Visa na Mikasa vya uchawi, kidogo niwe kipofu

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Hello jamiiforum,hope mu wazima wa afya ndugu zanguni.

Kwenye mada, Kama heading inavyosomeka ni kwamba

Nikiwa mtoto wa darasa la nne shule fulani mkoani,nilitokewa na muujiza ambao kwa wakati ule ulinitesa sana Tena mno sijui nisemeje,

Iko hivi ilikuwa ni mwezi wa sita tumetoka kumaliza mitihani ya kufungia shule ule muhula wa kwanza,kwahiyo kama kawaida yetu tuliosoma shule za kayumba hasa vijijini michezo ikawa imetawala.

Hawa wanacheza mpira wa makaratasi,huku rede, wengine wanazurura mtaani tu basi fujo tupu

Sasa basi mimi siku hiyo nilikuwa darasani na wanafunzi wachache tunatengeneza ndoano ili tukitoka hapo twende kuvua kwenye mto flani ulokuwa jirani na shule,utoto ni shida wakuu,basi

Wakati zoezi likiendelea akaja mwalimu mkuu akatuuliza,mnafanya nini? Tukamjibu tunajisomea na Ni kweli madaftari yalikuwa juu ya dawati,

Japo hatukuwa tunasoma tulikuwa tunachomoa vile vipini vinavyobana Yale makaratasi ambavyo ndio Ndoano zenyewe.

Nakumbuka yule madam alitupongeza sana,mitihani mmemaliza.....lakini bado. Mnajisomea!?! kitendo ambacho kwa shule za vijijini ni aghalabu kutokea.

Wakati anaondoka akaita Itovanilo nifuate,hapa ndipo stori inapoanzia

Najua aliniita kwakuwa nilikuwa si haba, very bright kuanzia usafi wa mavazi hadi kuongoza masomo darasani pia nilikuwa mkubwa we darasa la. Nne nina 14 years

Basi akaniambia nenda kwa madam Rose (siyo jina halisi) kachukue misumari ili niwape mafundi, ambao walikuwa wanaendelea na zoezi la kupaua madarasa mapya kwa ufadhili wa kampuni flani kule mkoani

Nani ambaye angetumwa kwa madam Rose angekataa,Hana mume au hakuwa ameolewa alikuwa mzuri,sura, shape hadi upole,nilimpenda akikutuma kwake unaingia hadi chumbani

Unagalagala weeee kwenye kile kitanda Cha chuma na spring zake za mduara,watu wanagombea kutumwa na yeye

Ndiye aliyekuwa anaongoza kwenda mjini ndio maana hata vifaa. Vingi vya shule alikuwa anaagizwa yeye

Barua Zote alikuwa anachukua kule mjini anakuja nazo kijijini ziwafikie walengwa.

Tuache masihara madam alikuwa pisi kali bwana Kuna mchizi ambaye ye alikuwa darasa la sita aliwahi kusema eti kwanini hakuzaliwa mapema ili awe umri sawa na madam Rose

Unazikuta chupi kaanika kwenye kwamba uani unanusa moja baada ya nyingine huku mkuyenge umesimama utoto rahaa jamani

So wakati naenda nilikutana nae njiani nikamweleza nilichotumwa na mkuu wa shule,akanijibu niende tu nikasukume mlango na huo mzigo upo tu sebuleni

Naam punde kidogo nikafika,lakini Kama mjuavyo ule ukorofi wa kitoto licha ya kuchukua ule mfuko nikawa nachungulia chumban kwa madam Rose,aiseeeh nilikutana na kitu Cha ajabu Sana mtu si mtu mnyama si mnyama yaani sitosahau rangi kama ya mtu albino (zeruzeru)

Miguu ikashika ganzi,nikabaki natetemeka na macho yakawa yanajaa ukungu,nikaona hapa nijivute tu. Nitoke nje ,nikajitahidi kujizoazoa kufika nje

Macho yakawa yapo shwari kabisa,basi nilipata nguvu za ajabu nikatimua mbio kuelekea home na si shule tena

Dah,kufika home mdingi akatambua kuwa ujio wangu si wa kawaida labda Kuna hatari,basi nikawa nalia tu muda huo wakanituliza Sana hatimaye nikawaeleza mkasa mzima

Baba aliingia chumbani akatoka na dawa flani.akachanganya na asali akanipaka usoni Kisha akaondoka. after 30 minutes akarejea akiwa na Babu mmoja ambaye ninamfahamu

Babu aliniangalia akatabasamu,akamwambia baba kwanini umempaka hiyo dawa ,je una uhakika hajawahi kutembea na mwanamke,baba akaguna kuonesha Hana uhakika

Babu akanambia kuwa nimweleze ukweli Kama niliwahi kulala na mwanamke nimwambie. Alisisitiza sana na kunambia Kama niliwahi basi atafute namna. Na dawa zingine na shughuli ingekuwa kubwa

Nikamwambia sijawahi, naam Ni nilikuwa na marafiki wengi wa kike ila hata zile kombolela sikuwahi kumbahatisha hata mmoja

Basi yule Babu akasema kama Ni hivyo basi.zoezi siyo gumu akachukua. kioo akasema jitazame nikawa najiona usoni nipo vizuri,wakati nimepakazwa asali na midawa kibao nikijiangalia kwenye kioo chetu naona jinsi uso ulivyojaa asali lakini hapohapo kioo Cha Babu naonekana Safi kabisa baba anauliza hii nj Nini Babu akajibu hii inaashiria katakasika Mambo aliyoona hayawezi kumletea madhara . sitosahau

Babu akanipa pole na kunihakikishia sitopata tatizo lolote,huku akitania nimtafute bibi(mchumba)ili nisiwe naona. Vitu vya.ajabu. akasema napaswa kuutoka umalaika na kuwa human being kamili

Baada ya.hapo yule Babu na mdingi walinipeleka shule mwl mkuu akaelezwa kisa chote alipigwa na butwaa. Pia alinilaumu kitendo Cha kutumwa halafu naenda kufanya vitu vingine ,akatwambia tuongozane hadi kwa madam Rose

Kufika tulimkuta madam kakaa kulekule chumbani kwake kalia Sana macho yamevimba sana,yule Babu akasema nanukuu

"Wewe mtoto Ni mzuri Tena una um bo zuri kwani unamiliki vitu visivyofaa"

Madam akajibu nanukuu

"Hii kazi ya ualimu sijaipata kirahisi,japo kwa haya yalotokea naacha kazi na narudi kwetu"

Nakumbuka baba aliuliza huo uchafu aliouna mwanangu uko wapi?madam alikaa kimya tu,yule Babu akasema hamuwezi kuona kitu tena.tuokaondoka zetu

Naam shule ilifunga na hata ilipofunguliwa tuliambiwa madam Rose ameomba ahamishwe,Japo nyuma ya pazia inaonekana aliacha. Kazi

Lakini hata mimi mwaka ulofuata baba mkubwa alikuja kutembea kijijini ,katika kukagua maendeleo ya masomo yangu akavutiwa hivyo nikahamishiwa Dar es salaam

Share mkasa wako na wewe msomaji tuburudike,tuelimike na tujifunze
 
Back
Top Bottom