GE2025 Kama ulikuwa hujamuelewa Polepole kuhusu uhuni

GE2025 Kama ulikuwa hujamuelewa Polepole kuhusu uhuni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,931
Reaction score
7,829
Nyerere alisema mtu yeyote anayetaka kwenda ikulu kwa kutoa pesa anataka kwenda kufanya biashara ikulu.

Tuliona Mbowe mwenyekiti wa chadema akiingia ikulu kukutana na rais Samia akiwa mifuko ya gwanda lake la chadema bapa.

Kutoka picha zikaonesha mifuko ya gwanda la chadema limetuna. Mara tukasikia no reforms no election. Lissu kuchukua kiti hakua na utani. No reforms no election ikawa kweli sio usanii.

Tukaja mkutano mkuu ccm kumteua makamu mwenyekiti tukaona wahuni wakafanya vitu vyao tukapewa mgombea urais bila secretariat kuwatangazia wanaccm pazia limefunguliwa ugombea urais wanaccm wenye kutaka kugombea wajitokeze kuchukua form. Wanaccm wakashangaa mgombea kateuliwa kwenye mkutano wa kumteua makamu mwenyekiti.

Mzee Makamba akafanya vitu vyake kinyume na katiba wahuni wakapeta.

Ona sasa upinzani walivyodhibitiwa ili kunyimwa haki yao kugombea. Lissu akatupwa ndani kesi ya uhaini. Heche naye kiherehere cha kwenda Kenya akatupwa ndani. Mpina kugombea urais kupitia Act Wazalendo akatupwa huko.

Maamuzi ya mahakama Mpina agombee yakatupwa huko kwa amri ya mwanasheria mkuu. Yote uhuni tu.

Sasa tuje uchaguzi. Kutokana na kitisho cha maandamano siku ya uchaguzi na hasira ya wanaccm kunyimwa chaguo lao kuhusu mgombea urais idadi ya wapiga kura huenda hata haikufika asimia 30. Siku hiyo kukawa na maandamano ya fujo hayajawahi kuonekana nchini tokea kupata uhuru.

Sasa matokeo ya uchaguzi mtu anakuja anatuambia wamepiga kura watu milioni 31 na kwamba Samia kapata asilimia 97 ya kura sawa na wale madikteta wakabila Rwanda wanapataga asilimia 99. Kila mtu anashangaa anacheka.

Hata mwalimu mwanzilishi wa taifa wakati wa chama kimoja alikua hapati hesabu hiyo. Kwa mfano 1965 nyerere alipata asimia 95 ya kura na mwaka 1970 akapata asilimia 96.9 huku miaka yote wapiga kura wakijitokeza kwa zaidi ya asilimia 70.

Tumeona hasira kubwa ya wananchi kwa jinsi uchaguzi umebanangwa kwa tamaa ya mtu mmoja. Kila dalili tuna mfanyabiashara ndani ya ikulu. Baafa ya kuapa tunaona msururu wa magari ya kifahari Range Rover za kifahari lukuki wakati wanamapinduzi kina Ibrahim Traore wanaachana na ufahari tunaona ubadhilifu mkubwa. Wakati huohuo tukiwa hatujapata jibu kuhusu matakwa ya rais aliyepita Angela Kizigha arudishe mabilioni aliyopewa na hazina bila kuwasilisha mali ila anaonekana kwenye vilingo vya awamu hii karibu na mama.

Kwa ufupi hapakua na uchaguzi tanzania kwa hivyo uchaguzi urudiwe na vyama vyote vipewe nafasi sawa kufuatana na Katiba.
 
Back
Top Bottom