Kama umepatia haya wewe ni shujaa

sambeke

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
702
1,000
*UTAJUAJE KAMA WEWE NI SHUJAA???*


1. Kama ulikata daftari mara mbili. Kipande kimoja ukaacha nyumbani na kingine ukaenda nacho shule. We ni shujaa.
2. Kama ulitumia kipande cha kandambili kama ufutio.
3. Kama ulikanyagia kisigino ulipotoka kuoga ili usichafuke kwa kuwa hauna kandambili....nakusalimu.
4. Kama kwenu mlianika betri za national ili ziongezeke chaji kwenu ni mashujaa.
5. Kama msichana ulienda mtoni ukakamata kale kamdudu kanapenda kucheza juu ya maji ukakaumisha kwenye nyonyo ili ziwe kubwa.......
6. Kama ulilala na sare za shule ili asubuhi usichelewe halafu asubuhi ukajikuta umejikojolea wewe ni shujaa.
7. Kama ulienda choo porini na ukajipangusa kwa nyasi hongera aisee.....
8. Kama uliweka chumvi kwenye uji mweupe ndio ukanywa....
9. Kama ulilamba sukari ukapangusa mikono na ukasahau mdomo....sema kichapo heheeee
10. Kama ulijifanya unalala ili upewe chapati mbili za kwanza aisee wewe shujaa.
11. Kama ulivaa kandambili za baba yako ukiwa darasa la 3 au la 2....hakika ulikuwa na ndoto shujaa wangu.
12. Kama uliogeshwa halafu ukaanikwa nje kwenye gunia haleluya wewe ni shujaa...
13. Kama ulinyolewa kwa wembe halafu ukatoka maturu na mashilingi.....
14. Kama ulibeba chakula kwenda shule kwenye kopo la mafuta ya Kimbo halafu kufika shule ykajikuta umebeba mafuta badala ya chakula...utakuwa nani kama sio shujaa?
15. Kama ulikuwa unatumwa ukaombe moto wewe ni shujaa....
16. Kama ulikuwa unakula queencake na unatafuna hadi karatasi.....shujaa wangu wa nguvu.....
17. Kama ulikuwa unavalishwa sare ya shule mkienda mjini hakika umefuzu.
18. Kama ulimuona yule jogoo wa TLP akiwa kifaranga......nakuapia wewe ni shujaa.
19. Kama dada yako au mpenzi wako alichoma nywele kwa mkebe wenye makaa ya moto (blow hot)....ninakupigia saluti.
20. Kama ulivaa suruali ya SAVCO, BIOACT na TOKYO na raba za LOSO au NORTH STAR...hao wengine ni mfano wa mashujaa tu.
21. Kama uliona mwanzo wa tamthilia ya The Bold and Beautifu au The Days of Our Lives.....
22. Kama visiting day shuleni baba yako alikuletea gazeti wakati wenzako wakiletewa chapati....shikamoo.
23. Kama kwenu kulikuwa na mwavuli mmoja wa kupeleka mtoto akipelekwa clinick na mvua ikinyesha mnajifunika kwa magunia.....
24. Kama uliogea karai la chuma.
25. Kama uliambiwa ushike sikio la kulia kwa kupitisha mkono wa kushoto juu ya kichwa ndio uende darasa la kwanza.....we ni rika na Anko J Kitime
26. Kama ulipaka mafuta yanaitwa RAYS ya bluu....wewe ni shujaa kama Kaka Gano
27. Kama sare yako ya shule ilikuwa na viraka vingi hadi watu wasitambue rangi ya sare ya shule yenu.....duh!
28. Kama ulichukia ule wimbo wa Maroon Commandos "hata wewe mwanafunzi amka kumekucha, hii ndiyo saa ya kwenda shule." Edo Kumwembe anatakiwa kukuamkia.
29. Kama kwenu mlikuwa na radio ya mbao aina ya SANYO wewe ni shujaa.
30. Kama ulipokuwa kijijini ukimuona baba wa jirani akirudi toka safari ulikuwa unakimbia walau kilomita 2 kwenda kuipasha familia yake "baba yenu anakuja"
31. Kama mlitumwa unga wa ngano kidogo kidogo kwa ajili ya kubandikia chart shuleni wewe ni mhenga.
32. Kama uliwaambia wazazi unaumwa tumbo kisha wakakuambia koroga chumvi kwenye maji kisha ukimbie shule....wewe kama sio shujaa ni nani?
33. Kama uliiimba mwenye kujamba tumbo lake lipasuke mara tatu kutuushhhh! Na ukawa pointed wewe ni shujaa.
34. Kama ulivalishwa mfupa wa ng'ombe shingoni kwa kuwa msumbufu darasani....
35. Kama ulishawahi kujifunga kamba matakoni siku mnakaguliwa nguo za ndani....wewe ni shujaa mkuu...
36. Kama ulikuwa unaenda kuangalia sinema ya kitambaa "watoto kaeni chini" ....
37. Kama ulivalishwa nepi na sio papmpers.....
38. Kama ulikunywa maji kwa kata na ukaogea sabuni ya REXONA wewe ni......
39. Kama wewe ni mwanamke na unakulaga maparachichi mawili peke yako......shujaa ni wewe.
40. Kama ulipenya njaa ya mwaka 1984 na bado unaijua facebook wewe ni shujaa.
41. Kama ulipakwa Giv au mafuta ya breki ya AGIP kwenye kidonda.....
42. Kama ulienda haja kubwa na ukajipangusa kwa mchanga au mawe .....wewe ni.......
43. Kama suruali ya kwanza ulivaa ukiwa sekondari....hata wewe ni shujaa.
44. Kama wewe ulikuwa hupati usingizi kwa kuwa una begi jipya au raba mpya za DH pia ni shujaa....
45. Kama ulienda shule peku huku umebeba kuni na maji ya kuwapikia walimu...hakika wewe ni rika na Kingunge Ngombale Mwiru.
46. Kama ulivaa kandambili mikononi wakati mnacheza mpira wa makaratasi "one touch".....
47. Kama uliweka kioo chini ya dawati ili uwachungulie wasichana...
48. Kama mpiga picha alishakuambia picha yako imeungua basi wahi kwenye foleni....
49. Kama ulishaimba " nasikia sauti ya mama. Sasa ni saa sita.....kwaheri mwalimu".....
50. Kama ulikuwa unaamini kuwa Nyerere ni rais wa Uganda.
 

Arie power

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
2,556
2,000
Nakumbuka nilimkimbilia baba wa rafiki yangu alikuwa anatoka kazini nikamwambie mwanae kafaulu la saba
 

kibaa

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
718
225
namba 22 inanifanya nionekane mwehu kwenye bus kwa jinsi nilivyocheka kwa nguvu
 

ikisimama panda

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,126
2,000
ukisema namba flani sema kabisa inaelezea nini sio uturudishe kuangalia inasemaje acheni ujinga,, atakae endelea kufanya hivo kudadake zake
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,342
2,000
Na kama ulikuwa unasikia ule wimbo wa Marijani Rajabu kila siku asubuhi radio Tanzania unaimba ''kumekuchaa sasa kumekuchaa.. majogo vijijini wanawika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom