa sina future wife wala wife material, nikaachana nae.
Simu ya laki 2.5 ni ipi mkuu? Au tecno?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom