The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
SANDUKU LA AGANO
Nadhani ushawahi kusikia neno Sanduku la Agano, lakini huenda hujui hasa ni kitu gani. Sasa leo wacha nikujulishe kama ifuatavyo:
Sanduku la Agano lilikuwa ni sanduku takatifu ambalo Waisraeli waliamuriwa na Mungu kupitia Musa walitengeneze kufuatana na maagizo aliyowapa. Sanduku hilo lilikuwa na Ushuhuda, yaani zile Amri Kumi za Mungu zilizoandikwa kwenye mabamba mawili ya mawe.
Soma Biblia: (Kutoka 25:8-10, 16; 31:18).
Sanduku la Agano lilikuwa na pete nne za dhahabu juu ya miguu yake minne, ambapo miti ya mshita iliyofunikwa kwa dhahabu ilitiwa kwenye pete hizo ili kulibeba.
Soma Biblia: (Kutoka 25:10-21; 37:6-9).
Ni kuhani mkuu pekee aliyeruhusiwa kuingia sehemu hiyo siku moja kwa mwaka, kwenye Siku ya Upatanisho, ambapo aliweza kuliona Sanduku hilo.
Soma Biblia: (Kutoka 40:3, 21; Mambo ya Walawi 16:2; Waebrania 9:7).
Baada ya miaka kadhaa, Sanduku hilo lilihamishwa kutoka Hema na kupelekwa kwenye Hekalu la Sulemani.
Soma Biblia: (Wafalme 6:14, 19).
Soma Biblia: (Wafalme 8:9).
Soma Biblia: (Hesabu 7:9; 1 Mambo ya Nyakati 15:15; Kutoka 25:12-16).
Wakati wa kuhamisha Sanduku hilo, pazia lenye kusitiri sehemu takatifu lilitumiwa kulifunika.
Soma Biblia: (Hesabu 4:5-6).
Soma Biblia: (Mambo ya Walawi 16:2; Hesabu 10:33-36).
Makerubi walioketi juu ya Sanduku hilo walikuwa mfano wa gari la Mungu (Yehova).
Soma Biblia: (1 Samweli 4:4; Zaburi 80:1; 1 Mambo ya Nyakati 28:18).
Soma Biblia: (Mambo ya Nyakati 28:11).
Soma Biblia: (Yeremia 31:31-33; Waebrania 8:13; 12:24; Yeremia 3:16; Ufunuo 11:15, 19).
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro.
Nadhani ushawahi kusikia neno Sanduku la Agano, lakini huenda hujui hasa ni kitu gani. Sasa leo wacha nikujulishe kama ifuatavyo:
Sanduku la Agano lilikuwa ni sanduku takatifu ambalo Waisraeli waliamuriwa na Mungu kupitia Musa walitengeneze kufuatana na maagizo aliyowapa. Sanduku hilo lilikuwa na Ushuhuda, yaani zile Amri Kumi za Mungu zilizoandikwa kwenye mabamba mawili ya mawe.
Soma Biblia: (Kutoka 25:8-10, 16; 31:18).
UJENZI
Sanduku la Agano lilikuwa na:- Urefu wa mkono 2.5
- Upana wa mkono 1.5
- Kimo cha mkono 1.5
- Urefu: Sentimita 111
- Upana: Sentimita 67
- Kimo: Sentimita 67
Sanduku la Agano lilikuwa na pete nne za dhahabu juu ya miguu yake minne, ambapo miti ya mshita iliyofunikwa kwa dhahabu ilitiwa kwenye pete hizo ili kulibeba.
Soma Biblia: (Kutoka 25:10-21; 37:6-9).
MAHALI LILIPO
Sanduku la Agano liliwekwa sehemu patakatifu ndani ya Hema, ambalo lilikuwa linaweza kuhamishika na lilitengenezwa wakati uleule pamoja na Sanduku. Katika Hema hilo kulikuwa na pazia lililositiri sehemu takatifu zaidi ili pasionekane na makuhani pamoja na watu wengine.Ni kuhani mkuu pekee aliyeruhusiwa kuingia sehemu hiyo siku moja kwa mwaka, kwenye Siku ya Upatanisho, ambapo aliweza kuliona Sanduku hilo.
