Kama ukiokota mtoto fanya hivi

Kama ukiokota mtoto fanya hivi

30P

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2017
Posts
7,456
Reaction score
7,938
Habari wakuu,

Sasa hivi kumekuwa na idadi kubwa ya matukio ya watoto wenye umri wa miaka 2-4 kupotea. Mara nyingi wazazi au walezi ndio hubebeshwa mzigo huu wa lawama kwa kutokua makini na waangalifu kwa watoto wao.

Baadhi ya watoto hupatikana wakiwa hai na salama huku wengine hupatikana wakiwa wafu, wamebakwa, kulawitiwa na mengine mengi yenye kudhuru.

Kama umeshawahi kuokota mtoto ni kitu gani ulifanya ilikuhakikisha mtoto huyo anarejea salama kwa wazazi au walezi wake?

Mimi nimetumia njia ya jadi (kupita nyumba kwa nyumba) kuulizia kama wanaweza wakawa wanamfahamu badala ya kwenda kumripotisha polisi kuepuka usumbufu.

Nawasilisha.
 
Mtoto Wa miaka mingapi?

Kama ni kichanga hicho nabaki nacho, Ila kama ni kuanzia mwaka mmoja huyo trip ya kwanza kwa Mwenyekiti Wa mtaa ndio kwa kuanzia baada ya hapo kama hajajitokeza mwenye nae naendelea kukaa naye ili mradi nimeshatoa taarifa kwa Mwenyekiti sina haja ya kwenda Polisi.

Polisi atakwenda Mwenyekiti kuwa kuna Mtoto ameokotwa katika eneo lake. Hivyo mwenye Mtoto ajitokeze na asipojitokeza na-create bond yangu kwa hiyo Mtoto.
 
Utaratibu sahihi nionavyo mimi.....Toa taarifa polisi,wao wataangalia hali yake na kama utakuwa tayari kukaa naye huku wakimtafuta mzazi wake, watakurhusu
Lakini pia toa taarifa kwa mjumbe wa mtaa wako,majirani na serikali ya mtaa,hii ni kuepusha kuja kuambiwa mwizi au mchawi.
 
Hili ndio jibu sahihi kuliko yote...

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Mtoto Wa miaka mingapi?

Kama ni kichanga hicho nabaki nacho, Ila kama ni kuanzia mwaka mmoja huyo trip ya kwanza kwa Mwenyekiti Wa mtaa ndio kwa kuanzia baada ya hapo kama hajajitokeza mwenye nae naendelea kukaa naye ili mradi nimeshatoa taarifa kwa Mwenyekiti sina haja ya kwenda Polisi.

Polisi atakwenda Mwenyekiti kuwa kuna Mtoto ameokotwa katika eneo lake. Hivyo mwenye Mtoto ajitokeze na asipojitokeza na-create bond yangu kwa hiyo Mtoto.

Ha ha ha kwa raha zako mkuu
 
Bahati yako unatumia fake ID maana wadada wa siku hizi wangekutupia watoto nyumbani kwako mpaka ungekoma
 
usalama wako ni kuripoti polisi tu, maana vinginevyo unaweza ukajikuta kwwnye matatizo bila kutarajia, binadamu sio wema
 
Back
Top Bottom