Kama uliwahi kurogwa au unamfahamu aliyerogwa elezea hapa na wengine wajifunze

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,393
1. Ndugu mmoja alipigwa marufuku kukatiza katika uwanja wa jirani akiwa anatoka kuteka maji. Huyu dada hakusikia akawa analazimisha, Yule mzee akampa onyo la mwisho, Kwa kiburi ndugu yule akalazimisha kupita. Siku iliyofuata alishangaa miguu inaishiwa nguvu na inakuwa ya baridi.

Tangu siku hiyo hakuweza kutembea na miguu ikawa myembamba nadhaifu. Alihangaika hospitali zote hadi baada kama ya mwaka na nusu alipopata dawa ya kienyeji haikuchukua wiki akwa mzima. Hadi sasa ni miaka zaidi ya 20 imepita ni mzima kabisa. Tafiti za kichawi zinaonyesha aliyemlemaza ni yule mzee jirani aliyekuwa hataki apite nyumbani kwake.

2. Kuna bibi alikuwa na wasichana watatu nyumbani kwake ila hawaongei muda wote. Wanamfanyia kazi zote hadi kupika. Siku bibi ameondoka kidogo, Jamaa aliyeniambia anasema akaforce kumuongelesha mmoja ambae muda wote alikuwa akimkazia macho kama anahitaji msaada ila kusema hawezi.

Alipofanikiwa kumuongelesha akajibu, Yule dada alishtuka kama mtu aliyeusingizini, akakimbia kama mwehu haijulikani aliishia wapi. Inaonekana Bibi alikuwa amewaloga hao wadada kutoka sehemu nyingine na wanamsaidia kazi, Ile kuongea ilimtegua na akili zikamrudia akapata fahamu.

Bibi aliporudi alimpa adhabu huyu mdau wangu, anasema alimgusa tu, jamaa akatembea siku nzima alipozinduka akili akajikuta kumbe alikuwa anatembea chini ya mti na kuzunguka hapohapo tu siku nzima. Ilibidi akimbie kijiji.

Kama unaushuhuda au story ya mtu kulogwa au wewe umewahi kulogwa unaweza kuleta na useme alisaidiwaje.

Wasalam
 
Back
Top Bottom