Soma Biblia: (Kutoka 40:3, 21; Mambo ya Walawi 16:2; Waebrania 9:7).
Baada ya miaka kadhaa, Sanduku hilo lilihamishwa kutoka Hema na kupelekwa kwenye Hekalu la Sulemani.
Soma Biblia: (Wafalme 6:14, 19).
VITU VILIVYOMO
Ndani ya Sanduku la Agano kulikuwepo:- Mabamba ya Mawe yenye Amri Kumi (Kutoka 40:20)
- Mtungi wa Dhahabu uliokuwa na Mana (Waebrania 9:4; Kutoka 16:33-34)
- Fimbo ya Haruni iliyochipuka (Hesabu 17:10)
Soma Biblia: (Wafalme 8:9).
UHAMISHWAJI
Sanduku la Agano lilibebwa na Walawi juu ya mabega yao kwa kutumia miti ya mshita. Miti hiyo haikuondolewa kwenye Sanduku hilo, hivyo Walawi hawakuhitaji kuligusa moja kwa moja.Soma Biblia: (Hesabu 7:9; 1 Mambo ya Nyakati 15:15; Kutoka 25:12-16).
Wakati wa kuhamisha Sanduku hilo, pazia lenye kusitiri sehemu takatifu lilitumiwa kulifunika.
Soma Biblia: (Hesabu 4:5-6).
UWAKILISHO
Sanduku la Agano lilihusianishwa na uwepo wa Mungu. Kwa mfano, wingu lilionekana juu ya Sanduku hilo, likiwa ishara ya baraka za Mungu kwa Waisraeli.Soma Biblia: (Mambo ya Walawi 16:2; Hesabu 10:33-36).
Makerubi walioketi juu ya Sanduku hilo walikuwa mfano wa gari la Mungu (Yehova).
Soma Biblia: (1 Samweli 4:4; Zaburi 80:1; 1 Mambo ya Nyakati 28:18).
MAJINA MBALIMBALI YA SANDUKU LA AGANO
Biblia inaliita Sanduku la Agano kwa majina tofauti kama:- Sanduku la Ushuhuda (Hesabu 7:89)
- Sanduku la Agano (Yoshua 3:6, 13)
- Sanduku la Yehova (2 Mambo ya Nyakati 6:41)
- Sanduku la Nguvu za Yehova (Wafalme 8:9)
Soma Biblia: (Mambo ya Nyakati 28:11).
JE, SANDUKU LA AGANO BADO LIPO?
Hakuna uthibitisho wa kisayansi au wa kihistoria kwamba Sanduku la Agano bado lipo. Biblia inaonyesha kuwa halihitajiki tena kwani Agano la Kale lilibadilishwa na Agano Jipya kupitia dhabihu ya Yesu Kristo.Soma Biblia: (Yeremia 31:31-33; Waebrania 8:13; 12:24; Yeremia 3:16; Ufunuo 11:15, 19).
JE, SANDUKU LA AGANO LILIKUWA NA NGUVU ZA PEKEE?
Hapana. Kuwa na Sanduku la Agano hakukuhakikisha ushindi au ulinzi wa Mungu. Kwa mfano:- Waisraeli walishindwa vitani dhidi ya jiji la Ai, licha ya kuwa na Sanduku hilo, kwa sababu ya dhambi zao (Yoshua 7:1-6).
- Walishindwa tena na Wafilisti kwa sababu ya uovu wa makuhani wao (1 Samweli 2:12; 4:1-11).
- Wafilisti waliliteka Sanduku hilo lakini walipatwa na majanga kutoka kwa Mungu, hadi walipoamua kulirudisha wenyewe (1 Samweli 5:11–6:5).
HITIMISHO
Sanduku la Agano lilikuwa moja ya vitu vya thamani kubwa kwa Waisraeli, likiwakilisha uwepo wa Mungu kati yao. Hata hivyo, kwa mujibu wa Agano Jipya, Sanduku hilo halihitajiki tena kwani agano jipya lilianzishwa kupitia Yesu Kristo.Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro.